Tukiendeleza utamaduni wa kuchagua viongozi wa serikali kwa ushawishi wa viongozi wa dini tutapotea

Nathason2

JF-Expert Member
May 20, 2015
598
680
Nakumbuka kwenye uchaguzi wa mwaka 2005 nilikuwa na uelewa mdogo hususani kwenye masuala mapana ya siasa za nchi yetu sikutaka kujihusisha na siasa kwa kuwa niliamini kufanya hivyo ni kupoteza muda wangu wa kujipanga kimaisha,siku moja nikiwa kwenye Ibada ya jumapili nilishituka kumsikia padri niliyemwamini akituelekeza waumini kuwa MH JAKAYA MRISHO KIKWETE ndiye chaguo la mungu kwa kuwa maneno yale niliyasikia kanisani na ukizingatia nilikuwa na uelewa mdogo wa siasa zetu ilinipasa kuyameza kama yalivyo.

Baada ya miezi kadhaa kupita MH KIKWETE akachaguliwa kuwa rais wa nne wa TANZANIA kwa kuwa wengi wetu tuliyaamini maneno yale ya makanisani na misikitini kuwa yeye MH KIKWETE alikuwa ni chaguo la mungu na atatufikisha kwenye MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA, bado nayakumbuka mafundisho yale jinsi yalivyonighafilisha baada ya maisha kunibana kutokana na mfumuko wa bei,kashfa za ufisadi ambazo mh kikwete alizifumbia macho chaguo la mungu likawa ndio TATIZO KWA KUBWA KWA WATANZANIA na hapo nikaanza kuchallenge maamuzi yangu ya kufanya uamuzi wa kumchagu JK kwa kuwasikiliza watumishi wa mungu na niaanza kuchallenge kauli wanazozitoa viongozi wetu wa dini na baadae nikagundua kuwa huwa ni maneno yao Binfsi.

Mwanzoni mwa mwezi May mwaka huu sikumbuki vizuri ilikuwa ni tarehe ngapi mtumishi wa mungu BAHATI BUKUKU alitoa nyimbo yake mpya ya LOWASSA akatuambia kuwa yeye lowasa amepakwa mafuta kama daudi,unahekima kama suleimani n.k na mengine mengi,ukitaka kuipata link hii hapa http://www.hulkshare.com/danimwanga/bahati-bukuku-lowasa

Siku lowassa alipotangaza nia ya kuomba ridhaa ya wana ccm wamchague apeperushe bendera ya CCM kwa nafasi ya Uraisi nilimsikia mchungaji wa kanisa la ufufuo na uzima Mchungaji GWAJIMA akiwaambia Watanzania kuwa Asiyempenda au kumkubali Lowassa akale malimau.

Kauli hizi na nyingine nyingi zinatolewa na watu ambao tunategemea wanatupandia sisi mambo mema ya Rohoni Jambo moja tu nataka kuwauliza Wana JF je haya maoni na mitazamo ya viongozi wetu wa dini na waimbaji wa injili kama tulivyoshuhudia safari hii kwa dada yetu BAHATI BUKUKU huwa ni mitazamo inayotokana na wao kumkubali mtu kwa dhamira za kweli au huwa ni njaa zao na uroho wa kupata chochote kutoka kwa wanasiasa

HITIMISHO:Tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi october niwaase ndugu zangu WATANZANIA Tuache utamaduni huu wa kufanya maamuzi ya kuchagua kwa kutegemea ushawishi wa viongozi wetu wa dini kwani tutalifikisha pabaya Taifa letu,ni vyema wananchi tukafanya maamuzi yetu binafsi ya kuamua nani tumchague na ni kwa sababu gani tunamchagua kuliko kuchagua kwa kutegemea ushawishi wa viongozi wa dini kwani wengi wao wanayatumikia matumbo yao na sio kutoa maoni yenye manufaa kwa waumini wao,hata hivo wao ni wana damu na nyama kama sisi hivo wanaweza kumpenda au kumchukia mtu(wanasiasa) pasipo na sababu za msingi na hivo wakatushawishi tumchague mtu ambaye hatufai.
 
Kuna waliomtungia Nyimbo za kwaya Mwigulu Mchemba kuwa ndiye rais acha yule askofu aliyesema auawe lowasa asiposhinda,....hizi taasisi za dini zimekaa kimaslahi mno siku hizi
 
Umeongea maneno yenye BUSARA sana.Ila viongozi wa kanisa watusaidie kuomba ili tupate chagua sahihi.Chaguo la Mungu kweli.
 
Kuna waliomtungia Nyimbo za kwaya Mwigulu Mchemba kuwa ndiye rais acha yule askofu aliyesema auawe lowasa asiposhinda,....hizi taasisi za dini zimekaa kimaslahi mno siku hizi

kwa hiyo huyo askofu yuko tayari kufa? ukizingatia jina lowassa limeshaondolewa kwenye kinyang'anyiro ndani ya ccm au anasubiri plann B ya lowasa Ifail ndio afe? mliokaribu na mwiguli mwombeni akabadilishe zile status zake kwenye mawe maana anaweza potosha historia kwa kudai alikuwa raisi 2015
 
Back
Top Bottom