Tujizuie Kuwa na Imani Kama ya Tomaso

Tujizuie Kuwa na Imani Kama ya Tomaso

John Achila Mukumwa

Senior Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
110
Reaction score
210
Tujizuie Kuwa na Imani Kama ya Tomaso

Tomaso ni Nani
Katika Agano Jipya, Tomaso, ni mmoja kati ya mitume 12 wa mwanzoni waliochaguliwa na Mwokozi wakati wa huduma Yake katika mwili wenye kufa
(Mathayo 10:2-3; Yohana 14:5). Ingawa Tomaso alitia mashaka juu ya ufufuko wa Yesu, hadi yeye mwenyewe alipomwona Mwokozi, uaminifu wake mkubwa ulimfanya awe radhi kukabiliana na mateso na mauti pamoja na Bwana wake (Yohana 11:16; 20:19-29).

Tomaso alizaliwa huko Galilaya kwenye Taifa Teule la Israeli katika karne ya kwanza. Aliitwa Teoma maana yake Pacha (Yohana 11:16).

Anaaminika kuwa alifanya mengi ya ushujaa wake wa uinjilisti nchini India, ambapo hatimaye aliuawa kwa kuchomwa mikuki na maaskari wanne mgongoni na kutokezea tumboni huko India, katika safari zake kama mumisionari wa makanisa ya huko.

Maelezo kuhusu tukio la Yesu na Tomaso
Tomaso hakuwepo Yesu alipotokea jioni ya ufufuo wake na hivyo kukosa kitia-moyo cha kwanza kilichopokelewa na wengine.

Kitabu cha Yohana 11:16; 20:19-31, kimesimulia kuhusu tukio kati ya Tomaso na Yesu
.
19 Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.
20 Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana.
21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.
22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.
23 Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.
24 Walakini mmoja wa wale thenashara, Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao, alipokuja Yesu.
25 Basi wanafunzi wengine wakamwambia, tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo.
26 Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu.
27 Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye.
28 Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu!
29 Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.
30 Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki.
31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.

Hadithi kuhusu Tomaso ni onyo kwa wanadamu

Kutokuamini kwa Tomaso
Tomaso anawakilisha watu ambao wanahitaji uthibitisho wa kimwili au wa moja kwa moja ili waamini mambo ya kiroho. Imani yake ilitokana na kuona na kugusa, badala ya kuamini bila kuona.

Maneno ya Yesu kwa Tomaso

Yesu alimwambia Tomaso: "Kwa sababu umeniona, umesadiki; heri wale wasioona wakasadiki" (Yohana 20:29). Hii inaonyesha umuhimu wa imani ya kweli inayotegemea ushahidi wa kiroho, si wa kimwili tu.

Funzo kwa Wakristo
1. Tuwe na imani isiyo na shaka
Wakristo wanaitwa kuamini bila kuona (Waebrania 11:1: Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana).
2. Yesu huheshimu wasiomwamini
Yesu alimheshimu Tomaso kwa kujibu mashaka yake, akionyesha kwamba hata wale wenye shaka wanaweza kuelekezwa katika imani.
3. Upo ushahidi wa ufufuo wa Yesu
Hadithi hii inathibitisha ufufuo wa Yesu na inasisitiza kuwa wokovu unapatikana kwa kuamini kuwa Yesu alikufa na kufufuka kwa ajili ya dhambi zetu (Warumi 10:9).

Fundisho kwa Wakristo wa leo
1. Wakristo wanapaswa kukumbuka kwamba imani inatakiwa iwe msingi wa maisha yao hata bila uthibitisho wa kimwili.
2. Wakristo pia wanapaswa kuwa na huruma kwa wale wenye shaka kama Yesu alivyokuwa kwa Tomaso.

Maana ya ujumbe wa Tomaso

Tomaso alipotambua uhalisia wa Yesu, alikiri waziwazi kwamba Yesu ni "Bwana" na "Mungu." Hii ni mojawapo ya tamko la wazi la uungu wa Yesu, katika Injili.

Imani ya Tomaso kwa ushuhuda wake katika ufufuko wa Kristo ni ushahidi wa kutosha kuwa Imani yetu tuliyo nayo hakika ni ya kweli kabisa na hakuna mashaka na kwa hiyo tuna kila sababu ya kujivunia imani yetu na kwamba hatujapotea bali tuko katika njia sahihi ya kumfikia muumba wetu. TUKIO LA TOMASO KUKATAA UFUFUKO WA KRISTO ULIKUWA NI MPANGO WA MUNGU KUTUTHIBITISHIA UKWELI WA UFUFUKO WA KRISTO KWETU KWA SISI WAUMINI WA LEO.

Yesu ni Rafiki Mwema (Yohana 15:13-14). Alikufa msalabani kwa ajili yetu wanadamu. Wakristo wanapaswa kukumbuka kwamba imani inatakiwa iwe msingi wa maisha yao hata bila uthibitisho wa kimwili.

Ushuhuda uko wazi. Tuwe na Imani na Yesu. Tusiwe na Imani kama ya Tomaso.
 
Back
Top Bottom