Tukitukuze kiswahili chetu

Fredinho

JF-Expert Member
May 18, 2016
971
1,137
Nipo naangalia michezo ya olympiki, washindi wote wanajieleza kwa lugha ya nchi wanakotokea kwa furaha na kujiamini bila kujali wanahojiwa kwa kiingereza, kifaransa au kireno, halafu napiga picha jinsi watanzania tunavyodharau watu na viongozi mbalimbali wanaotumia kiswahili kama lugha ya mawasiliano katika mikutano au hafla mbalimbali, eti tunatamani watumie kiingereza ili tuone wako juu na ni wasomi.

Najiuliza ni kwanini hatukionei ufahari kiswahili chetu? Sitashangaa mtanzania atakaeishinda medali yoyote akihojiwa atakavyojitahidi kuporomosha kiingereza cha kuunga unga kisichoeleweka wakati kiswahili anakielewa mwanzo mwisho. Ifikie hatua tuwalazimishe wao watutambue sisi, badala ya sisi kuendelea kuwatukuza wao.
 
Back
Top Bottom