Tukiwa outing anageuka bubu

Tukiwa outing anageuka bubu

Wakuu,

Ninakwazwa na tabia ya binti mmoja hivi ambae nimempa heshima kubwa ya kumtoa outing sehemu ya daraja la juu ambapo hata mimi huwa siendi. Huyu binti yupo kwenye middle-class anaishi na wazazi wake na ni mhitimu wa chuo.
Mimi ni mjasiriamali nina duka la jumla huku uswahilini na pia najihusisha na kilimo cha mchele mkoani, nilipomaliza nilisota sana benchi nikaamua kuwa mfanyabiashara na sasa mambo yapo levo namalizia nyumba Bunju.

So nikasema acha nitafute mtoto mzuri msomi niwekendani nikampata mtoto mmoja hivi mkali sana akakubali kimsingi kuwa na Mimi hatujazini bado. Lakini kuna jambo bado sijalielewa kwamba tukiwa outing haongei chochote mm ndo nageuka muongeaji mkuuNikikaa kimya basi ndo tunakua kama mabubu vile.

Tena unakuta nimejikoki nimempeleka sehemu ya maana na tulivu lakini ni yale yale, nikianzisha habari za Mkurunzinza kufurumushwa Burundi ambazo ndio zilikua zina trend hii wiki nzima iliyokwisha anakuuliza Mkurunzinza ndio nani.Nikisema nianzishe story za Escrow na bunge ambazo msomi yoyote hapa Tz hawezi kushindwa kujua.

Unakuta yupo kimya nikisema haya sasa ngoja nizungumzie mapenzi ambayo ndio yametuleta hapo date pia kimya nikimuuliza kama ananipenda anasema ndio. Haya myweather na manny wamepigana majuzi ulilionaje pambano? Ananiuliza ni akina nani hao.

Hivi wadau mkiwa date ni lazima watu muongelee mapenzi mwanzo mwisho?Au kwenye date kama hii ambapo mpenzi anakaa kimya mwanzo mwisho unafanyaje? Au hanipendi?



da kumbe kuongea ni kipaji. Mpaka nashindwa kutoa ushauri coz mtoto wa chuo lazima ajue hayo mambo. Maana nategemea date kama iyo stori kibao eg barcelona na yanga ndo habari ya mujini kweli anashinda kujua wanacheza lini na ni akina nani watakuwa kwenye kikosi?

Jingine hata kuchangia katiba?

Au kuongelea uchumi ili akulete kwenye the main topic ili ujiongeze baada ya date? Its impossible

sasa basi binti inaonekana ana ndege 2 na wewe ukiwemo ila kasimama mguu pande mguu sawa hataki kukuzoea wewe na ukakoleakwa penzi kwa sababu anategeshea kwa yule john ambae mnazidiana kidogo kiuchumi au appearance so hajielewi!
 
<img src="/images/styles/JamiiForums/smilies/glasses-nerdy.png" border="0" alt="" title="Glasses Nerdy" smilieid="191" class="inlineimg"><img src="/images/styles/JamiiForums/smilies/glasses-nerdy.png" border="0" alt="" title="Glasses Nerdy" smilieid="191" class="inlineimg">&nbsp;please give us the age difference!!!!!
 
Akuu nlishajiondekeaga, I was never comfortable around him na hakua mkali kabisaa

Ulianza kumuheshimu sana kupita kiasi kwa kujua a kutokujua! matokeo yakawa hayo!
 
Kijana usiwe na hofu bado anakupenda, ila nawe sijui unaremba nini Uzuri wa mwanamke mkishaonananae uchiuchi hakuogope tena, outing inayofwata mtakua na vitu Vingi vya kudiscus.
Jaribu.!
 
nazani story zako unazompigisha azifagilii.
sasa Fanya hivi,mtoe out kwa Mara nyingine tena,then mwambie keo zamu yako kuanzisha mada,kila siku Mimi ndio naanzisha story.
akisema sina neno,then pateni chochote then muondoke.
next time muombe aje kwako kukutembelea,akija usifanye ajizi omba mchezo in a polite manner .
 
Back
Top Bottom