Tukumbuke fadhila za mashujaa wetu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
TUKUMBUKE FADHILA ZA MASHUJAA WETU.jpg
TUKUMBUKE FADHILA ZA MASHUJAA WETU 2.jpg


Mzee Mwinjuma Ali Nkonga ambaye ni miongoni mwa Watanganyika waliopigania Uhuru Wa nchi hii kabla ya Uhuru akiwa amesahauliwa na mwajiri wake ,ambapo anaishi kijiji cha Msente Handeni Tanga,ni vema sasa Serikali ikawaangalia Wazee hawa ambao wanaishi Kwa Mateso makubwa bila ya msaada Wa waajiri wao kwani walijitolea Kwa nguvu zao zote.
 
Mimi kijijini kwetu Mzee moja R I P namhifadhi jina. Alizunguka na makaratasi, kwenda wilayani kutafuta haki za mwanaye aliyefia vitani bila mafanikio, mpaka kifo chake. Watu wengi sana wamesahauliwa na hasa ukiwa nje ya system.
Ujumbe umesha kwenda kwa wanaohusika iliyobakia ni utekelezaji wake tu huo ujumbe.
 
Ndio maana vijana wengi saivi ukiwambia habari za uzalendo wanakushanga.unaipenda nchi kwa moyo wako wote badae nchi yako inakupotezea
 
Ndio maana vijana wengi saivi ukiwambia habari za uzalendo wanakushanga.unaipenda nchi kwa moyo wako wote badae nchi yako inakupotezea

Nadhani una shida kidogo ya ' Concept ' nzima ya ' Patriotism ' Mkuu na si vibaya ukarejea tena katika ' Makabrasha ' yako ukajielimisha zaidi. Kwa kukusaidia tu kwa haraka haraka ukitaka kuielewa na ' Kuishiba ' hii dhana nzima rejea ile Kauli ya aliyewahi kuwa Rais wa Marekani JF Kennedy aliposema kwamba " Usiseme Marekani imekufanyia nini bali sema Wewe umeifanyia nini Marekani ".

Mwisho kabisa nikusaidie tu kukuambia ya kwamba ' Mzalendo ' wa kweli kwa nchi yake huwa hasubiri Shukrani au Akhsante bali siku zote hujivunia na hufurahia kuona juhudi zake kama Mtanzania zimeweza Kuifikisha hapa ilipo na kama ni ' thawabu ' za alichokifanya basi atazipata kutoka Kwake Mola / Maulana.

Tukienda kwa mfumo huu kwamba kila Mtanzania aliyeifanyia jambo fulani nchi hii akumbukwe tu nadhani basi hata Mimi na Wewe pia tunatakiwa tukumbukwe kwani yawezekana tumechangia kitu fulani ' positive ' kwa nchi yetu hii. Sema tu labda Serikali ije na mtindo wa kuwafungulia Bima za Afya na kidogo kuboresha Pensheni zao endapo tu pale Uchumi wa nchi utaruhusu. Na msisahau kwamba kuna wengine walipewa vitu vingi tu enzi zao ila walizifuja kwa starehe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom