Tukiwa na viongozi wasiojiamini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukiwa na viongozi wasiojiamini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Expedito Mduda, Jun 3, 2012.

 1. Expedito Mduda

  Expedito Mduda JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Watanzania wengi sana leo wajiuliza: Hivi katika uongozi wa mwalimu haya tunayo yaona sasa yalikuwepo? Mfano, sehemu ya nchi kuamua kujiita ni nchi kwa kuvunja katiba kwa wazi kabisa na kuachwa bila kuchukuliwa hatua.

  Watu wa kikundi fulani kuamua kuharibu mali za watu wa kikundi kingine na kuambiwa tu waache hayo mambo bila kuchukuliwa hatua inayoonekana. Viongozi kuiba mali ya umma na kuishia kuwabembeleza kuachia nyadhifa eti uchunguzi wa kishikaji ufanyike.

  Ujambazi kukithiri hata mchana kweupe watu kunyang'anyawa mali zao. Watu kuuawa na kuacha mambo yapite kana kwamba ameuawa nzi na si binadamu!

  Hivi mwalimu angekuwepo haya yangetokea? Hivi kweli mwalimu angekuwepo watu wangepewa adhabu eti kosa kuzaliwa katika eneo lenye dhahabu kama kule Mara? Hivi mwalimu angekuwepo watu wangefukuzwa kutoka maeneo walozaliwa eti kupisha wanyama pori waendelee kujitanua ili wazungu waje kufurahi? Kufukuza bila fidia! Hivi kweli kungekuwa kuna mtu hajalipwa fidia ya mabomu Gongo la Mboto?
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Kuongoza miaka 20 kweli nyerere alipendwa.
   
Loading...