Elections 2010 Tuko vitani

domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,545
1,719
Namuangalia mama yangu aliyekuwa mwalimu wa shule ya msingi, yupo kitandani anaumwa, hana uwezo wa kujitibu. Ukweli ni kwamba tunasubiri siku yake tumzike, matibabu yake mpaka nje ya nchi na yeye ha qualify kupelekwa nje kwani umri wake ni mkubwa wanasema wenye mamlaka. lakini mama yangu si mtu mzima kama Waziri nanii na yule nani wa jeshi ambaye amepelekwa nje ingawa damu yake imeshachafuka.

Mdogo wake marehemu babu ametoka lakini hatujui kama atarudi, yeye ameenda kufuatilia madai ya marehemu kaka yake yale ya jumuiya ya afrika mashariki, najua wazee siku hizi wanapigwa virugu, maji ya kuwasha na mabomu ya machozi eti wanadai tangu 1977, miaka thelathini na ushee hivi, hata yule jamaa wa maamuzi magumu naye alikuwapo lakini mmmmhh

BBaba yeye bado anafuatilia kiinua mgongo chake, lakini miguu yake ndio inayomsumbua zaidi, wanamwambia sijui cheki iliandikwa hakwenda kuichukua sijui sasa imefanyaje sijui

Huyu mdogo wangu nae ni msumbufu, mi nilishamuambia kuwa hawa watu hawataki ukweli, yeye kaenda huku sijui ndo yudomu kachonga mdomo wake wamemwambia analeta siasa chuoni.

Sijui kama mama yangu atapona, sijui kama babu yangu atarudi salama, sijui kama baba yangu atalipwa haki yake au nae atakufa akiidai, na huyu mdogo wangu sijui hatima yake ni nini. Mimi kaka yake nilipangiwa kufundisha mpanda, nimekuja nyumbani mara moja, sijalipwa bado fedha zangu za kujikimu, sijui kama kweli nitalipwa kwani kaka yetu mkubwa yeye alipangiwa kufundisha shule moja hapa mjini mwaka 2004, alifanya kazi mwaka mmoja bila kulipwa mshahara wala chochote, akaaugua, akafa mpaka leo kaburi lake halijalipwa.

Hapa maeneo ya amana kuna kichaa mmoja anasema tuko vitani, tunapigana na adui, adui asiyeonekana adui anayeitwa SERIKALI YETU
 
najua umeme kijijini kwenu ni ndoto!maji jee mnayapata km ngapi?vipi hali ya shule hapo kijijini kuna waalimu,madawati,vitabu?hali ya chakula ikoje?
 
Domokaya, hadithi hii inasikitisha sana. Ila ikifika muda wa uchaguzi , msitusaliti na kuwachagua hao hao.
Sisi wadanganyika ni wepesi sana wa kusahau ikifika muda wa kufanya maamuzi magumu.
 
Mpwa, uko juu, hii story kwa mtu mwelewa imebeba meseji sahihi kwa wakati sahihi.....tuiendeleze hivi, na yule mdogo wetu wa kike wa mwisho amepata ujauzito alipokuwa kidato cha kwanza kwenye ile shule yetu mpya ya Kata ambako alibakwa wakati anarejea nyumbani akitokea shuleni, pana kaumbali kiasi cha kilomita nane au tisa hivi na msitu na mapori hivyo siku ile alichelewa kutoka shule kwa kuwa alikuwa na adhabu aliyokuwa akiifanya baada ya kuchelewa shule juzi, sababu ya kuchelewa ni kwamba alikua amepitia kwa babaetu mdogo kuomba ada ya shule (japo pia hakuipata).

Na yule mjomba wetu, mdogo wake Mama wa mwisho aliekuwa amefungua kioski pale mjini Nyamagana amekamatwa na Polisi eti alihusika kwenye kuupinga unyanyasaji waliokuwa wakifanyiwa na Halmshauri/Manispaa ya Jiji, hivyo mambo yanazidi kuwa magumu, hivi nikuambiavyo hivi; jana usiku na juzi pia tumeshindia na kulalia uji lakini kubwa zaidi waziri wa mambo ya ndani ndg fulani amefika hadi hapa kijijini lakini hakuongea nasi japo hata salamu, tulitamani sana kusikia kauli yake kuhusu ndugu zetu waliokatishiwa maisha yao na watu waliopewa dhamana ya kutuibia na kutuuwa. Pengine hili litakuwa ndilo chozi langu la mwisho niandikapo waraka huu, maana naskia kuna fununu kuwa natafutwa eti nimekuwa mchochezi kwa kusema ukweli wa wanyonge ambao ni uongo kwa watawala; kama wabunge hawatasinzia au kulala sana leo huko bungeni kama juzi; naomba wasambazie nakala ya ujumbe huu ili waweze kujipima na kuchukua maamuzi magumu; pengine damu yetu na damu ya wale waliotangulia iwe sadaka, ubani na fukizo takatifu kwetu na kwa watoto wa watoto wetu.
 
