Tukienda hivi kama taifa hatufiki

Tukienda hivi kama taifa hatufiki

jindundu

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2025
Posts
679
Reaction score
580
Asalaam Alaykum, Bwana Yesu asifiwe, Shalom, Tumsifu Yesu Kristo.
Kutokana na mambo yanayoendelea nchini kwa Sasa Kisiasa na kijamii.

Nami nikiwa mmoja wa raia wa Tanzania wanaotamani kuona Haki, amani na maendeleo yanatamalaki katika Taifa letu, kuanzia kesho nitaanza kuandika mfululizo maoni, na ushauri wa nini kifanyike wakati huu tunapoelekea kwenye zoezi muhimu la Uchaguzi Mkuu 2025.

Nitashauri juu ya kesi zinazomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.

Nitashauri juu ya matukio ya suala baya la utekaji na mauaji linavyoichafua nchi yetu ndani na nje.

Nitashauri kuhusiana na hoja za Ndugu yetu Humphrey Pole pole kwa kina na kwa kirefu.

Pia nitashauri kuhusu mwelekeo na matumaini ya watanzania kabla ya Uchaguzi Mkuu na matarajio baada ya zoezi hilo Tukufu.

Tukosoane kwa hoja na kustahimiliana. Kwa kufanya hivi tutaimarisha Umoja na Mshikamano wetu kama Taifa.

Ni Mimi ndugu yenu niliye mdogo kuliko wote, naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom