Tukio hili sitalisahau kamwe

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
1,583
2,697
Ilikuwa mwaka 2014,January, saa 2 usiku nikiwa natokea Geita kuelekea Kahama nikiwa na usafiri wangu wa pikipiki aina ya Baja 250, nikiwa katikati ya Pori mara nikaona gari kama inakuja kwa kasi kutaka kunipita, nilipunguza mwendo ili kuipatia nafasi zaidi ipite, lakini badala yake na yenyewe ilipunguza mwendo na kisha polepole ikasimama mbele yangu.

Niliogopa sana nikadhani pengine inataka kuniteka,nami nilipunguza mwendo nikiwa na lengo la kugeuka nilikotoka, lakini kabla sijafanya lolote ghafla nikasikia mlio wa risasi, niliogopa sana nikahisi ni mimi ndo nimepigwa hiyo risasi nikaongeza mwendo kwa kasi sana,niliamua kukimbia mwendo wa kifo, na kweli nilikimbia si mchezo kama km10 baade niliona mbele yangu gari imesimama na kuna kundi kubwa la ng'ombe.

Gari zilikuwa mbili mmoja ikiwa upande kuelekea Kahama na nyingine ikiwa Geita na zote zilikuwa gari mpya sikuweza kujua aina yake ila zilionekana kama Toyota Brevis.Niliendelea na safari kwa hofu kubwa, na cha ajabu mahali pale hapakuwepo mtu yoyote,zaidi ya zile gari na ng'ombe.

Nilipofika katika kijiji kimoja kilichochangamka sana kinaitwa Bukoli, niliogopa kuendelea na safari nikaamua kulala hapo.Napoandika hapa najiuliza maswali mengi na yasiyo na majibu kila leo.Ni nani hao waliokuwa kwenye ile gari iliyonipita na kusimama pale msituni?

Je ni hao kwenye gari ndo walifyatua risasi na kwanini risasi ilifyatuliwa?
hao ng'ombe na zile gari mbili kulikuwa na nini? Na je matukio yote mawili yanaendana au yapo tofauti?Ni siku ambayo sitaisahau kamwe, kesho yake nilifuatilia katika vyombo vya habari ili kujua kama kuna tukio lolote lilitokea lakini hadi leo kimya.
 
Pole sana mkuu ni hatari sana kusafiri umbali mrefu ukiwa alone na ulitakiwa kutoa taarifa polisi ili wafuatilie
 
Unasafiri usiku peke yako ukiwa na pikipiki ulitegemea nini, ni lazima utaingiwa na hofu, mimi huwa nasafiri usiku peke yangu lakini natumia gari na ndani nakuwa na chamoto
 
Ilikuwa ndoto ama?Inakuwaje gari isimame mbele yako ndo wafyetue risasi?
 
Ulifika kwenye kijiji kilicho changamka.... hukutoa taarifa polisi- KWANINI? Unasubiri taarifa kwenye vyombo vya habari- KWANINI? kama wewe hukuripoti, polisi na wanahabari wataambiwa na nani?.... tutaaminije taarifa hii!??
 
  • Thanks
Reactions: R.K
Ilikuwa mwaka 2014,January, saa 2 usiku nikiwa natokea Geita kuelekea Kahama nikiwa na usafiri wangu wa pikipiki aina ya Baja 250, nikiwa katikati ya Pori mara nikaona gari kama inakuja kwa kasi kutaka kunipita, nilipunguza mwendo ili kuipatia nafasi zaidi ipite, lakini badala yake na yenyewe ilipunguza mwendo na kisha polepole ikasimama mbele yangu.

Niliogopa sana nikadhani pengine inataka kuniteka,nami nilipunguza mwendo nikiwa na lengo la kugeuka nilikotoka, lakini kabla sijafanya lolote ghafla nikasikia mlio wa risasi, niliogopa sana nikahisi ni mimi ndo nimepigwa hiyo risasi nikaongeza mwendo kwa kasi sana,niliamua kukimbia mwendo wa kifo, na kweli nilikimbia si mchezo kama km10 baade niliona mbele yangu gari imesimama na kuna kundi kubwa la ng'ombe.

Gari zilikuwa mbili mmoja ikiwa upande kuelekea Kahama na nyingine ikiwa Geita na zote zilikuwa gari mpya sikuweza kujua aina yake ila zilionekana kama Toyota Brevis.Niliendelea na safari kwa hofu kubwa, na cha ajabu mahali pale hapakuwepo mtu yoyote,zaidi ya zile gari na ng'ombe.

Nilipofika katika kijiji kimoja kilichochangamka sana kinaitwa Bukoli, niliogopa kuendelea na safari nikaamua kulala hapo.Napoandika hapa najiuliza maswali mengi na yasiyo na majibu kila leo.Ni nani hao waliokuwa kwenye ile gari iliyonipita na kusimama pale msituni?

Je ni hao kwenye gari ndo walifyatua risasi na kwanini risasi ilifyatuliwa?
hao ng'ombe na zile gari mbili kulikuwa na nini? Na je matukio yote mawili yanaendana au yapo tofauti?Ni siku ambayo sitaisahau kamwe, kesho yake nilifuatilia katika vyombo vya habari ili kujua kama kuna tukio lolote lilitokea lakini hadi leo kimya.
Mkuu naomba uniambie ni pori gani hilo!? Baada ya kuacha lami Nyankumbu hadi kamena hakuna pori kubwa lolote hadi Inkina ama Bukoli pia ukitoka Bukoli hadi Ntonho kabla ya Buyage hapo ndipo kuna pori kidogo (lakini tayari ulikuwa umeshafika Bukoli na tukio limeshatokea. Je uliunganisha kutoka Bukoli hadi Kahama ama ulilala Ilogi (Bugarama ama Kakola)? Je uliendelea hadi Luguya,Segese,Ntobho baadae Kahama? Mkuu bado sijaelewa au ulikuwa umejidunga? Huko ni home napafahamu kimgogomgogo.
 
Hadi raha ukisikia Lunguya, ilogi, kamena, segese...aiseee
 
Back
Top Bottom