Tukta, siasa na mustakabali wa "nji" hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukta, siasa na mustakabali wa "nji" hii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzito Kabwela, Mar 12, 2010.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Mara ya kwanza sikuamini kama kweli TUCTA wamedhamiria kutomwalika Rais na zaid wametangaza MGOMO wa wafanyakazi wote Tanzania.

  Mimi ni mfanyakazi pia, sina tatizo na sababu walizozitoa kujustfy mambo hayo MAZITO huenda kwa nyakati tulizo nazo na tunazoelekea zinaweza kuleta manufaa.

  Tatizo nilionalo hapa ni SIASA kutawala zaidi kuliko utashi wa kusaidia maendeleo. Viongozi wa TUCTA nao wamekaa kisiasa na iliwahi kuelezwa kuwa katika vyama wanachama wanaoifanya TUCTA iwepo viongozi wao wamegawanyika kiitikadi za vyama.

  Kutokana na hilo nashawishika kuamini kuwa hakuna UTASHI wa pamoja katika hili la kutomwalika Rais na la Mgomo.

  Sasa basi, endapo option hii waliyoichagua isipoleta mafanikio yoyote (serikali ikiendelea kufanya sanaa) TUCTA watachukua uamuzi gani wa juu zaidi ya huu?

  Na suala la kumobilize watu wagome likishindikana (nategemea kuwa hivyo)hawaoni kuwa watakuwa wamenunua dharau kwa bei rahisi?

  Tunajifunza nini na tunawafundisha nini watoto na vizazi vijavyo jinsi ya kudai haki zetu?

  Je, ni kweli TUCTA walikosa njia mbadala za kumaliza mgogoro huo hadi kukimbilia kushawishi na kuamua hivyo?

  Na endapo TUCTA wakafanikiwa (naamini ni muujiza tu) ni nini madhara yake kiuchumi na kijamii?

  Ni kweli TUCTA haiendeshwi kisiasa?
  Wana JF nisaidieni tafadhali
   
 2. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Nadhani wewe ndio unaleta siasa hapa! Mgomo maana yake ni nini? Kwamba katika njia za kawaida za majadiliano mmeshindwa kufikia mwafaka aidha upande mmoja hautaki kukubaliana na hoja ya msingi ya upande mwingine, Kinachofanyika ni kugoma! Mimi naona wanahaki ya kugoma Serikali hii ilipoingia madarakani ilikuja kisayansi zaidi ikaundwa tume kutathimini mishahara ya wafanyakazi mapendekezo yakatolewa..... and that was it! so wacha wagome........
   
Loading...