Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,110
Ajali za barabarani ni moja kati ya sababu zinazosababisha upotevu wa nguvu kazi ya taifa. Imekuwa kawaida kwa magari ya abiria kuzidisha mizigo wanakuwa wanawaomba watu wasogee mbele pindi wafikapo kwenye mizani ili kukwepa faini.Sasa leo,mi nasafiri kutoka mwanza kuelekea Dar.Tulipofika karibu na mizani Konda kama kawaida:Mliokaa seat za nyuma naomba msogee mbele...Mi nimegoma then nikauliza kwanini nikusaidie wakati unahatarisha maisha yangu? Tumezozana kidogo na baadhi ya abiria wakanitaka nikubaliane nae ili tuwahi but nimegoma mwanzo mwisho wao wakasogea then tukapita.Vp mwenzangu umeshawahi kumbana na usumbufu huu!