Tujue kwanini Wahehe wepesi wa hasira na kujinyonga?

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Ukitembelea mkoa wa Iringa unakutana na visa vingi vya watu wa jamii ya Wahehe kuwa na hasira na kujinyonga kwa haraka.Hata humu makazini unaweza kukutana na mtu wa Uheheni akawa mpole lakini ni mwingi sana wa hasira.Kumekuwa na simulizi na ushuhuda wa moja kwa moja ya jinsi Wahehe wanavyojinyonga au kuwa na hasira mpaka kuzila mambo,wanasema Wahehe ni watu wenye kiburi cha chinichini,hasira na maamuzi "magumu" ikiwemo kuuwa mtu au hata kujinyonga.

Hizi hazibaki kuwa ni simulizi tu zisizo na ushuhuda kama zile za wahehe kula mbwa,shuhuda za Wahehe kuwa na hasira,kiburi na hulka za kujinyonga tumezishuhudia,Wadada wengi wa ndani(House Girls) ni Wahehe,wengi wana matukio ya kumfanyia kitu mbaya tajiri kama watazulumiwa au kunyanyaswa,wapo walioamua kujinyonga ndani ya nyumba za maboss wao au hata kuweka watoto kwenye friji na wao kuchukua uamuzi wa kujiuwa,kisa tu wamekasirishwa na maboss wao.Wapo wanaume wa Kihehe ambao wakikasirishwa au kudharauliwa huchukua uamuzi wa kujinyonga baada ya kuuwa.

Inasemekana Muhehe hataki "dharau",hawapendi kujipendekeza wala kuomba omba,wao kila kitu utasikai wanasema "Ndimgaya sida" yaani "hana shida" hata kama atakuwa na shida kubwa,lengo ni kutoonekana mnyonge au muombezi,ni bora akafa na tai shingoni.

Kuna matukio mengi ya kihistoria juu ya Wahehe na hasira na kujinyonga,inaanza wakati wa mkoloni na Mtwa Mkwawa,jeshi la Mkwawa lilipomuuwa Jemedari wa Kijerumani Zelewisky na maiti kurudishwa Berlin,zipo simulizi za Mkwawa kujinyonga na mambo kama hayo.

Iringa ina historia ya "kuadabisha" viongozi wa Serikali wanaokuja bila "hodi",kabla ya tukio la Mwamwindi na Dr Kleruu,kulikuwa na tukio la Mkuu wa Mkoa(RC) miaka ya 1960's akijulikana kwa jina la Said Shamshana,huyu alikuwa RC wa pili baada ya Uhuru,akiwa Iringa tarehe 09 Desemba msimu wa kilimo,aliwahimiza Wananchi walime sana mazao ya chakula ili walau wapate kuuza na kujiongezea kipato,watu waliitikia na wakalima chai,kahawa na alizeti kwa wingi kiasi wakasahau kulima mazao ya chakula,mwaka uliofuata kukawa na uhaba wa mahindi,kiasi Iringa Milling Machine ikakosa mahindi ya kuandaa unga,wakati huo Iringa ikifahamika kama "The basket of Tanzania" kwa umahiri wa kilimo cha mahimdi Isimani(Tuliisoma Geography shule ya Msingi).

Tarehe 07/07 siku ya Wakulima,RC akaja uwanja wa Samora kafura sana,akawatukana Wahehe mbele ya wake zao kuwa ni wapumbavu,wamelima mazao ya biashara bila uwiano na chakula,hivyo kusababisha uhaba wa chakula...Matusi yaliwaingia kwelikweli,Akainuka mzee mmoja akifahamika kwa jina la Mzee Mwakivike,asili yake kijiji cha Lumuli-Ulete,akiwa na mgolole wake begani,akawa anapandisha jukwaani aliko RC na watu wa itifaki,akiwemo Marehemu Hussein Shekilango,wakati huo akiwa kama kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo wa Mkoa,Mzee Mwakivike akiwa na mwendo wa madaha,watu wakidhani ni Mzee wa TANU akienda kukidhi muktadha wa itifaki ya chama,alipofika meza kuu akamramba kerebu kadhaa RC Shamshama bila taarifa,taharuki ikazuka na Mzee akakamatwa,katka maelezo yake akasema amechukua hatua hiyo baada ya kutukanwa mbele ya mke wake na "mtu wa kuja",ambaye mwaka jana alihimiza walime mazao ya biashara halafu mwaka huu anawatukana.Shamshama akahamishwa na Nyerere maana wazee wa mji waliapa kumtoa koromeo.Hizi ni hasira na hulka za Wahehe...visirani,hasira,kiburi na kujitundika.

