Biashara niliyofungua Aprili 2022 nimeifunga Agosti 2024

Mr IQ

JF-Expert Member
Jun 23, 2015
871
997
Habari za majukumu wana JF,

Leo naleta mada hii iwe kama funzo kwanaotaka kuanza biashara au wanaofanya biashara.

Nianze kwa kwakusema biashara inaitaj mtu uwe na roho ngumu yaani usiwe na huruma.
Mambo yaliyochangia kufunga biashara Yangu:

1. Uaminifu. Binafsi ni mtumishi wa serikali, hivyo nahitaji kuwa na mtu/kijana atakaeweza kusimamia biashara, lakini kwenye biashara yangu ilikua ni mtiti, vijina sio waaminifu karne hii, ikitokea umewagundua tu wanachukua chao na kusepa. Na wanasepa kwa kukupa hasara.

2. Changamoto za mahusiano zilivuruga biashara yangu. Waswahili wana kwambia kosea vyoote ila usikosee kuoa hapa ni siwe msemji sana ila kama mke wako mgomvi ana, hasira na wivu uliopitiliza hutoboi mzee kila siku litaibuka jipya.

3. Nilifeli kwenye usimamizi. Mahali biashara ilipo na sehemu y kazi pana umbali mrefu hali hiyo ilinifanya nitumie siku za weekend kuangalia bishara inaendaje. Uhuru wa kijana from Monday to Friday ulifanya niwenapigwa za uso. Ilifika mahali mauzo ya wiki hayafikii hata pesa ya kulipa pango.

4. Aina ya biashara niliyofanya pia inaweza kuwa ni sababu kwasababu niya msimu, kuna msimu biashara haiendii kabisa inakua ngumu sanaa.

Ilifika mahali kodi ya pango natumia salary yangu na hadi sasa kodi ya TRA imenishida kulipia. Leo naandika barua ya kusitisha kuwa mlipakodi kwenye biashara yangu.

Mpango mkakati wa kuanza tena biashara.
Ninampngo wa kubadilisha biashara ila najipa kwanza pumziko la mwaka mmoja ivii... kupunguza machungu ya hasara niliyoingia kwakipindi chote cha biashara.
 
Habari za majukumu wana jf. Leo naleta mada hii iwe kama funzo kwanaotaka kuanza biashara au wanaofanya biashara.
Nianze kwa kwakusema biashara inaitaj mtu uwe na roho ngumu yaani usiwe na huruma.
Mambo yaliyochangia kufunga biashara Yangu:
1. Uaminifu. Binafsi ni mtumishi wa serikali, hivyo nahitaji kuwa na mtu/kijana atakaeweza kusimamia biashara, lakini kwenye biashara yangu ilikua ni mtiti, vijina sio waaminifu karne hii, ikitokea umewagundua tu wanachukua chao na kusepa. Na wanasepa kwa kukupa hasara.
2. Changamoto za mahusiano zilivuruga biashara yangu. Waswahili wana kwambia kosea vyoote ila usikosee kuoa hapa ni siwe msemji sana ila kama mke wako mgomvi ana , hasira na wivu uliopitiliza hutoboi mzee kila siku litaibuka jipya.
3. Nilifeli kwenye usimamizi. Mahali biashara ilipo na sehemu y kazi pana umbali mrefu hali hiyo ilinifanya nitumie siku za weekend kuangalia bishara inaendaje. Uhuru wa kijana from Monday to Friday ulifanya niwenapigwa za uso. Ilifika mahali mauzo ya wiki hayafikii hata pesa ya kulipa pango.
4. Aina ya biashara niliyofanya pia inaweza kuwa ni sababu kwasababu niya msimu, kuna msimu biashara haiendii kabisa inakua ngumu sanaa.
Ilifika mahali kodi ya pango natumia salary yangu na hadi sasa kodi ya TRA imenishida kulipia. Leo naandika barua ya kusitisha kuwa mlipakodi kwenye biashara yangu.
Mpango mkakati wa kuanza tena biashara.
Ninampngo wa kubadilisha biashara ila najipa kwanza pumziko la mwaka mmoja ivii... kupunguza machungu ya hasara niliyoingia kwakipindi chote cha biashara.
Hii kitu imewahi nikuta usiombe aisee
 
Maboss wengi mnafeli kwenye usimamizi. Ukiachana na ninyi waajiriwa kuna wengine wapenda uboss hupendelea kuweka vijana hata kama anao uwezo wa kukaa mwenyewe..

Biashara ikielekea kubiduka kifo cha mende huona aibu kusimama wenyewe wajitafute tena, huamua kufunga kukwepa aibu ya kuuza mbao tupu dukani.
 
