Tukomalie kudai risiti tunapofanya manunuzi

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,273
Reaction score
25,297

Kama ilivyo kwenye vita ya kupambana na rushwa na ufisadi, hili kwake halina mjadala, na kimsingi ni suala jema.

Ni suala jema kwa sababu kodi inayokusanywa na serikali ndiyo inayotumika kugharimia shughuli zake mbalimbali za kuwapatia huduma za msingi wananchi.

Kwenye baadhi ya nchi, pamoja na kuwa kulipa kodi ni suala la kisheria kwa mwananchi yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, lakini pia kulipa kodi ni wajibu wa kiraia.

Raia wema huona fahari kulipa kodi, kwa kuwa wanajua inaenda kugharimia shughuli kwa ajili ya ustawi wao.

Rais Magufuli ameendelea kuhimiza wananchi walipe kodi, kupitia majukwaa mbalimbali.

Amenukuliwa kupitia vyombo vya habari, akihimiza wananchi wenye sifa ya kulipa kodi wafanye hivyo.

Kwamba hata pale wanapoenda kufanya manunuzi ya bidhaa dukani ama kulipia huduma yoyote ile ya kibiashara, amehimiza wananchi wadai risiti.

Kwamba katika kila bidhaa ama huduma inayolipiwa, kuna asilimia ya serikali inayobakia ambayo inapaswa kwenda serikalini kwa ajili ya kugharimia shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Mjadala unaona pengine kuna baadhi ya watu hushangaa wanaposikia serikali ikishupalia watu walipe kodi.

Ieleweke kwamba, serikali ikiwa ni pamoja na mihimili mingine ya dola kama vile Bunge lenye jukumu la kutunga sheria na Mahakama yenye jukumu la kutafsiri sheria, pamoja na idara zake mbalimbali, zinahitaji fedha ili ziweze kutimiza majukumu yake barabara.

Mbali na fedha kwa ajili ya uendeshaji wa mihimili hiyo, kunahitajika fedha za kuwalipa watumishi wa serikali, wabunge, majaji na mahakimu, na yote hiyo inatokana na kodi inayokusanywa na serikali kutoka kwa walipa kodi.

Kuna kodi za aina mbalimbali, kuanzia ile ya mapato, ambayo kimsingi mfanyakazi yoyote hulipa kutegemeana na mshahara wake.

Kwamba kuna asilimia ambayo hukatwa na kupelekwa hazina, kwa ajili ya shughuli za kiserikali.

Kuna kodi ya majengo au mali isiyohamishika ambayo hulipwa kutokana na thamani ya mali ama jengo lenyewe.

Aidha, kuna kodi ya mauzo ambayo Dk.Magufuli amekuwa akiisisitiza mara kwa mara, inayopatikana pale mtu anapoenda kununua bidhaa dukani ama huduma sehemu panapouzwa huduma.

Kwa kila bidhaa inayonunuliwa, kuna asilimia inayokatwa na muuza duka ama mtoa huduma kama kodi ya serikali.

Hata hivyo, Mjadala unaona kwamba, pamoja na juhudi zote zinazoonyeshwa na Dk. Magufuli za kuhimiza wananchi kudai risiti pale wanaponunua bidhaa dukani, bado mwitikio uko katika kiwango cha chini.

Nasema hivyo kwa sababu, Mjadala umekuwa akishuhudia wananchi wengi wanaoenda kununua bidhaa kwenye baadhi ya maduka, tena mengine ya jumla jumla, wakiwa wanatoka bila ya risiti.

Kimsingi, kitendo hicho hakina maelezo mengine zaidi ya kuwa ni cha kukwepa kodi.

Ni cha kukwepa kodi toka kwa mwananchi mwenyewe aliyenunua bidhaa na akaacha kudai risiti, lakini vilevile kwa muuzaji.

Hali hii haiko kwenye biashara za maduka yanayouza bidhaa tu, bali hata kwenye maduka ya dawa.

Kimsingi kitendo hiki ni cha kumuangusha rais wetu mwenye dhamira ya kuona wananchi wakifaidika na keki ya taifa kupitia huduma za elimu, afya, maji, miundombinu, ulinzi na usalama, masoko na zinginezo.

Nimesema kwamba suala la kulipa kodi katika nchi zingine ni la kisheria na wajibu kama ilivyo hapa kwetu.

Pengine tofauti iliyopo kwa sasa ni kuwa Dk. Magufuli, anajaribu kupandikiza kwa wananchi moyo wa kulipa kodi ili waone kuwa ni wajibu wao kama raia.