Simulizi wa Mwamwindi sio ngeni,anajulikana jinsi alivyomuuwa RC Dr Kleruu,akampakia kwa gari lake na kumzungusha kwenye vilabu vya pombe Iringa mjini,baadae akapeleka maiti Central Police na akiwa ameweka maiti kwenye gari la mkuu wa mkoa,na alipofika akawambia polisi "chukueni mzoga wenu,hivi huyo aliyemleta huyu huku hakumwambia kuwa huku kuna wanaume?",baada ya hapo ni kesi na hatimaye kunyongwa,kuna simulizi za Wazee kuwa Nyerere hakutaka kuidhinisha Mwamwindi kunyongwa,na aliomba nafasi ya kuonana na Mwamwindi ili kujua ni kwanini hasaa aliamua kumuua RC DR Kreluu,RC kijana na msomi wa ngazi wa udaktari,kifo kilichomstua sana Nyerere na kuhisi harufu ya uasi,lkn majibu ya Mwamwindi kwa Nyerere yalikuwa ya "kiburi,hasira na dharau".Hatimaye Mwamwidi akapigwa kitanzi gereza la Isanga Dodoma....Hii ni tabia nyingine ya Wahehe kuwa na kiburi,hasira na kuwa tayari kufa...Sijui ni kwanini??
Kuna simulizi nyingi na za kutosha juu ya tabia hii ya Wahehe(Watani zangu),wanasifika kwa hasira,kiburi(wao huita kidada) na kujinyonga,waliwahi muachia Nyerere viti kwenye mkutano kijiji cha Tanangozi baada ya Nyerere kusababisha vilabu vya ulanzi kufungwa ili wananchi wakamsikilize kwenye mkutano,ajabu Nyerere akachelewa nyuma ya muda aliokuwa ametarajiwa kufika...walichofanya na kumsubiri,ile anaanza kuhutubia watu wakanyanyuka...TUJUE,KWANINI WAHEHE WANA HASIRA NA KUPENDA KUJINYONGA???
 
Hawa jamaa kwa kujinyonga kwao Ni kama msukuma Na baiskeli. Basi demu moja tulizinguana akanitumia text kuwa anajinyonga Na kuniambia kuwa ntawajibika basi nkaogopa kwelikweli ukizngatia hulka Yao .
 
yaani nimecheka hii story,JF Balaaaa

Mleta uzi amejitahidi kuchimbua yote yanayowahusu kabila hili.Kwetu wasomaji angeileta kama simulizi na uhalisia wa kabila hili la Wahehe zaidi ya kutuuliza ni nini kinachopelekea hayo yote aliyoyataja kwani sidhani kama kuna sifa aliyoiacha.
 
mkoa wa asili ya mwandishi watu hawjinyongi?
 
Tunasimamia utu wetu, tunajua kuwa utu wetu ni jambo muhimu zaidi, tunakua wapole kwasabubu tunafikiri sana kabla ya kutenda na sisi kwa asili sio wagomvi na hatupendi ugomvi ila ole wako unionee hasa kwa jeuri ya nguvu, pesa au cheo... Shauri hilo ni Mungu ndiye ataamua sio mwanadamu. Ulichonacho ni chako usinitishe utaumia, ukinidharau hata ukinikuta nakufa usinisaidie, ole wako unisaidie nikipona unalo, kwa mke wangu ni jehanam usisogee, usiingilie maslahi yangu ntadeal na wewe perpendicularly, mazuri yako mpelekee mkeo kwangu leta heshima. Ukinidharau na ukanishinda nguvu sitaweza kubeba huo uchungu nitarest in peace
Najivunia unyalukolo wangu.
Ndio hivyo yaani
 
Kama kweli wahehe wapo hivyo ulivyosema,, hebu niambie tangu mwaka huu uanze kuna wahehe wangapi wamejinyonga,,? acha kuongea kwa hisia brother! Je, kama hamna ina maana kipindi hicho chote hamna mhehe yeyote aliekasirka?
 
Mleta uzi amejitahidi kuchimbua yote yanayowahusu kabila hili.Kwetu wasomaji angeileta kama simulizi na uhalisia wa kabila hili la Wahehe zaidi ya kutuuliza ni nini kinachopelekea hayo yote aliyoyataja kwani sidhani kama kuna sifa aliyoiacha.
upo sahihi mkuu@geraldkowero,japo uwasilishaji na story yenyewe vinachekesha sana
 
Acheni kukariri, hakuna wahehe wanaojinyonga kama mnavyofikiria,
Wahehe ni wakarimu sana ila usije ukautumia vibaya huo ukarimu ukaleta dharau ,
But hizo story za kujinyonga nadhani ni story za utani tu maana hata mleta Uzi ukuliulizwa umeshuhudia matukio mangapi ya wahehe kujinyonga nadhani utakuwa hauna kabisa.
 
Kama kweli wahehe wapo hivyo ulivyosema,, hebu niambie tangu mwaka huu uanze kuna wahehe wangapi wamejinyonga,,? acha kuongea kwa hisia brother! Je, kama hamna ina maana kipindi hicho chote hamna mhehe yeyote aliekasirka?
Mi najua wasichana wa kihehe ndio wadada wa home aka beki tatu
 
Tunasimamia utu wetu, tunajua kuwa utu wetu ni jambo muhimu zaidi, tunakua wapole kwasabubu tunafikiri sana kabla ya kutenda na sisi kwa asili sio wagomvi na hatupendi ugomvi ila ole wako unionee hasa kwa jeuri ya nguvu, pesa au cheo... Shauri hilo ni Mungu ndiye ataamua sio mwanadamu. Ulichonacho ni chako usinitishe utaumia, ukinidharau hata ukinikuta nakufa usinisaidie, ole wako unisaidie nikipona unalo, kwa mke wangu ni jehanam usisogee, usiingilie maslahi yangu ntadeal na wewe perpendicularly, mazuri yako mpelekee mkeo kwangu leta heshima. Ukinidharau na ukanishinda nguvu sitaweza kubeba huo uchungu nitarest in peace
Najivunia unyalukolo wangu.
Ndio hivyo yaani

Pamoja sana nami mnyarukolo mwenzio
 
Hawa jamaa kwa kujinyonga kwao Ni kama msukuma Na baiskeli. Basi demu moja tulizinguana akanitumia text kuwa anajinyonga Na kuniambia kuwa ntawajibika basi nkaogopa kwelikweli ukizngatia hulka Yao .
bado upo nae?
 
Back
Top Bottom