AFYA:
Muhimbili imeboreshwa
Wagonjwa wanakwenda kutibiwa nje hada vigogo wamepungua
CT SCAN Zinapiga kazi
Hospitali yaMlongazila imeanza kazi
Huduma ya dialysis kuanza kutolewa Mlonganzila
Huduma za Tiba ya mionzi kutolewa kwenye hospitali za kanda
Hospitali za mikoa zimepandishwa hadhi
Ujenzi wa Theatre kwenye vituo vya Afya umepamba moto
Bajeti ya dawa imepaa kutoka bilioni 20+ hadi bilioni 200+
MSD inaagiza dawa kutoka kwa Manufacturers na sio wapiga dili
Upatikanaji wa dawa muhimu ni zaidi ya 80%
Coverage ya BIMA ya afya kwa wote inaendelea vyema refer Toto Afya cards n.k
Kitengo cha kupambana na Majanga kimeboreshwa
Matukio ya ubakaji na uonevu wa kijinsia yanapungua
Albino wapo salama
Viwanda vya dawa vinajengwa
........UNATAJA NIENDELEE.....?TUSIKIMBIANE HAPA!
Kwenye afya ni bora ungekaa kimya. Kwasababu Mosi, umeaacha kuzungumzia mambo ya maana kama Maternal morality, perinatal death na infant mortality badala yake unaabdika none sense hapa.
Pili, Uhaba wa vifaa tiba bado ni tatizo katika vituo vya afya na hospital za serikali, si ajabu kukosa vitu vidogovidogo kama syringes na gloves
Tatu, Vituo vya afya na hospitali za serikali ukiachilia mbali uhaba wa wauguzi na madaktari bado hata wengi waliopo hawana mafunzo toshelevu au mafunzo stahiki. Wengi ni wababaishaji kwa sababu wamewekwa kwenye nafasi ambazo hawakustahili, wanatumia trial and error. Kwa mfano ukiangalia Mtaala wa uuguzi, Muuguzi wa cheti (enrolled nurse) hufundishwa kumanage normal labour peke yake, abnormal labour tunawafundisha kumuandaa mama kwa referral. Sasa maajabu ya serikali inawaajiri hawa na inawapeleka hospitali za mikoa na shift anaingia yeye na medical attendant (ambaye si nurse)! Halafu mnataka eti muujiza utokee maternal deaths zipungue!!
Nne, Nurse patient ratio na doctor patient ratio ni kubwa mno! Mimi ninashangaa kwa nini wauguzi bado wanaendelea na kazi, sijui ni umasikini wao na familia zao. Nimebahatika kutembealea na kufanya kazi katika hospitali, vyuo na vituo vya afya tofauti tofauti, miongoni mwao vipo vya serikali na vya kanisa. Nilichojifunza ni kwamba matatizo ya vituo vya afya na hospitali za serikali yanafanana kote. Katika kituo kimoja nilikuta kazi wanazofanya manesi wanne na medical attendant wawili hospitali nilotoka, wao atafanya nurse mmoja au wawili!!! Kwa nini watu wasife??
Tano, sababu ya baadhi ya referrals ni za ajabu. Ati mama anakuwa reffered kwenda hospitali ya wilaya kisa ultrasound!!! Yaani unampandisha mama kwenye ambulance hadi hospitali ya wilaya kisa ultrasound!! Mmeweza kununua ambulance lakini kipimo kama ultrasound mmeshindwa hadi muingize siasa!!!
Sita, ile mishahara kuanzia Medical doctor hadi enrolled nurse inasikitisha! Ninashangaa kwa nini bado wanaendelea na kazi na wako comfortable kabisa.
Mwisho, ingawa serikali hii imeonyesha madhaifu mengi lakini kuna baadhi ya mazuri mh magufuli anastahili pongezi kwa upande wa kudhibiti upiga dili MSD na idara zingine.
Mwisho kabisa. Serikali haijawa serious na afya za watanzania thus why wao wanaenda India, ujerumani, Nairobi, South Africa, Ubelgiji na kwingine.