Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,525
- 1,521
Kwa miaka karibu 20, Tanzania imekuwa katika mchakato wa siasa za vyama vingi. Katika miaka hii 20, damu imemwagika, dhuluma imetokea, uonevu na unyanyasaji umeendelezwa, kauli za kudai haki na usawa zimeendelea kupuuzwa kila mwaka na CCM kimeendeleza utawala wa kibabe kwa kukataa kuanzisha mchakato wa kuundwa kwa Katiba mpya na hata kupuuzia kabis akilio cha kuwa na tume huru ya Uchaguzi.
Zaidi ya hayo, Serikali ya CCM imetumia vyombo vyake vya Serikali kama TISS, Polisi, Jeshi, Mamlaka ya Kodi na taasisi nyingine kisiasa na kwa manufaa yake kwa kudhibiti na kuunyanyasa ule msukumo na wimbi la mfumo wa vyama vingi vya kisiasa na demokrasia.
CCM wamehakikisha kuwa wanapanda mbegu chafu ya kuuonyesha Upinzani kama ni ushetani an udhalimu wa hali ya juu, kiasi cha kuwatishia Watanzania kuwa wapinzani wakipewa dhamana ya kuongoza Tanzania, yaliyotokea Rwanda, Congo, Somalia na kwingineko kuliko na machafuko yatatokea Tanzania.
Watazania walichosahau kuwauliza CCM ni hili, ikiwa Upinzani wa leo iwe CUF, Chadema, TLP, NCCR au chama kingine ambacho si CCM kikawa madarakani kuongoza Taifa letu, ni nani basi ambaye atachukua upanga na majambia kuhatarisha amani yetu na kuleta vita vya ndani? Je hili haliashirii kwamiaka yote kuimbwa wimbo huu kuwa CCM kamwe haitakuwa tayari kukubali kauli za Wananchi kuikataa na kuinyima dhamana ya kuongoza Tanzania?
Je ni sababu hii ya kung'ang'ania madaraka na uchu wa madaraka imefiikia CCM kutafuta mbinu za kila aina katika kila uchaguzi kuhakikisha kuwa inatabngazwa mshindi kwa hali na mali au kama kule Mwanza walikodai "kaza buti hata kwa nguvu" ni lazima CCM ishinde?
Ni kutokana na fikira hizi potofu za kung'angania madaraka na kujiopna kuwa wao CCM ndio Alpha na Omega wa siasa za Tanzania ndipo palipofikia Mwenyekiti wake ambaye alitangazwa kuwa mshindi wa kugombea Urais, Bwana Jakaya Kikwete kutangaza wakati wa kampeni kuwa Upinzani ni nakala.
Haiyumikiniki kuwa juzi wakati wabunge wa Chadema waliposimama na kutoka nje ya Bunge wakati akihutubia, Bwana Kikwete alithubutu kutoa kauli ambayo ni wazi ya kitisho kwa Upinzani.
Nanukuu na kumnukuu kauli yake
Ili kuonyesha uroho wao wa madaraka na hata kutokujali maslahi ya Taifa zima na kwa manufaa ya wote, Chiligati amefikia kutoa kauli kama hii ambayo inaashiria wazi kuwa CCM haiko tayari kukaa chini na kufanya haki na kukaa na wenzao kuunda katiba mpya. Nikimnukuu Chiligati amesema hivi
Alichokificha kukisema Chiligati na hata Kikwete an Makamba ni kuwa Uchaguzi ulikuwa na madoa na hivyo uhalali wa Serikali yake ni wa mashaka. Wanachokificha ni kuwa haki ilikanyagwa na kufumbwa mdomo kwa kigezo cha Katiba na Tume zimesema hivyo hakuna cha kubadilisha.
Na ndio maana kitendo cha Chadema kutoka nje ya hotuba ya Kikwete kama Rais akihutubia Bunge kimewashitua sana na kila mtu anatafuka kuleta ujuzi wa kisheria au kikatiba kulaani kitendo cha Chadema huku wakisahau kuwa hakuna mahali popote kwenye Katiba au Sheria panaposema ukipingana na Rais au ukatoka nje ya mkutano wake kama kitendo cha kumpinga ni ukosefu wa nidhamu, uvunjaji wa sheria au kuidharau Kariba.
