Tujiulize Pamoja! Ni Coincidence au MUNGU Ameongea?

Tujiulize Pamoja! Ni Coincidence au MUNGU Ameongea?

Upumbavu mwingine,hivi kwa akili zako wewe ndo mwenye wizara ufisadi unaweza kufanyika wizarani kwako bila wewe kujua? Na bado alikua anatetea bungeni.usicho kijua ni sawa na usiku wa giza
nchi za wenzetu kashifa kama hizo hata asinge nusa harufu ya ubunge tena sema walisha jua wengi wetu ni mazuzu kama wewe inakuwa ndo faida yao.
 
Upumbavu mwingine,hivi kwa akili zako wewe ndo mwenye wizara ufisadi unaweza kufanyika wizarani kwako bila wewe kujua? Na bado alikua anatetea bungeni.usicho kijua ni sawa na usiku wa giza
nchi za wenzetu kashifa kama hizo hata asinge nusa harufu ya ubunge tena sema walisha jua wengi wetu ni mazuzu kama wewe inakuwa ndo faida yao.
Msiowapenda wanazidi kuja. Mungu anazidi kuwaonyesha na ufedhuli wenu.
 
Amani ya Bwana iwe nanyi wadau,

Natumai wote mu wazima na mnaendelea vizuri sana. Ikiwa ni siku ya jumapili nikiwa namtafakari raisi wangu mpendwa ndugu John Pombe Magufuli kwa jinsi anavonikosha na utendaji wake uliotukua mara ghafla kuna jambo limenijia kichwani ghafla.

Jambo hili linamuhusu mtu mmoja ambaye hakuwa anafahamika na jamii ya watanzania ila alikuja kujizolea sifa kemkem pale alipoteuliwa kuwa waziri wa nishati na madini. Huyu si mwingine bali ni Prof Muhongo ambaye kwa miaka 2 tu aliyokaa pale nishati na madini tuliona utekelezaji wa kasi wa miradi ya usambazaji umeme vijijini kwa record ambayo nchi haikuwai kuwa nayo, pili tuliona utekelezaji na ukamilishwaji wa ujenzi wa bomba la gesi ambalo leo tumeanza kuona faida yake, tatu tuliona ubanwaji wa mirija ya ufisadi kwenye sekta ya madini na gesi kitu kilichowafanya watu wenye nia mbaya nae wamuundie zengwe na kumtengenezea chuki kwa watanzania hadi akajiuzuru.

Kichwa cha mada kinasema tujiulize kwa pamoja kuwa ni Coincidence au MUNGU ameongea na labda watu wanaweza jiuliza ninataka kusema nini hasa?

Kitu ninachotaka kukisema hapa ni kuwa kuna kitu kimetokea hasa juu ya kundi la watu waliokuwa wanaongoza kumsema Prof Muhongo vibaya, hili kundi lote limekutwa na mambo mazito sana ambayo sidhani kama watanzania wenzangu mmeyaona ila nataka tu kushare nanyi at least na nyie muone alafu tujiulize kwa pamoja kuwa Je ni Coincidence au MUNGU AMEONGEA KUWAJIBU WOTE WALIOKUWA WANAMTENGENEZEA PICHA MBAYA PROF MUHONGO KWA WATANZANIA?

Mimi nimeona list fupi ya watu ambao ngoja niiweke hapa,

1. Christopher Ole Sendeka.
Huyu aliweka chuki ya wazi na Prof Muhongo, huku akipewa airtime kubwa na ITV aliwekeza kumkaanga vibaya sana Prof Muhongo ila leo ubunge kaukosa. Je ni ?coincidence au adhabu toka kwa MUNGU?

2. Reginald Mengi.
Huyu najua kila mtu anajua ugomvi wake na Prof Muhongo na najua kwa ma smart analyist huyu alichangia kama asilimia 85 ya kuangushwa kwa Prof Muhongo kupitia media zake na marafiki zake wa kisiasa ila juzi tu kambi ya mgombea uraisi ambaye inasemwa alijitolea kumsupport imeanguka vibaya na sasa hajui la kufanya kwa sababu ambaye alikuwa hampendi na kumuunga mkono ndugu Magufuli ye ndo kawa raisi. Kwa haya yaliyompata ni coincidence au adhabu toka kwa MUNGU?


3. David Kafulila
Huyu ndo aliwekwa kama mastermind wa kumkaanda Muhongo bungeni ila kilichompata kwenye matokea ya ubunge tunajiuliza kuwa je ni coincidence au ndo adhabu ya MUNGU kwa yale aliyotenda dhidi ya Prof Muhongo???


4. Moses Machali
Huyu naye alihusika sana kumkaanga Prof Muhongo sijui kwa kujua au bila kujua ila yaliyomkuta kuangushwa kwenye ubunge tunajiuliza Je ni coincidence au ndo MUNGU kamjibu?

