Tukifika kwenye mizani nitawaomba abiria msogee mbele

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,110
Ajali za barabarani ni moja kati ya sababu zinazosababisha upotevu wa nguvu kazi ya taifa. Imekuwa kawaida kwa magari ya abiria kuzidisha mizigo wanakuwa wanawaomba watu wasogee mbele pindi wafikapo kwenye mizani ili kukwepa faini.Sasa leo,mi nasafiri kutoka mwanza kuelekea Dar.Tulipofika karibu na mizani Konda kama kawaida:Mliokaa seat za nyuma naomba msogee mbele...Mi nimegoma then nikauliza kwanini nikusaidie wakati unahatarisha maisha yangu? Tumezozana kidogo na baadhi ya abiria wakanitaka nikubaliane nae ili tuwahi but nimegoma mwanzo mwisho wao wakasogea then tukapita.Vp mwenzangu umeshawahi kumbana na usumbufu huu!
 
Mi yalinikuta mwaka jana mwishoni nikiwa natokea moshi kuja dar,
walinibana nisogee mbele nikagoma kata kata na nilikuwa na binti yangu naye nikamkataza kwenda mbele,
waliniona noma na wakati wa kushuka wakasema bahati yako ungekuwa na
mzigo hata kilo tano ungelipia hela. Abiria inabidi tuwe tunaangalia vitu vya kukubali
siyo kila kitu tunasukumwa sukumwa tu.
 
Mimi pia yamenikuta hayo. Ukweli ni kwamba wanataka usogee mbele ili kama gari imezidi kidogo nyuma ibalance!
 
Ajali za barabarani ni moja kati ya sababu zinazosababisha upotevu wa nguvu kazi ya taifa. Imekuwa kawaida kwa magari ya abiria kuzidisha mizigo wanakuwa wanawaomba watu wasogee mbele pindi wafikapo kwenye mizani ili kukwepa faini.Sasa leo,mi nasafiri kutoka mwanza kuelekea Dar.Tulipofika karibu na mizani Konda kama kawaida:Mliokaa seat za nyuma naomba msogee mbele...Mi nimegoma then nikauliza kwanini nikusaidie wakati unahatarisha maisha yangu? Tumezozana kidogo na baadhi ya abiria wakanitaka nikubaliane nae ili tuwahi but nimegoma mwanzo mwisho wao wakasogea then tukapita.Vp mwenzangu umeshawahi kumbana na usumbufu huu!

Mi mara nyingi tu niligoma tena yale ya Dar to Nairobi ndo wana mchezo huo sana
 
Ni vizuri watu wa mizani wawe wanaingia na ndani ya mabasi wanayopima ili kuangalia kama kuna watu walionyanyuliwa kwenye mizani. Naamini na wao wanasafiri watakuwa wanaijua hii tabia.
 
polisi,dereva,trafiki,wanaopima mizani wooooote ni wadhaifu af lao ni moja kwa hiyo hapo anaeteseka ni mm ww.
 
yaani mmenipandisha ghadhabu ghafla, nimejikuta nimekataa kusogea kwenye kochi ili mtoto akae.

Duh, kumbe niko home, nyie watu kunikalisha kwenye tuthpick sitaki.
 
Back
Top Bottom