Tukio gani linakufanya uamini kuwa Mungu yupo?

No Escape

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
6,663
7,774
Lazima kila binadamu anaamini uwepo wa Mungu haijalishi Dini wala nini ila kuna jambo labda unahisi ni la kipekee linatokea hapa Duniani au limewahi kutokea hata kwako wewe mwenyewe mpaka limekufanya uamini kweli Mungu yupo.

Kwa mfano mimi kila ninapoona giza linaingia na halafu tena kesho yake kunakucha yaani kunakucha. Hii kwangu ni sababu tosha ya kuamini uwepo wa Mungu, hakuna mwanadamu mwenye uwezo wa kulifanya hili Duniani kote.

Ahsanteni, Asubuhi njema.
 
Tukio la kuwepo kwangu nikiwa na umbo maalumu lilisanifiwa vizuri.Nina milango ya fahamu ambayo imetengenezwa kwa mfumo wa ajabu na inafanya kazi kwa namna ya pekee.Umbo langu lenyewe limetengenezwa kwa materials za hali ya juu.Mifumo yote ya mwili kuanzia dygestive system,blood system,nervous system nk imepangiliwa kwa ustadi wa hali ya juu kiasi cha kunipa imani juu ya nguvu ya aliyeunda mifumo hii.Ningekuwa sijaumbwa mimi nadhani nisingekuwa na umbo maalum zaidi ya kuwa na irregular shape.God Is Great..
 
Nyusi zangu!!

Kila nikifanya mazoezi huwa natokwa ns jasho lenye ladha ya chumvi ambalo kiuhalisia likiingia machoni ntapata tabu ya muwasho wa macho!

Nyusi hunisaidia kukwepesha jasho lisiwe na mtiririko ulionyooka kwenda machoni. Kwa usanifu huu naamini kuna suprime Being aliyehusika na hii design.

so, God is there and here people!!!!

[HASHTAG]#wadadamnaotindanyusimunguanawaona[/HASHTAG]
 
Kuzaliwa ukiwa hujitambui na kadri siku zinavyozidi kusonga. Unakuta unajitambua na kujijua ww ni nani bila ya kufundishwa na MTU, na pindi kifo kinapo tupata. Haijalishi unahitajika vipi duniani kwa wakati huo, siku yako ikifika lazima nafsi yako itaonja umauti haijalishi uko wapi na unafanya nini.
HAKIKA MUNGU YUPO
 
Mpaka sasa sijajua kwanini na ujanja wangu wote huu mimi binaadam, nashindwa kumrudishia uhai binaadam au kiumbe mwingine yeyote yule???.

Ni nini kigumu!!!!, hii ni ishara kwamba kuna nguvu inayoamua yaliyopo bila kupingwa.
 
Lazima kila binadamu anaamini uwepo wa Mungu haijalishi Dini wala nini,Ila kuna jambo labda unahisi ni la kipekee linatokea hapa Duniani au limewahi kutokea hata kwako wewe mwenyewe mpaka limekufanya uamini kweli Mungu yupo.Kwa mfano mimi kila ninapoona giza linaingia na halafu tena kesho yake kunakucha yaani Kunakucha! Hii kwangu ni sababu Tosha ya kuamini uwepo wa Mungu,Hakuna mwanadamu mwenye uwezo wa kulifanya hili Duniani kote....Ahsanteni,Asbh njema.
Huhitaji Mungu kuelezea hilo, unahitaji kujua dunia inavyojizungusha tu.
 
Back
Top Bottom