5. Hamis Kingwalala
Huyu naye alijitolea sana kumsema vibaya na kumkaanga Prof Muhongo, ila kwa kuangushwa na bashe na kuukosa ubunge sote tunajiuliza je ni coincidence au MUNGU ndo amemjibu?

6. Zitto Kabwe
Huyu naye alihusika sana kwa yaliyompata Prof Muhongo ila kwa Chama chake ambacho amekijenga kwa nguvu sana kupata mbunge mmoja tu kwenye uchaguzi huu tunajiuliza naye ni coincidence au MUNGU amemjibu kwa aliyomfanyia Prof Muhongo?

7. Felix Mkosamali
Huyu naye kama machali tu alimshupalia sana Prof Muhongo ila sasa amekosa hata ubunge wenyewe sasa tunajiuliza je ni coincidence au naye MUNGU amemjibu?

8. Deo Filikunjombe.
Huyu sitamzungumzia kwa sababu maadili ya dini yangu hayaniruhusu.

Sasa ndugu zangu kwa haya yote yaliyotokea naomba tujiulize kwa pamoja Je ni Coincidence au MUNGU AMEONGEA?

9. Lembeli
Huyu nae kama kawaida yake kusimama anaposimama mzee machache kulimponza kwa sababu nae alimshupalia Muhongo ila nae amekosa ubunge kabisa

10. James Mbatia
Huyu naye akitegemea cheap popularity alimshupalia sana Prof Muhongo na kilichompata ni kuwa chama anachokiongoza kama mwenyekiti kimepoteza viti katika ngome zake na kwa kifupi amebaki kama mbunge pekee wa chama chake bungeni kutoka kuwa na wabunge 4


MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATANZANIA.

cc. Pasco, Faiza Foxy, Gentamycine, Rweye, Elungata, Lizaboni, Kanone

Unaonekana umetumwa kafie mbele huko! Unuongelea Kigwangala yupi wewe? Sio yule mbunge wa sasa wa nzega vijijini? Muhongo huyu huyu aliyetaka kusoma matokeo ya F6 ya Ole Sendeka bungeni au mwingine? Huyo mzee unayempigia chapuo ana madoa makubwa tu.
 
Eti Bashe kamuangusha Kingwangala, redo your homework asee, hujui hata wabunge halafu unajifanya kufanya uchambuzi?
Ila nina kaswali kadogo: Hivi hata mtu akiiba ni Mungu kaongea kwa mujibu wa imani yako?
 
Kama braza msukuma akimpa hata unaibu waziri huyu jamaaa basi nitaamini Sisim ni ile ile ile
 
Unaonekana umetumwa kafie mbele huko! Unuongelea Kigwangala yupi wewe? Sio yule mbunge wa sasa wa nzega vijijini? Muhongo huyu huyu aliyetaka kusoma matokeo ya F6 ya Ole Sendeka bungeni au mwingine? Huyo mzee unayempigia chapuo ana madoa makubwa tu.
Ndugu Muhomgo anabebwa na uadilifu na utendaji wake uliotukuka not otherwise.
 
Eti Bashe kamuangusha Kingwangala, redo your homework asee, hujui hata wabunge halafu unajifanya kufanya uchambuzi?
Ila nina kaswali kadogo: Hivi hata mtu akiiba ni Mungu kaongea kwa mujibu wa imani yako?
Hujui kuwa Kikwangalala alimkimbia bashe nzega mjini na bila kuwepo nzega vijijini tungemsahau kabisa kwa sababu bashe alimuweka pabaya sana????
 
Mkuu una uhakika na ulichokiandika hapa kweli?

Hamisi Kigwangala kaukosa ubunge?

Zitto Kabwe naye kaukosa ubunge!??

Please, labda mimi ndiyo sijakuelewa lakini naamini nimekuelewa ila nahisi wewe "umefufuka toka kwa wafu" na kwa hiyo huna information za kutosha ya kinachoendelea hapa duniani ktk kipande cha Tanzania!!

nafikili hujamuelewa kuhusu hao watu uliowataja
 
Ulienda Vizuri Ila ulipofika kwa Kigwangala nikaona unaendeshwa kwa nguvu ya viroba.
 
Serikali ya CCM iliamua kuwashughulikia kikamilifu wale wote walio komalia kukwapuliwa kwa mabilioni ya ESCROW. Kwa kiasi fulani walifanikiwa japo walikumbana na nguvu ya umma kwenye majimbo ya akina Lissu, Mbowe, Mbatia nk.

Waliweka nguvu nyingi huko matokeo yake wakaisahau Zanzibar ikawa inawaponyoka, wanakuja kustuka imeondoka. Wakaona heri lawama kuliko fedheha, wameweka mpira kwapani😛eace::msela:
 
Kwani zile pesa za sandarusi na mabox zilienda wapi? muongo anajua nani kachukua?Swali la kujiuliza hapa ni kwa nini waxiri wa fedha na gavana wa bot mpaka leo HAWAJAWAJIBIKA
 
Back
Top Bottom