TUKO PAMOJA NAO

TUKO PAMOJA NAO

Vitalis Konga

Senior Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
127
Reaction score
231
Timu ya Uongozi wa CCM yenye wajumbe sita inayoongozwa na Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga na Ndg. Humphrey Polepole ambao ni Wakuu wa Idara CCM Makao Makuu, tayari imewasili na kuweka Kambi Mkoani Mwanza Wilaya Ya Ukerewe katika kisiwa Cha Ukara ili kuhakikisha mambo yote yanayoendelea kusimamiwa na Serikali yanakwenda vizuri ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Majeruhi wanapatiwa matibabu ya haraka pamoja na wale wote ambao wamepoteza maisha kuhakikisha kuna kuwepo na utaratibu mzuri wa kuwasitiri na kuwahifadhi.

Nini maoni yako kuhusu hii ziara ya viongozi?
 
Sioni sababu ya wao kuwepo kule ikiwa wameenda kama chama. Lakini kama wakiwa na dhamira ya kibinadamu ni sahihi. Eti wanahakikisha masuala ya serikali yanakwenda vizuri ha ha ha ha! kumbe wameona nguvu za vyombo vya serikali zimepungua katika kuimarisha usalama na huduma ikabidi waende. Hii ni kutaka kuji........
 
Maoni ya nini sasa?mkiona ni wanasiasa mnajaribu kutafuta vi mada visivyo na mashiko kupata wachangiaji mitandaoni na kuongelea siasa hata kwenye majanga.hao ni viongozi wa chama dola na wameenda kwenye janga lililotokea kama waTanzania,nikitu kisichohitaji maneno mitandaoni maana yatakua ni maneno yasiyo na maana,msibani nako kujadiliwe?
 
Mmmh ....

Wameenda kutonesha vidonda

Na kuchukua ramb rambi

Hawanaga jipya ccm

Babu zao na hawa wote wale wale

Like fathers like sons
 
majeruhi tena" ... acheni masihara",.. sidhani kama wanafika hata wa tano
 
Back
Top Bottom