Tuko vitani. tuungane tuwe na umoja, la sivyo ......

Mangaline

JF-Expert Member
May 19, 2012
1,045
221
Katika hali kama hii, katika wakati kama huu, ambapo upande mmoja wa walala hai unatumia nguvu kubwa kupinga na kudhoofisha upande wa walala hoi, kunahitajika kuwa na umoja, na kushauriana pasipo kupingana ili kuleta "solidarity" ya kweli. Kamanda mpigania haki, Dr. Uli, kaonewa, hivyo sote walala hoi hatuna budi kuona kama "an injury to dr. uli, is an injury to us all."
Mwanaharakati mmoja, juzi alitusihi tufanye maandamano kupinga tendo hilo, cha kushangaza, tulipishana mno katika mawazo yake, bila kutoa "constructive idea" ya namna ya kuboresha wazo alilokuwa nalo.
Hii inaonesha kuwa kundi la walala hoi, hatuna solidarity, na hivyo, saa ya ukombozi wa kweli si sasa na yamkini iko mbali.

WAZO LANGU:-
Kama kweli tunahitaji mapinduzi ya kweli, ya kuuondoa unyonge wetu, lazima tusaidiane kunyoosha wazo la kila mmoja wetu, na siyo kutoa "destructive idea" kwa kila mwenzetu. Walala hai tutambuane, tuwe na umoja.
"ASIYE KINYUME CHETU, YUKO UPANDE WETU"
 
Back
Top Bottom