‘Tukitengana na Zanzibar tutashambuliwa’

Bujibuji Simba Nyanaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
61,614
2,000
MKAZI wa Kata ya Nkoma, Lazaro Daudi, amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uendelee kwani ukivunjika Zanzibar itaweza kuishambulia Tanganyika.
Alisema kuwa, kuungana kwa nchi mbili hizi kunasaidia kudumisha amani na utulivu hivyo suala hilo lidumishwe.
"Tukijitenga na Zanzibar tutaisha, watakuwa wanaingia kwenye maji na kutokea bandarini hatimaye warushwe mabomu," alisema.
Alisema ili kuipunguzia Serikali gharama endapo rais, mbunge au diwani akifariki, mtu aliyeshika nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa ndani achukue nafasi yake.
Naye Kato Kiumbani (70), mkazi wa eneo hilo alitaka waruhusiwe kuachana na zao la pamba kwa kuwa Serikali hailijali.
Wakulima wa pamba tumekuwa tukipata hasara kila mwaka, ni bora turuhusiwe kuachana na ukulima wa zao hili,"alisema Kiumbani:

"Kwa upande mwingine tangu nakua naona Serikali haitaki wafugaji, kule porini wameleta ndege wanawafukuza ng'ombe wetu wanavunjika miguu na wanakuwa wanazaa bila mpangilio, hili suala liangaliwe."

Alisema pia kuwa, madaktari wasiruhusiwe kumiliki maduka ya dawa kwani wanatumia nafasi hiyo kuiba dawa za hospitali za umma.

"Unaenda hospitalini unaambiwa dawa hakuna halafu daktari anakuelekeza duka la kwenda kununua dawa, hii siyo sawa haya maduka yatakuwa ni yao na wanapeleka huko dawa za hospitali zetu," alisema.

Kwa upande wake Masanja Kurwa, alitaka Katiba ijayo iwatambue wanaume waliofiwa na wake zao na kuwapa fursa ya kupata misaada mbalimbali.

"Mbona wanawake wajane wanapewa misaada lakini wanaume wakifiwa na waume zao hawapewi msaada, wanaume tuliofiwa na wake zetu na sisi tutambuliwe," alieleza.

 

Bujibuji Simba Nyanaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
61,614
2,000
Yaaani watu wanaongea uzuzu mwanzo mpaka mwisho
"Tukijitenga na Zanzibar tutaisha, watakuwa wanaingia kwenye maji na kutokea bandarini hatimaye warushwe mabomu,"

Wakulima wa pamba tumekuwa tukipata hasara kila mwaka, ni bora turuhusiwe kuachana na ukulima wa zao hili
Hii katiba itakuwa kubwa kama encyclopedia
 

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
6,664
2,000
Hii katiba ina-expose kiasi cha ujinga wa watanzania. No wonder CCM inashinda kila uchaguzi.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,452
2,000
ccm imewalisha limbwata hao

Na ni maoni ya watu dizaini hiyo ndiyo yatakayopewa uzito mkubwa na Tume na hatimaye kuamua mustakabali wa Katiba na hatimaye taifa letu. Kimzaha mzaha hivi hivi!
 

Makindi N

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
1,067
1,250
A 51 yrs old nation! Halafu JK anasema maendeleo yalioletwa na CCM sio ya kubezwa hata kidogo! His focus being more on quick gains and not time and quality of what the government offers. We ended up having rotten system.... poor government, poor people (in everything), poor infrastructures, poor relationships (ktk nyanja zote), its poor, poor, poor etc....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom