Tukimaliza awamu hii bila STATE OF EMERGENCY tumshukuru Mungu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
299,604
752,011
State of emergency ni hali ya hatari, kiongozi wa nchi anapotangaza hali ya hatari basi karibia kila kitu kinakuwa na ukomo, kuanzia mitandao ya kijamii inaweza kuzimwa yote, mijadala na hata muda wa kulala ama kuamka, kukusanyika nk nk, hali ya hatari si jambo jema kwakuwa uhuru kwenye kila jambo unakuwa na kikomo... Limited freedom
Magufuli yuko kwenye pressure kubwa sana ya kujaribu kuweka mambo sawa.. Kuna wakati naona kabisa hastahili kila lawama,....wa kulaumiwa pakubwa sana ni JK aka Mr dhaifu
Nchi ilifika mahali ikawa kwenye auto mode, miaka kumi ya JK ilizalisha milima ya matatizo ambayo ndio hii Leo hii Magufuli anajaribu kuisawazisha
Kuna hulka Kama hulka na mitazamo pia na kila mwanadamu ana madhaifu yake, Magufuli si malaika kwamba anaweza kufanya kila kitu kwa ukamilifu wake, kuna mahali anapatia na kuna mahali anakosea, wote tuko hivyo, hakuna mkamilifu
Mwanzoni ilionekana ni Kama upinzani ndio unamuandama sana Magufuli lakini kadiri siku zinavyosonga na mambo yanavyokwenda hata watu wake ndani ya chama wanaanza kuonyesha upinzani wa wazi kabisa
Hili si jambo la afya sana... Na Inawezekana kabisa likawa linamuumiza Magufuli pakubwa tu.. Inawezekana kabisa nia yake ni safi dhamira yake ni nzuri lakini anaona kabisa watu hawamuelewi
Hili limejidhihirisha juzi alipotoa angalizo kwa wamiliki wa vyombo vya habari.... Ile sauti ilibeba uzito wa kile alichomaanisha. Hatanii na hashindwi asilani kufanya kweli
Ukichangizwa na wapinzani wako haiumi sana ila unapoona kuna uasi wa wazi ama wa kificho unaanza kujitokeza ndani ya watu wako mwenyewe kitisho kinakuwa dhadhiri na inapofikia hapo hakuna njia nyingine bali kuchukua uamuzi mgumu ili uweze kufanya kazi kwa amani.... Wengine hutangaza hali ya hatari na jeshi kushika hatamu
Chochote kitakachotokea Magufuli hana mzigo mkubwa wa lawama kama Kikwete...wakati ule tulipanda sasa tunavuna
Tuangalie hili kwa asili yake tutaona wazi tatizo lilianzia wapi.....

NB: hii inaweza kuwa post yangu ya mwisho kwenye jukwaa la siasa....
 
Chamsing maguful asiangalie matakwa ya nan anampenda nan hampend but awe na msimamo na kazi na pia awe anakaribisha ideas vitu ambavyo naamin anafanya.
Hata jakaya alichukiwa , mawazir wake waligeuka wapigaji ndio maana mirad ya maendeleo ilikuwa inflated. Mradi wa reli ya kisasa inflated, mradi wa airport inflated, mradi wa hostel inflated.
Soo hata kama mtu yupo karibu yako na haeleweki eleweki wacha amchukie rais.
Ukicheka na nyan utavuna mabua mjomba.
Jaribio la kupindua nchi probability ya kufanikiwa ni 0.5% na majaribio mengi yamefel.
 
PhD in chemistry holder trying to opt political science in final year! What do you expect ? Nothing but doomed state.
Tunapishana padogo sana kila upande una nia njema....nia njema ya kujenga Tanzania mpya Tanzania ya neema na ustawi wa watu wake... Lakini hatuaminiani, ikitokea siku tukafanya colabo ya wapinzani na ccm things will change in a very mean time
Ila tukizidi kushupaza shingo na kukaziana misuli huku tukikamiana kwenye kila jambo 2020 itafika hatujafanya kitu
Tunahitaji maridhiano
 
Mkuu heshima kwako.
Kwanza sidhani kitu kama hicho kinaweza tokea maana kinaweza shuttdown economy,na kila mtu akaamua ku pack na kuondoka.
We have tight security system
Kile Rais Maguful anaweza fanya ni kutoa tu amri ya kuzuia mijadala ya kisiasa na watu wakaelekezaa wakafanye kazi..... Which ni ngum kidogo ku digest.

Kingine ni kuwashikilia active radicles had atakapomaliza awam yake..... Kigum nacho kidogo

Kingine ni kuamrisha vyombo vya habar kutorusha mambo yanayoenda kinyume na nia yakr nzur ya kutuletea maendeleo.. Which is easier.. MWAKYEMBE CHAPA KAZI...
IMG-20170325-WA0006.jpg
 
Ukifika huko ni sawa tu lakini chanzo ni "kutojitambua, kutojiamini n.a. kukurupuka kwa utawala" Jambo jema halilazimishwi na baya hujiondoa lenyewe baada ya uelewa kupatikana.Wakati wa harakati za uchaguzi, mgombea mmoja alisema na kusisitiza "elimu". Wengi hasa wasiompenda hadi leo hawataki kuona mantiki.Lakini ukweli ni kuwa ukombozi wa kweli utapatikana tu uelewa ukiwa kwa wengi.Pamoja na viashiria vyoote vya ukengeufu wa utawala huu wapo wanaoshangilia,kuchekelea na kushabikia.Mawakili wameonyesha njia, ni jukumu la raia wengine kukataa kupelekeshwa.Hali ya hatari itakuja kutokana na upuuzi wetu.
 
Tunapishana padogo sana kila upande una nia njema....nia njema ya kujenga Tanzania mpya Tanzania ya neema na ustawi wa watu wake... Lakini hatuaminiani, ikitokea siku tukafanya colabo ya wapinzani na ccm things will change in a very mean time
Ila tukizidi kushupaza shingo na kukaziana misuli huku tukikamiana kwenye kila jambo 2020 itafika hatujafanya kitu
Tunahitaji maridhiano
Kweli Mzee .kwa kuongezea tu no 1 anahitajika awe na hekima ya uongozi anadhani kuwa no 1 in kujua kila kitu kumbe angeweza kushauriwa vizuri mambo yakaenda
 
Back
Top Bottom