View attachment 109102
1972 Hawa si wachezaji wa Ngumi bali ni wachezaji wa Taifa Stars wakikaguliwa na Rais wa Sudan wakati huo.
Mkuu hii ilikuwa 1972 sudan wakachezea kichapo cha 3-0 ilikuwa Timu inatisha sana acha sahizi mashalobalo kibao.
Anaye mtmbulisha Rais Nimeir ni Nahodha wetu Abdulhaman Jumaa!
Kutoka kushoto ni beki Abdallah Mohamed"CHUMA",anayefutia ni beki Said Zimbwe;na anayefutia ni mshmabuliaji Abdallh Kibaden Mputa;huyo anayeonekana kichwa tu kama nipo sahihi ni mshambuliaji Juma Masementi!
Hao walikuwa wana ujua mpira mno na miili mikubwa ukikutana nao utadhani wacheza mieleka;siku hizi wachezaji wetu hawana kabisa miili!
Said Zimbwe? mbona kama miaka ya 80 (mpk early 90's) mimeshawahi kumuona akicheza. are u sure? Said Omar Zimbwe, right? alikuwa beki , ana kichwa "kirefu" hivi. tena beki wa pembeni km Garry Neville
Wa kwanza kutoka kushoto ni Abdallah Chuma alikuwa ni Centre Half (No 5) wa timu ya taifa kwa miaka 10, alikuwa akitokea timu ya Bandari Mtwara, anafuatia Zimbwe kutoka moja ya timu za Tanga sina uhakika kati ya Costal Union na African Sports, anafuatia Kitwana Manara Centre Forward wa timu ya Yanga na Taifa, anayetambulisha wenzake ni Abdulrahman Juma alikuwa anacheza namba 6 Yanga na timu ya taifa. Anaeonekana kichwa tu ni Abdallah Kibaden alikuwa anacheza namba 10 Simba na timu ya taifa