Tukitaka kula inabidi tukubali kuliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukitaka kula inabidi tukubali kuliwa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Anfaal, Mar 9, 2010.

 1. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hizi ndiyo hali za migodini mingi nchini ambayo Watanzania wanajitafutia riziki, (Picha kwa hisani ya the East Africa).
  Maoni yangu ni kwamba uchimbaji wa namna hii si endelevu (subsistance). Si uchimbaji ambao unaweza ukaleta manufaa kwa Taifa au hata kwa wananchi in the long-run.
  Awamu mbalimbali zimekuwa zikihamasisha uwekezaji hususani awamu ya tatu na ya nne, wananchi wakiamini kuwa huenda madini yakatukomboa katika umasikini ulikithiri. Lakini ukweli unabaki wazi tokea enzi za mwadui mpaka sasa hakuna manufaa ya maana yanayoonekana licha ya takwimu mbalimbali zinatolewa. Hii inathibitishwa na kuongezeka kwa urari na viashiria mbalimbali vya kiuchumi vikionyesha kuwa hakuna hatua tunazopiga isipokuwa zile zinazotamkwa kwenye makaratasi na majukwaa. Mf. Suala la ajira, Wakati serikali ikidai kuwa zaidi ya watu mil 1 wameajiriwa katika kipindi cha miaka minne, ukweli unabaki kuwa ni vigumu kuweza kuainisha waziwazi maeneo ya ajira ambao watu hawa wanapatikana. Hili linathibitishwa na ukweli kwamba kwa nchi kama Tanzania kupata takwimu ya watu ambao hawapo kwenye ajira ni suala gumu. Pia kipimo cha maendeleo kinaweza kupimwa na upatikanaji wa huduma nyeti kama umeme (chini ya asilimia 10 ndio wanaupata), maji (inakadiriwa asilimia 60!!!!), elimu (ya msingi zaidi ya 90% ila kiwango ni cha kutia mashaka makubwa) nk.
  Hivi karibuni serikali ilipitisha mswada ili kuhakikisha kuwa watanzania wanadhibiti njia za uchumi kwa kuanza na makampuni ya simu na kuondoa mianya mbalimbali ya ukwepaji kodi na baadaye ikaaminika kuwa sekta ya madini nayo ipo kwenye mchakato huo. Tatizo bado linabaki kuwa, hata kama serikali itachukua hatua hiyo je ni Watanzania wangapi wanauwezo wa kununua hisa katika mashirika hayo? Usimamizi wa soko la Hisa kwa wakati huu uko vipi? Na imani ya wawekezaji itakuwaje? watakubali kuliwa au wamezoea kula tu?
  Hoja ya msingi; Sekta ya madini ni sekta muhim na inayoweza kuleta ahueni inayoonekana kwa Watanzania. Wakati huu ambapo ufanisi hauonekani muelekeo wa taifa kulist makampuni ya madini ni muafaka? Binafsi naona hakuna haja ya kuchimba madini maana nadhani athari/hasara zake ni kubwa kuliko faida tunazotajiwa.
   

  Attached Files:

 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...