Ni kwa misingi hiyo ndipo Mjadala unapowaasa wananchi kudai risiti kwa kila bidhaa ama huduma wanayonunua ili kodi yote ya serikali iweze kupatikana kwa ustawi wa taifa.

Chanzo: Nipashe
 
Hivi hadi wauza majeneza wanatakiwa kua na EFD?
 
Watu hawawezi changia huu uzi,

Wabongo wanataka serikali iwafanyie kila kitu wakati hawataki kuisaidia serikali ktk ufanyaji kazi wake.
 
Ushauri mzuri. Binafsi nalipa kodi vizuri. Nashangaa kwa nini tusilipie kodi ndoa
 
Kodi ikitumika vizuri,wananchi watalipa kodi bila shurti. Sio kumwekea ulinzi bashte zaid ya makamu wa rais, kujenga uwanja wa ndege sehem ambako hamna ulazima, matumizi kutoizinishwa na bunge, hasara za fidia ambazo hazieleweki nk. Tumieni hera za walipa kodi vizuri msikimbilie tu kulaumu walipakodi
 
Serekali ifanye kazi zake yenyewe kama ambavyo inavyofanya ktk chaguzi* Tusisumbuane* Wakachukue kodi mimi nikadai Risiti???" Ili iweje? Kazi yakudai risiti kwenye kilo ya sukari mimi sina huo muda wakupoteza, cham singi kama hawatoashi waajiri vijana wawasaidie
 
Kodi zenyewe tunalipa lakini viongozi wetu wanazitumia kwa dharau wanajenga kwao tu nakujinunulia magari ya kifahari mahospitali hayana dawa mashule madawati hadi tuchangishane tena, mitaani tunapigwa na mabomu ya machozi magari ya washa washa yanapita kila mara kututisha, tuna watendea mema lakini wanatulipa mabaya.
 
Kodi inalipwa sana na wananchi .....tatizo matumizi ya kodi inayolipwa wananchi hawaioni!matumizi ya kodi yetu ni mabaya?
Naomba niulize Swali Hivi tanzania tuna tax return?maana Kwa baadhi yetu tuliyobahatika kutembea tumeona wenzetu huko mwananchi kila baada ya muda fulani anarudishiwa asilimia fulani ya kodi aliyolipa!hii kitu sijawahi iona tanzania zaidi ya mwananchi kuambiwa alipe kodi tu.....huku anasisitizwa kuchukua risiti

Ova
 
Nidai risit kwa lip? jema ambayo kodi yangu inanitende,kwa hilo ntakuwa muongo,huduma ya maji hakuna,umeme umekuwa shida,dawa nazo shida,kila kukicha tunaambiwa tuchangie kodi ya maendeleo,mara mchango wa madarasa,bado maabara yaani kwa sasa ninaamini kodi ya kichwa ipo ila ipo indirect,na vyuma vimekaza huo uzalendo utatoka wapi? ilhal kodi zetu zinatumika kwa maslahi ya Watu wachache
 
Mleta uzi unaona watu walivyo na hasira? halafu kwa nini duniani kote watu hawapendi kulipa kodi hata wakilipa hulipa kwa kulazimishwa?
 
KODI TUNAZOLIPA MNATUMIA HIZO KUWA NYANYASA WATANZANIA WENZANGU KUTUMIA NA NDUGU ZENU AISEEE HAPANA SITAKUJA KUDAI RISITI KWANZA WAKINIULIZA HUWA NAWAAMBIA USINIPE NENDA KATUMIE NA FAMILIA YAKO AU KUZA MTAJI WA BIASHARA YAKO HIV
 
Kama ilivyo kwenye vita ya kupambana na rushwa na ufisadi, hili kwake halina mjadala, na kimsingi ni suala jema.

Ni suala jema kwa sababu kodi inayokusanywa na serikali ndiyo inayotumika kugharimia shughuli zake mbalimbali za kuwapatia huduma za msingi wananchi.

Kwenye baadhi ya nchi, pamoja na kuwa kulipa kodi ni suala la kisheria kwa mwananchi yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, lakini pia kulipa kodi ni wajibu wa kiraia.

Raia wema huona fahari kulipa kodi, kwa kuwa wanajua inaenda kugharimia shughuli kwa ajili ya ustawi wao.

Rais Magufuli ameendelea kuhimiza wananchi walipe kodi, kupitia majukwaa mbalimbali.

Amenukuliwa kupitia vyombo vya habari, akihimiza wananchi wenye sifa ya kulipa kodi wafanye hivyo.

Kwamba hata pale wanapoenda kufanya manunuzi ya bidhaa dukani ama kulipia huduma yoyote ile ya kibiashara, amehimiza wananchi wadai risiti.