Nakumbuka mimi biashara yangu ilikufa kabla ya kuanza. Ilikuwa nianze kuuza kuni sokoni kwa morombo. Mtaji ulikuwa 130k. Ni kulipia tu lori then mnaenda kwenye pori fulani ukipita Mirongoine mnaokota kuni na kuzipakia. Ile ndo tunamalizia kupakia tukaona watu wa maliasili wako jirani upande ambao tungepita muda wa kurudi. Ikabidi tuziache tu kuni maana maliasili wangetufanya kitu mbaya sana endapo wangeziona kuni. Hiyo biashara nikaachana nayo mazima na kurudi town lori tupu.
 
Habari za majukumu wana JF,

Leo naleta mada hii iwe kama funzo kwanaotaka kuanza biashara au wanaofanya biashara.

Nianze kwa kwakusema biashara inaitaj mtu uwe na roho ngumu yaani usiwe na huruma.
Mambo yaliyochangia kufunga biashara Yangu:

1. Uaminifu. Binafsi ni mtumishi wa serikali, hivyo nahitaji kuwa na mtu/kijana atakaeweza kusimamia biashara, lakini kwenye biashara yangu ilikua ni mtiti, vijina sio waaminifu karne hii, ikitokea umewagundua tu wanachukua chao na kusepa. Na wanasepa kwa kukupa hasara.

2. Changamoto za mahusiano zilivuruga biashara yangu. Waswahili wana kwambia kosea vyoote ila usikosee kuoa hapa ni siwe msemji sana ila kama mke wako mgomvi ana, hasira na wivu uliopitiliza hutoboi mzee kila siku litaibuka jipya.

3. Nilifeli kwenye usimamizi. Mahali biashara ilipo na sehemu y kazi pana umbali mrefu hali hiyo ilinifanya nitumie siku za weekend kuangalia bishara inaendaje. Uhuru wa kijana from Monday to Friday ulifanya niwenapigwa za uso. Ilifika mahali mauzo ya wiki hayafikii hata pesa ya kulipa pango.

4. Aina ya biashara niliyofanya pia inaweza kuwa ni sababu kwasababu niya msimu, kuna msimu biashara haiendii kabisa inakua ngumu sanaa.

Ilifika mahali kodi ya pango natumia salary yangu na hadi sasa kodi ya TRA imenishida kulipia. Leo naandika barua ya kusitisha kuwa mlipakodi kwenye biashara yangu.

Mpango mkakati wa kuanza tena biashara.
Ninampngo wa kubadilisha biashara ila najipa kwanza pumziko la mwaka mmoja ivii... kupunguza machungu ya hasara niliyoingia kwakipindi chote cha biashara.
2026 utaifungua una nyota ya 2.4.6....
 
Kwakuwa umeshajua kilichokukwamisha,sasa unaweza kufanya tena vizuri zaidi,ila hapa no.2 kuwa napo makini sana, wanasema usicheke na nyani utaambulia mabua.Ninamfahamu jamaa alikuwa na duka limesheheni vitu kibao ni kama mini supermarket,alikuwa anafanya mwenyewe,ikatokea jamaa akapata shuguli nyingine akamuachia mkewe yeye akawa anakuja akipata nafasi,huwezi amini biashara iliyumba vibaya mno,mke hajui customer care,full kunununa na kufokea wateja,aliposhtuka wateja wamemkimbia na biashara imeshuka,ikabidi arudi mwenyewe kijiweni,mpaka sasa yuko vizuri sana na mke sikumuona tena pale dukani,maana ilifikia mahali mpaka walikuwa wanafokeana live na mkewe pale dukani...
 
2. Changamoto za mahusiano zilivuruga biashara yangu. Waswahili wana kwambia kosea vyoote ila usikosee kuoa hapa ni siwe msemji sana ila kama mke wako mgomvi ana, hasira na wivu uliopitiliza hutoboi mzee kila siku litaibuka jipya.

Ni mwanamke ambae alikuwa anataman kwenye biashara yangu nisiwe na wateja wanawake,akija mwanamke ninaefahamiana nae ni demu wangu,nikichelewa kurudi nilikuwa na wanawake,ukimuachia yeye mara anawanunia watu yaan shida tupu,haelewani na washikaj zangu
 
Aliposema Mheshimiwa Dr. Mchungaji Eliona Kimaro kwamba kufanya biashara au ajira na vijana wa kikristo ni ngumu, maana ni wezi na ni wavivu mlimnyanyasa, mkampa aibu,

Haya tuambie wewe.

Ni hivi kila msimu alikuwa anauza, ila akiuza simu yako kesho ananunua nyingine anaweka kwenye shelf, faida anatia mfukoni,

But anyways usiogope, just try again
 
Back
Top Bottom