Al-Watan
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 11,891
- 14,563
Hana sababu ya kuumba ulimwengu unaoruhusu maovu kwa sababu asili yake ni mazuri na upendo, mazuri na upendo usio mwisho. Uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani anao, ujuzi wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani anao, upendo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani anao.Hapo uliposema hana sababu ya kuumba ulimwengu huu panahitaji maelezo,wewe umejuaje kuwa hana sababu au umekisia tu? na kama umekisia basi maelezo yote yanayofuata ni kwa sababu ya makisio yako tu?
Kwa nini aumbe ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?
Kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati yeye ni Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani ni contradiction.
Ni sawa na kusema mtu yupo Dar physically, halafu kwa wakati huo huo hayupo Dar physically.
Ni kitu ambacho hakiwezekani kuwepo.
Hivyo, Mungu huyo hayupo.