Domokaya, hadithi hii inasikitisha sana. Ila ikifika muda wa uchaguzi , msitusaliti na kuwachagua hao hao.
Sisi wadanganyika ni wepesi sana wa kusahau ikifika muda wa kufanya maamuzi magumu.

Aise, pole sana Mungu aingilie kati
 
yeah hii ndo nchi yetu ilipofikia pole sana ndugu yangu mdogo wako bado hujui atarudi lin chuo. Martin luther king Jr once said 'freedom will never voluntarily given by the opressor it must be demanded by the opressed'
 
tuko vitani hasa wakuu. na kwetu hii ni vita kubwa kuliko vile vita 2 za dunia. hii ndo dunia yetu na kwa hiyo hii ndo vita yetu kubwa ya dunia. sasa nimeamini kuwa ili kuendelea tunahitaji vitu 4 i.e. 1. watu 2. ardhi 3. siasa bora na 4. uongozi bora. tunavyo hivyo 2 vya kwanza. lakini nina mashaka sana na cha tatu. lakini cha tatu huletwa na cha 4 ambacho kwa uhakika kabisa HATUNACHO. Nani anatuwekea hawa bora viongozi? inaweza kuwa ni sisi wenyewe, kimakosa, kishabiki au kiupeo mdogo. lakini pia sisi hujifunza kuwa huyu tuliyemweka mwanzoni ni bomu na sasa tusimweke tena. lakini pia hawa wabovu wasio kuwa na malengo kwetu bali kwao binafsi nao hawataki kuyaachia hayo madaraka. kwa hiyo basi ni jukumu letu sisi kuhakikisha hawachakachui uchaguzi wetu ili mwisho tuwe na uongozi tuliouchagua na sio tuliochaguliwa na wenye nguvu za mabavu. TUSIKUBALI ASILANI., la kutia hamasa ni kuwa nguvu za mwisho tunazo sisi. hata leo hii tukiamua kuzitumia, tutasawazisha haya matatizo yote na DOmokaya atakuwa na story tofauti kabisa na hii aliyoisimulia hapa... NA TUFANYE HIVYO SASA!
 
kweli tuko vitani mdogo wangu aasoma sekondari ya kata alikuwa anajisomea kwa kibatari siku hizi anatumia mbalamwezi kwa kuwa mafuta ya taa yamepanda bei baba hawezi kumudu kununua. waziri alisema mafuta ya dizeli na petroli yatashuka bei lakini yanapanda kila siku, kweli tuko vitani. wadogo zangu wanakalia mawe darasani na kila siku wanapata funza sababu ya vumbi darasani. eeh mola tuokoa waja wako.
 
Kwa kweli inasikitisha jaman huu ndio uhalisia wa maisha yetu, tutavumilia mpaka lini? Aaaaaaarrrrggghhh
 
Naialika familia yenu iwe na mgomo wa pamoja. Yani mgomo wa kifamilia dhidi ya serikali. Hali yenu ndo yetu ndugu.
 
Basi basi Mpwa, ukilia sana utakuja niliza na mie tukose wa kumbembeleza mwenzie...basi tumwamini MUNGU wote ni wake....huwanyeshea mvua wema na wabaya; hapa ndio kwenye busara ya MUNGU iliyo ngumu kuiliko chochote
Haya marefu yamezidi urefu binamu...
Inaniuma sana
nikifikiria huwaga ninalia
Inaniuma sana...
 
Kweli wazee tupo vitani, na Maandishi yanasomeka ukutani.

My people, lets be the winners not the whiners, the leaders not the followers, the victors, not the victims. Let’s change the paradigm of the government movement that has served to marginalize and ridicule us for not following their collective agenda. Tumechoka

“Oh...
Maybe one by one,
We can see that something
Can be done...
With a little piece
From everyone
We can make a stance,
We can heal this land...” By KYMAN MARLEY- one by one
 
Back
Top Bottom