Tukio la arusha – tuzungumze tumalize tofauti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukio la arusha – tuzungumze tumalize tofauti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yona F. Maro, Jan 5, 2011.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndugu Wazalendo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  Nimesikitishwa sana na Tukio la Arusha , Ambapo Polisi wa Kutuliza Ghasia walitumia Nguvu Kujaribu kuwaondosha Wananchi wa Arusha waliokuwa Njiani kuelekea Uwanja wa NMC kwa ajili ya Mkutano Leo .
  Baada ya hapo ni fujo zilizoenea maeneo kadhaa katika mji huo , mpaka ninapoandika Ujumbe hii inasemekana Dr Slaa na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema wamechukuliwa na askari hao wa kutuliza ghasia , Hapo kabla taarifa zilisema Ndugu Freeman Mbowe na Mama Slaa walikamatwa Na FFU .
  Pamoja na hayo kumetokea Tukio la kurushiwa mawe kwa Jengo la Ofisi za CCM mkoani Arusha ambapo vioo Kadhaa vimepasuka , wapangaji kwenye jengo hilo walikimbia hivyo kujaribu kujiokoa kutokana na mawe hayo .
  Kitendo hichi ni cha kupingwa kwa mfano na viongozi wetu wa dini pamoja na serikali pamoja na vyama vya kisiasa , Asasi za kiraia na Mashirika ya kutetea haki za Binadamu .
  Tukio la leo limeiweka Nchi yetu Tanzania Haswa Arusha GENEVA ya Afrika katika Ramani nyingine ya dunia , Jinsi watu wanavyojadili tukio hili kwenye vyombo vya habari kuanzia radio mpaka mitandao na tovuti kadhaa za maoni Hatujui huko majumbani Habari hizi watazichukuliaje na hata hatujui kesho Tanzania itaamkaje .
  Kwa tukio hili la mengine yaliyotokea katika kipindi cha miezi 2 iliyopita toka kumalizika kwa uchaguzi mkuu inaonyesha nchi yetu ina matatizo ya kutokuaminiana na ule mshikamano wa wananchi kwa wenyewe na viongozi wao unaonyesha kupungua kwa kiasi kikubwa sana .
  Tunaomba viongozi wafanye liwezalo kukaa chini kumaliza Tofauti hizi na kutoa tamko la pamoja kumaliza matatizo yaliyopo sasa hivi nchini yanayohusiana na uchaguzi uliopita ili tuweze kuendelea mbele .
  Mwaka huu nchi yetu inatimiza miaka 50 toka kupata uhuru – Itasikisha sana kusheherekea miaka 50 ya uhuru kwa vurugu na uvunjivu wa amani unaoendelea nchini .
  Jamani tuwe Wazalendo na kukaa mezani kwa majadiliano utumiaji wa nguvu kwa pande zote hauwezi kuwa suluhisho la kudumu , utumiaji wa nguvu mara nyingi unahusisha na visasi na utaacha vidonda ambavyo ni ngumu kuponyesha kwa kipindi kifupi .
  NCHI YETU NI YETU SOTE – TUKAE TUJADILIANE KUMALIZA TOFAUTI TUSONGE MBELE .
   
 2. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Mkuu Shy.

  Nitasema labda! Uliyoyasema ndiyo maneno stahili lakini nani atakusikiliza? nani ana muda huo? kwa sababu kila mmoja hamuhitajii mwenziwe na anajiona yeye amekamilika na anajitosheleza. Kwa ubabe watatawala na kwa ubabe tunawashinikiza mpaka wakubali.... tunafikiria hivyo na punde tutafanya maandamano tena kupinga kuzuiwa kwa maandamano yetu!!! hii ni Tanzania mpya, sawa na jini aliefunguliwa toka kwenye chupa (kwenye alfulela ulela) hapa ukiyasema maneno hayo (ambayo ndio ukweli) hayatakiwi bali yale waliyoyabariki wateule! BILA KUJADILIANA, BILA KUWA NA FIKRA PEVU basi....
   
 3. K

  Kizito Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  POLISI wa TZ hawataki kuukubali wakati maana wajiona kama vile ni taasisi ndani ya sisiemu. Kwani ni sababu zipi hizo za kiintelijensia kama sio kuvuruga mambo? yote tisa lakini tutafika tu.
   
 4. M

  Matarese JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Inabidi na sisi tuanze divide and rule, tuwashughulikie polisi mmoja mmoja, kwani si tunaishi nao!
   