Kwamba katika kila bidhaa ama huduma inayolipiwa, kuna asilimia ya serikali inayobakia ambayo inapaswa kwenda serikalini kwa ajili ya kugharimia shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Mjadala unaona pengine kuna baadhi ya watu hushangaa wanaposikia serikali ikishupalia watu walipe kodi.

Ieleweke kwamba, serikali ikiwa ni pamoja na mihimili mingine ya dola kama vile Bunge lenye jukumu la kutunga sheria na Mahakama yenye jukumu la kutafsiri sheria, pamoja na idara zake mbalimbali, zinahitaji fedha ili ziweze kutimiza majukumu yake barabara.

Mbali na fedha kwa ajili ya uendeshaji wa mihimili hiyo, kunahitajika fedha za kuwalipa watumishi wa serikali, wabunge, majaji na mahakimu, na yote hiyo inatokana na kodi inayokusanywa na serikali kutoka kwa walipa kodi.

Kuna kodi za aina mbalimbali, kuanzia ile ya mapato, ambayo kimsingi mfanyakazi yoyote hulipa kutegemeana na mshahara wake.

Kwamba kuna asilimia ambayo hukatwa na kupelekwa hazina, kwa ajili ya shughuli za kiserikali.

Kuna kodi ya majengo au mali isiyohamishika ambayo hulipwa kutokana na thamani ya mali ama jengo lenyewe.

Aidha, kuna kodi ya mauzo ambayo Dk.Magufuli amekuwa akiisisitiza mara kwa mara, inayopatikana pale mtu anapoenda kununua bidhaa dukani ama huduma sehemu panapouzwa huduma.

Kwa kila bidhaa inayonunuliwa, kuna asilimia inayokatwa na muuza duka ama mtoa huduma kama kodi ya serikali.

Hata hivyo, Mjadala unaona kwamba, pamoja na juhudi zote zinazoonyeshwa na Dk. Magufuli za kuhimiza wananchi kudai risiti pale wanaponunua bidhaa dukani, bado mwitikio uko katika kiwango cha chini.

Nasema hivyo kwa sababu, Mjadala umekuwa akishuhudia wananchi wengi wanaoenda kununua bidhaa kwenye baadhi ya maduka, tena mengine ya jumla jumla, wakiwa wanatoka bila ya risiti.

Kimsingi, kitendo hicho hakina maelezo mengine zaidi ya kuwa ni cha kukwepa kodi.

Ni cha kukwepa kodi toka kwa mwananchi mwenyewe aliyenunua bidhaa na akaacha kudai risiti, lakini vilevile kwa muuzaji.

Hali hii haiko kwenye biashara za maduka yanayouza bidhaa tu, bali hata kwenye maduka ya dawa.

Kimsingi kitendo hiki ni cha kumuangusha rais wetu mwenye dhamira ya kuona wananchi wakifaidika na keki ya taifa kupitia huduma za elimu, afya, maji, miundombinu, ulinzi na usalama, masoko na zinginezo.

Nimesema kwamba suala la kulipa kodi katika nchi zingine ni la kisheria na wajibu kama ilivyo hapa kwetu.

Pengine tofauti iliyopo kwa sasa ni kuwa Dk. Magufuli, anajaribu kupandikiza kwa wananchi moyo wa kulipa kodi ili waone kuwa ni wajibu wao kama raia.

Ni kwa misingi hiyo ndipo Mjadala unapowaasa wananchi kudai risiti kwa kila bidhaa ama huduma wanayonunua ili kodi yote ya serikali iweze kupatikana kwa ustawi wa taifa.

Chanzo: Nipashe

Mkuu,unaonekana unayoandika umejifunza “point za darasani”..kuna vitu vya msingi kabisa,tena vingi tu umeacha kuhusiana na hiyo kodi
*kati ya maksi 10,nakupa 0.5...umejaribu
 
Utamtambuaje wewe kama mteja tu, ambae unaambiwa dai risiti?
Kuna risiti za kawaida, ambazo hutolewa na wafanyabiashara ambao hawajafikia hayo mauzo. Na pia, Kula unaponunua bidhaa zenye thamani y TSH. 5000 unatakiwa kutoa risiti. Kwa hiyo siyo kwamba kila manunuzi unayofanya utapewa risiti. Viongozi wengi, hasa wanasiasa hutoa maagizo ya vitu ambavyo hawavielewi, ingawa vingime wanavielewa. Ila wanaotekeleza ndio wanaojua.
 
Back
Top Bottom