Tuko serious Lowassa awe Rais?

mkuu hawawezi kukuelewa hata kidogo.
Sijui ni nan katuloga watanzania mpaka kuwa wapumbavu kiasi hiki.

Wanadanganywa eti anauchukia umaskin ndio anauchukia kwa familia yake lakn sio kwa watz.

wewe ndo umerogwa ukawa tuko fit
 

Kaka watu kama wewe ndio taifa linawahitaji. Hongera sana kwa kuona hili na kulielezea hapa. Najua utatukanwa na wanywa viroba lakini message umeshaitoa. Nimesema huko nyuma kwa wenye macho waone, ila taifa letu limekuwa ovyo sana. Ukitaka kuona angalia majibu watakayo toa kuhusu post yako. Halafu si tu Monduli. Hivi Lowasa kafanya nini hasa katika hii nchi..tuwe wakweli. Kasimamia kitu gani na kikafanikiwa mpaka mwisho?
 

Nimeipata hoja yako. Ni kweli kabisa Magufuli ana upungufu wake kama mgombea yeyote yule. Hatuwezi kupata mgombea malaika.

Labda ni suala la lugha au maneno muafaka ya kutumia. Kati yake na Lowassa, ana nafuu, au afadhali au ni bora. Ni Lugha tu. Huyo mwingine upungufu wake umezidi kipimo kwa vigezo vyovyote vile.
 

Saana tu, nikiona mijitu yenye kichwa yanathubutu kuishabikia ccm. Umezaliwa wapi weye?? Mgombea urais mwenyewe anashangaa inakuwaje mtu aende hospitali mgonjwa, apimwe na Dr. halafu ashauriwe kwenda kununua dawa duka la mtu binafsi. Miaka 54+ baada ya uhuru. Wewe huumwi???? Basi weye ni kichaaaaa
 
Kwa mamlaka aliyonayo rais (kikatiba) bora rais safi kwenye chama kichafu maana ana uwezo wa kufurukuta na kuwanyoosha....nchi hii inataka rais aliye na political will baas...waliopita sidhani kama walishindwa...hawakuwa nayo...nina imani kubwa sana na Magufuli...hata ukimtizama usoni....unaona kabisa jamaa ni mkweli...

 

embu compare mondoli na wilaya zingine
 
Bwana nani anakudanganya lowasa kuchukua nchi hii,hizo ni ndoto,nsye analijua hilo kakabwa koo hana ujanja[/QUOTE

kwa sababu we rais wa maboya wa fb unadhan kila mtu anaota kama wewe
 


WEWE CHAGUA KUNDI LA CHENGE sisi TUNACHAGUA kundi la TINDU LISSU
 
nakumbuka picha iliyoonywesha na kituo cha star tv kuhusu shule ya monduli shule imechoka halafu walikuwa wanaomba msaada huku mbunge wao aliyekuwa akisikika kutoa msaada hakufanya chochote huyu ni msanii hana mpango na maskini ila wezi na matajiri wenzake
 
Magufuli tumeshasikiliza Sera zake ambazo ni zile zile, amekazana kusema anaashangaa tumefikaje hapa kila kitu anashangaa unajiuliza kwani alikua nchi gani? Kesho njooni mmsikilize Sera zake kabla ya kuonga hapa kua hana Sera, pia sidhani kama kuna ukweli wowote kua monduli hakuna maendeleo, au mlitaka awalazimishe wasivae mashuka? Tafuteni hoja za msingi
 
Mkuu sibonike, hapo kwenye red tunahitaji elimu ya kutosha kuhusu uchaguzi wa mwaka huu. Maana hata mimi nimeungana na Dr. Slaa kupumzika, ila nimepoteza dira ya kura yangu niipeleke wapi? JF ebu wekeni hoja hapa ili nifanye maamuzi sahahi.
 
Mkuu sibonike, hapo kwenye red tunahitaji elimu ya kutosha kuhusu uchaguzi wa mwaka huu. Maana hata mimi nimeungana na Dr. Slaa kupumzika, ila nimepoteza dira ya kura yangu niipeleke wapi? JF ebu wekeni hoja hapa ili nifanye maamuzi sahahi.

Kipi ni rahisi kusahihisha? Mgombea safi kwenye chama kichafu au chama kisafi chenye mgombea mchafu?

Kwa lugha nyingine, kipi ni rahisi zaidi - chama kisafi kumuweka sawa mgombea wao mchafu wakishinda uchaguzi au mgombea safi kuwaweka sawa watu wa chama chake akipata uongozi?

Kwa kutumia maneno ya Nape - kipi nafuu? Kuweka Oil safi kwenye gari chakavu au kuweka Oil chafu kwenye gari mpya?

Nahisi kila mtu atakuwa na jibu lake hapa.
 

Kiswahili kibovu rais wako mwenyewe unayemtaka ana kiswahili kibovu balaa,bora huyu ni zile za l na R
 
Magufuli ni Rais wa awamu ya tano tumwamini ataweza kukutumikia vema watanzania kunyoosha mafisadi.

Anyooshe mafisadi wakati yeye mwenyewa BONGE LA FISADI . Kumbuka 10 percent ya kwenye mabarabara yanayoharibika ndani ya mwaka, majengo ya umma, kumbuka hesabu za CAG
 

tupo serious ccm kuendelea kututawala?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…