White party
JF-Expert Member
- May 5, 2015
- 1,021
- 1,151
Nilipata changamoto kubwa sana first born alipoanza shule,kila tukitunza ada na mwenzangu ilikua haitunziki hata tukipata ka tatizo kadogo tunachukua hapo hapo vichwa viliuma kwelikweli.
Tulijitahidi Hadi kuweka kwa watu lakini ka pepo ka si Kuna hela kwa fulani hakakutuacha salama,ikabidi nikae chini peke yangu kwanza ili nijue tunajikwamua vipi.
1.Wazo la kwanza kunijia ni je tunahitaji kuweka kiasi gani kila mwezi ili kufikia lengo la ada kwa mwaka?
2.Hii pesa inatunzwa wapi ili tusishawishike kuichukua?
Katika kujiuliza kwa watu wawili watatu ndo mmoja akanishauri,...nifungue akaunti ya mtoto na nisichukue kadi ya ATM ili nione aibu kwenda benki kila mara tena kwenye akaunti ya mtoto kupunguza aibu iliyoje!!!
Ndugu zangu imesaidia sana,Sasa Niko mwezi wa8 kamchezo kamenoga natunza huko Hadi pesa za mipango midogo ya baadae,pesa yoyote inayotokeza nje ya salary ht kama 20 inatupiwa huko yani Sasa navuta pumzi.
N.B :Kipato changu ni cha kawaida sana chini ya laki5 kwa mwezi naamini waTz wenzangu wengi tunaangukia hapa. Pia msinishauri kufanya biashara hiyo ilishashindikana kwangu.