Tukipungiza ada za shule binafsi tutapunguza msongamano kwenye shule za kata!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
36,155
29,677
Wanafunzi wanakaa chini kwenye shule za umma kwa kuwa kuna msongamano.Msongamano huu unasababishwa na mengi lakini la muhimu ni uwezo mdogo wa wazazi wenye kipato cha mfanyakazi wa serikali kushindwa kuwasomesha watoto wao kwenye shule binafsi.

Tutakapoweka ada elekezi kama level ya Chuo kikuu tunaweza kupunguza msongamano huu.

Leo hii gharama ya shule binafsi inapanda kwa kuwa na makorokoro mengi yasiyo na tija...mfano bustani za shule zinafanyiwa kazi na vibarua badala ya kuwatumia wanafunzi ili wajifunze stadi za kazi.
 
Naamini, ada katika shule za binafsi "Zikipunguzwa" na hivyo kupunguza pia "msongamano" katika shule za kata, Kiwango cha Elimu katika shule hizo binafsi KITASHUKA pia.....
 
Serikali dhaifu ikishindwa kitu
Shule zimewekwa ili kila mtu achague atakapo kutokana na elimu anayotaka, kuwalazimisha watu wote wasome kama wengine ai swala salama
 
Unadhani shule za binafsi zilianza leo?
Je unaongeleaje kuhusu ELIMU KUWA NI HUDUMA YA JAMII VS BIASHARA?
 
basi serekali ifungue shule zake itoze ada kidogo afu tuone kama izo shule hazijafungwa ndani ya miaka 2. shule private ni biashara watu wamewekeza hela nyingi kujenga shule na kuajiri walimu bora leo unataka kuwapangia watu ada kisa serekali Imeshindwa kuendesha shule zake...
 
Back
Top Bottom