 5. V

  Vipaji Senior Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 11, 2009
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Polisi wa tanzania wamezoea kulala kwenye mapango na kulala chumba kimoja familia tatu hadi nne na kusema ndiyo bwana kila kunapokucha. Mapolisi walikuwa wanatetea ufisadi ili asije tajwa god wao kwenye majukwaa lakini tutasonga mbele mwaka huu lazima kieleweke lazivyo hata serikali ing´olewe madarakani kwa nguvu. Imeniuma sana sana!
   
 6. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Walioko madarakani ambao ndio wenyejukumu la kuweka mazingira ya majadiliano ndo hao kama mnavyowaona!! Ni maguvu na ubabe tu!! Watu kukusanyika ni haki yao ya msingi. Hawajafanya fujo.... hakuna hali ya hatari iliyotangazwa..... wanatawanywa kwa nguvu kubwa kupita kiasi namna hiyo... kwa nini?? Hawa watawala wanagonga gogo..... na mlio watausikia..... Uvumilivu, busara, fikra pevu..... vyote hivyo vina ukomo mkubwa. Na ukomo huo umeshajili. Walioko madarakani wameshindwa kusoma alama za nyakati. They say "Give the people what they want... if you don't... they'll take it by force!!!... of which is disastrous!!!....
   
 7. T

  Topical JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Waliovunja ofisi ya chama tawala na kuwasumbua wapangaji watafutwe waonje mkono wa sheria

  Waliokiuka amri halali ya polisi ya kutokufanya maandamano wapelekwe kwenye mkono wa sheria

  Tunataka taifa lenye watu wanaojiheshimu ok? na kuheshimu maisha ya watu wengine...

  Sisi wote siyo cdm arusha tunatakiwa tuendelea na shughuli zetu, ndio maandamano yenu hayatuhusu mnatulazimisha
   
 8. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Police Jiandaeni msije zalisha walenga shabaha.........
   
 9. C

  CalvinPower JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 60

  Walioko madarakani ambao ndio wenyejukumu la kuweka mazingira ya majadiliano ndo hao kama mnavyowaona!! Ni maguvu na ubabe tu!! Watu kukusanyika ni haki yao ya msingi. Hawajafanya fujo.... hakuna hali ya hatari iliyotangazwa..... wanatawanywa kwa nguvu kubwa kupita kiasi namna hiyo... kwa nini?? Hawa watawala wanagonga gogo..... na mlio watausikia..... Uvumilivu, busara, fikra pevu..... vyote hivyo vina ukomo mkubwa. Na ukomo huo umeshajili. Walioko madarakani wameshindwa kusoma alama za nyakati. They say "Give the people what they want... if you don't... they'll take it by force!!!... of which is disastrous!!!....
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,803
  Trophy Points: 280
  Asante Shy kwa mtazamo wako. Ni kweli hii ni nchi yetu sote. Sasa kwanini tunafanya mambo kama vile hatujari lolote litakalotokea? Tumedanganya nafsi zetu kiasi kwamba tumekuwa vipofu hatuoni tena sababu ya kuipenda nchi yetu? Nchi hii haiwezi kuwa salama kama raia hawafuati sheria na serikali haitimizi wajibu wake
   
 11. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Tuna watawala nchi hii bila viongozi.
   
 12. L

  LAT JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Kinyaa..
   
 13. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  We ni mtako sana.
   
 14. Ikimita

  Ikimita JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 302
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sio wote humu ndani ni mashabiki wa vyama vya siasa na walio wengi hatufurahishwi na haya yaliyotokea lakini suluhu sio upuuzi unaouleta, utafunga wangapi? Kikubwa ni kwamba lazima pawepo consesus kuhusu masuala ya siasa kama kweli tunataka hali ya utengamano. Bila consesus hakuna mtu anaweza kuendelea na shughuli zake kwa amani. Sisi, mtu mmoja mmoja, sio kisiwa katika jamii.
   
 15. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,082
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Hii ndio tabu ya kunywa gongo 24/7 bila kula.(TKG 24/7 BK) Jamaa anaongea whatever comes forth. Kwa maneno haya lazima huyu mlevi kajiendea haja kubwa kwenye suruali yake alafu hana habari...
   
 16. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,477
  Likes Received: 1,435
  Trophy Points: 280
  Mtazamo mzuri, lakini kwa nini iwe baada ya vurugu na watu kupoteza maisha
   
Loading...