mpaka sasa hiki kitu kinanitatiza sana
1. Cha kwanza, popote pale upinzani inaposhinda iwe uchaguzi mdogo, wa serikali za mitaa au mkuu wanasema uchqguzi ulikuwa wa huru na haki ila wakishindwa sasa husema kuwa uchaguzi haukuwa wa huru na haki. je , uchaguzi wa huru na haki ni ule unaotangaza upinzani washindi bila kushinda?
2. nashindwa kuelewa mpaka sasa , wapinzani na wewe mleta mada , tume huru mnayotaka mnataka iwe na vigezo gani. Kazi ya tume ni kusimamia na kutangaza matokeo ya uchaguzi , hayo mengine tume haifanyi. zoezi zima la upigaji kura linasimamiwa vyema na mawakala wa vyama na hata uhesabuji kura pia. masanduku ya kura yanahifadhiwa mpaka miezi 6 baada ya matokeo kutangazwa na kama kuna pingamizi linapelekwa mahakamani. mchakato huo mzima , mnataka tume huru iweje? iwe na mawakala wa upinzani tu? itangaze upinzani wameshinda kumbe si kweli?
wapinzani hasa mawakala wao wanachoshindwa ni kuwaambia ukweli watanzania kuwa tumeshindwa na CCM na kushindwa kufanya hivyo watanzania wanaamini kuwa hakuna tume huru kumbe ni tume ni huru kabisa na inatenda haki.
Maneno hayo yanajenga sononeko ndani ya jamii na kutokea mtanzuko wa ukweli halisi ambao unafichwa na upinzani kwa maslahi yao binafsi