nasrimgambo
JF-Expert Member
- Jan 10, 2017
- 1,898
- 2,459
Wakubwa shikamoni,
Mimi mwezenu nina katabia ka kufuatilia sana habari juu ya miradi ya maendeleo ya maeneo mengi ya nchi yetu, tena huwa nafarijika sana ninaposikia miradi fulani ikisonga mbele.
Katika miradi niliyokuwa nina shauku nayo kuifuatilia nilipoisikia tu kuwa inakuja, ni huu mradi wa Kigamboni new city ambao uliimbiwa sana enzi za awamu ya nne, hasa zama ambazo mama yetu Tibaijuka alipokuwa Waziri wa masuala ya ardhi, na hata enzi mkubwa Magu alipokuwa waziri wa ujenzi.
Ila katika tafiti zangu za juu juu siku hizi huu mradi siusikii hali yake inaendelea vipi, maana kimya cha wadau wake wa wizara na hata Makonda mkuu wa jiji, kimetamalaki
ni kama huu mradi umesahaulika.
Sasa huu uzi nimeuanzisha ili kukata kiu yangu na yeyote atakaye kufahamu yanayoendelea juu ya Kigamboni new city.
Wenye kufahamu masuala yoyote juu ya mradi huo, karibuni kutujuza.