Cicadulina
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 974
- 2,366
Kwa faida tu ya wasomaji, ngoja nieleze historia fupi ya wimbo huu. Katika dunia nzima, hasa Afrika Kusini kwenyewe ulikoanzia, unajulikana kama “Nkosi Sikelel’ iAfrika” – maneno ya lugha ya ki-Xhosa, yenye maana ya “Mungu Ibariki Afrika.”
Mtunzi wake anaitwa Enoch Sontonga, aliyekuwa mwalimu katika shule moja ya misheni ya Kimethodisti, Johannesburg, Afrika Kusini.
Aliutunga ukiwa kama utenzi mwaka 1897. Uliimbwa kwa mara ya kwanza hadharani mwaka 1899 katika ibada ya kuwekwa wakfu mchungaji Boweni, wa Kanisa la Methodist.
Kwaya ya Sontonga na kwaya nyinginezo zikawa zinauimba mara kwa mara katika matukio jijini Johannesburg na Natal. Watu wakaupenda.
Mnamo Januari 8, mwaka 1912, katika mkutano wa kwanza wa Chama cha Wazawa wa Afrika Kusini (SANNC), mtangulizi wa ANC, wimbo huo uliimbwa mara baada ya sala ya kufunga mkutano.
Mwaka 1925, ANC ikauchukua kama wimbo wake rasmi ulioimbwa mwishoni mwa mikutano yake. Tangu hapo, wimbo huo umejulikana nje ya Bara la Afrika kama wimbo wa ANC, kwani ulikuwa ukiimbwa katika mikutano ya ANC katika harakati za ukombozi.
Harakati hizo ndizo zilifikisha wimbo huo hadi kwetu. Nasi tulipopata uhuru, tukauchukua kama wimbo wa taifa, tukautafsiri kwa Kiswahili, tukapunguza baadhi ya aya na kuubakiza kama ulivyo leo.
Zambia nao walifanya hivyo. Namibia pia waliutumia. Zimbabwe nao waliuiga, lakini baadaye “walipopata akili” wakautema, wakatunga wimbo wao.
Kwa kipindi kirefu, Afrika Kusini ilikuwa na “nyimbo mbili za taifa.” Mmoja ulijulikana kama wimbo rasmi na mwingine, usio rasmi.
Wimbo rasmi (uliotumiwa na serikali ya makaburu) uliitwa kwa jina la Die Stem (ki-Afrikaans), yaani Wito wa Afrika Kusini; na usio rasmi (uliotumiwa za wanaharakati wa ANC), ndio huo Mungu Ibariki Afrika.
Siku ANC iliposhinda uchaguzi wa kwanza kidemokrasia mwaka 1994, nyimbo hizo mbili zikatangazwa kuwa nyimbo rasmi za taifa, lakini mwaka 1996 ziliunganishwa; yakachukuliwa maneno huku na huku, ghani ikabaki ile ile ya wimbo wa ANC, ukakarabatiwa na kuwa kama ulivyo leo.
Kwa Afrika Kusini, Nkosi Sikelel’ iAfrika, kabla na baada ya uhuru, ni ishara ya uhuru na mapambano ya ukombozi wao. Unaimbwa katika lugha mbalimbali Kixhosa, Kiingereza, Kisesotho na Kiafrikaans.
Maneno yaliyo katika aya ya kwanza yaliandikwa na mtunzi mwenyewe (Enoch) katika lugha yake ya Xhosa. Mwaka 1927, aliyekuwa mmoja wa washairi maarufu wa nchi hiyo, Samuel Mqhayi, aliongeza aya nyingine saba katika lugha hiyo hiyo.
Kabla ya hapo, mwaka 1923, Solomon Plaatje, mmoja wa waandishi mahiri nchini humo, ambaye pia alikuwa miongoni mwa waasisi wa ANC, ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuurekodi wimbo huo katika studio jijini London, akisindikizwa na muziki wa piano uliopigwa na Sylvia Colenso.
Mwaka huo huo, kiwanda cha uchapaji cha Lovedale Press, katika Jimbo la Eastern Cape, kilichapisha nakala yenye aya zote katika kijitabu. Juni 11, 1927, wimbo huo ulichapishwa katika gazeti la Umtetela Wa Bantu, ukaingizwa pia katika kitabu cha ushairi cha Kixhosa kwa ajili ya kuwafundishia watoto shuleni.
Wimbo huo pia uliingizwa rasmi katika kitabu cha nyimbo za Kixhosa kwenye Kanisa la Wapresbyteri kilichojulikana kama Ingwade Yama-culo Ase-rabe, mwaka 1929. Mwaka 1942, Moses Mphahlele, alichapisha nakala nyingine za wimbo huo katika lugha hiyo na kuzisambaza ili umma ukariri vema maneno yake.
Kwaya ya Ohlange Zulu, ya Mchungaji John L. Dube, ndiyo iliyokuza wimbo huo, kwa kuuimba mara kwa mara katika matamasha mbalimbali jijini Johannesburg.
Taratibu ukawa wimbo maarufu katika mikusanyiko ya kidini, kijamii na kisiasa; badaye ukarekodiwa pia na wasanii kina Ladysmith, Black Mambazo, Boom Shaka na Mahotella Queens.
Historia hiyo pekee inaonesha kwamba sisi bado hatuna wimbo. Kama tunavyoimbiwa na wasanii wa CCM kwamba “CCM ina wenyewe,” basi tuna sababu ya kuamini pia kwamba hata wimbo huu tunaouita wa taifa, una wenyewe – na wenyewe ni Afrika Kusini. Nadhani Wazimbabwe waliligundua hilo mapema. Wakaachana nao. Sisi tunangoja nini?
Ni bahati mbaya kwamba vijana wale waliobishana nami hawakuwa wanajua historia ya wimbo huo kama nilivyoieleza hapa. Vinginevyo, walikuwa na hoja; na wangetuaibisha. Tuna wasanii wa kutosha kutunga nyimbo zetu.
Watunge. Kama hatutaki mpya, basi tuchukue zilizopo, zinazoeleza kwa kina historia na utaifa wetu, tuzifanye rasmi nyimbo zetu za taifa, kwani huu tunaoimba sasa si wimbo wetu.
Kwa hisani ya Ansbert Ngurumo