Kwa haki waliodharau Katiba ni CCM kwa kuipuuzia pale inaposema wazi kuwa haki lazima iwe sawa kwa kila Mtanzania na Serikali imepewa dhamana ya kutengeza mazingira sawa kwa kila mtu bila kujali dini, elimu, jinsia, umri au utashi na itikadi ya siasa.
Kwa kuwa ni utamaduni wa Mwenyekiti kushika hatamu, hata yale makombo ya Zidumu Fikra za mwenyekiti, leo hii Makamba anadiriki kuwakoromea Chadema, Chiligati anawakebehi na kudai ni ukosefu wa nidhamu, mbona hawakusema lolote pale Wajumbe wa NEC na CC kutoka Zanzibar alipogomea kikao kule Butiama mwaka jana?
Na hao wote wanojiita Wasomi na wataalamu wa Sheria ambao wanakilaani kitendo cha Chadema, je wanalaani kwa misingi ipi?
Je wao hawatampa hifadhi mtoto au mke anayenyanyaswa na kupigwa na Baba Mume mwenye nyumba?
Kama ni kutaka suluhisho na kuepusha mgogoro wa kisiasa na kikatiba, basi CCM ingefanyia kazi mabadiliko haya miaka 150iliyopita na isingejilazimisha kushinda kuule Zanzibar au huku Bara. Ama isingelitumia Polisi, TISS, TRA, Msajili wa Vyama au Tume ya Uchaguzi kuendeleza mfume wake dume wa kuongoza kwa mabavu.
Kama Uchaguzi huu haukutoa mwangaza kwa CCM kubadilika na kufanya kama walilofanya kwa CUF kule Zanzibar, basi kitendo cha Chadema kuondoka Bungeni kinawapa Watanzani amatumaini kuwa CCM na Rais wa Jamhuri ni watu wa kawadia na si Miungu ya kuogopewa.
CCM wamelewa Madaraka na wanajiona Miungu waabudiwe na kunyenyekewa. Ndugu Mtanzania, kura yako ya hapana na Chadema kutoka nje ya Bunge wakati Rais akihutubia Bunge ni jambo la kawaida na ni demokrasia ya kweli.
Wapimeni Chadema kwa uwezo wao wa kazi na si kusikiliza kejeli, vijembe na vitisho kutoka CCM.

Rais Kikwete alikatiza hotuba yake, akanyamaza huku uso wake ukisononeka; akawa ameduwaa, akakohoa kidogo, huku wabunge wa CCM wakipiga makofi kuwazomea CHADEMA; na baadaye alitoa kauli ya kejeli akisema, Hata wasionichagua hawana serikali nyingine ni hiihii. Watakwenda, watarudi, hawana mwingine wa kumwomba yao yatimie zaidi ya serikali ya CCM ambayo mie ndiye rais wake.
Ili kuonyesha uroho wao wa madaraka na hata kutokujali maslahi ya Taifa zima na kwa manufaa ya wote, Chiligati amefikia kutoa kauli kama hii ambayo inaashiria wazi kuwa CCM haiko tayari kukaa chini na kufanya haki na kukaa na wenzao kuunda katiba mpya. Nikimnukuu Chiligati amesema hivi
Waangalizi wa uchaguzi walishatoa taarifa kwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki, sasa iweje CHADEMA peke yao kutotambua matokeo kama si uchochezi unaoweza kusababisha uvunjaji wa amani na kuleta vurugu nchini? alihoji Chiligati katika taarifa hiyo.
Alisema kwa mujibu wa sheria na Katiba ya nchi, matokeo ya Rais yakiwa yametangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hayapaswi kuhojiwa na mahakama wala chombo chochote, hivyo rais yuko madarakani kwa matakwa ya Katiba hiyo. Sasa madai ya CHADEMA kwamba iundwe Tume Huru ya Uchaguzi ichunguze nini?....Nia yao wanataka tuache kazi ya kushughulikia maendeleo ya wananchi ili tuingie katika mgogoro wa Kikatiba utakaodumu kwa muda mrefu na kuiingiza nchi katika misuguano na mzozo wa kisiasa? aliuliza.