OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 457
- 773
Deni la Taifa kwa sasa limepanda kutoka Trilioni 108 mwezi Mei hadi trilioni 116 Mwezi Agost. Hili ni ongezeko la 7.41% ndani ya kipindi cha miezi miwili tu. Deni hili linaweza kunasibishwa na taarifa kuwa exchange rate imezingua, lakini ieleweke kuwa thamani ya shilingi imeimarika kuanzia mwezi wa nane mwanzoni.
Mwezi wa tano, shilingi ya kitanzania ilifikia kuwa 2686 kwa dola moja ya Marekani ambapo hadi sasa shilingi imepanda thamani hadi kufikia 2458 mwanzoni mwa mwezi Agost.
Niiweke hii sawa, yaani kama tulikuwa tunadaiwa dola 100 mwezi wa mei maana yake tulikuwa tunadaiwa Tsh 268,600. Ikiwa hatujaongeza hela ya kukopa na tukabaki na deni hilo hilo la dola 100 mwezi august deni kwa shilingi lingekuwa Tsh 245,800. Yaani lingepungua kutokana na kupanda kwa thamani ya shilingi.
Hata kama tutaweka riba kwenye deni, haingewezekana kwamba deni liwe linapanda kwa 7% kwa miezi michache. Hii ni kusema kuwa kuna hela nyingi zimekopwa kwa kipindi cha miezi miwili, huku bunge likiwa halipo kuidhinisha matumizi ya fedha.
Nawasilisha.
Pia soma >> Tanzania: Deni la Taifa lafikia trilion 116