Tujitahidi kutunza pesa,mimi nilianza hivi

White party

JF-Expert Member
May 5, 2015
1,019
1,149
Nilipata changamoto kubwa sana first born alipoanza shule,kila tukitunza ada na mwenzangu ilikua haitunziki hata tukipata ka tatizo kadogo tunachukua hapo hapo vichwa viliuma kwelikweli.

Tulijitahidi Hadi kuweka kwa watu lakini ka pepo ka si Kuna hela kwa fulani hakakutuacha salama,ikabidi nikae chini peke yangu kwanza ili nijue tunajikwamua vipi.

1.Wazo la kwanza kunijia ni je tunahitaji kuweka kiasi gani kila mwezi ili kufikia lengo la ada kwa mwaka?

2.Hii pesa inatunzwa wapi ili tusishawishike kuichukua?

Katika kujiuliza kwa watu wawili watatu ndo mmoja akanishauri,...nifungue akaunti ya mtoto na nisichukue kadi ya ATM ili nione aibu kwenda benki kila mara tena kwenye akaunti ya mtoto kupunguza aibu iliyoje!!!

Ndugu zangu imesaidia sana,Sasa Niko mwezi wa8 kamchezo kamenoga natunza huko Hadi pesa za mipango midogo ya baadae,pesa yoyote inayotokeza nje ya salary ht kama 20 inatupiwa huko yani Sasa navuta pumzi.

N.B :Kipato changu ni cha kawaida sana chini ya laki5 kwa mwezi naamini waTz wenzangu wengi tunaangukia hapa. Pia msinishauri kufanya biashara hiyo ilishashindikana kwangu.
 
Naomba nisitie neno hapa.ahahahah
Mtoto aliyelelewa ktk mazingira ya frustration ya maisha kama hizo frustrations ya mleta mada lazima naye ni frustrated tangu udogoni. Kwa hiyo siyo ajabu aka-opt hata kuwa mpiga debe stendi kinyume matarajio ya mzazi......hapo ndipo mzazi sukari/pressure hushuka na kupanda.
 
Dah..inasikitisha sana mkuu..nawengi wetu tunalea kwa frustration sanaa.
Unamshauri nn sasa huy mdau..maaa kwa frustration h izo halaf mtoto azingue kwel jamaa anaweza kudanja
 
Peleka mtoto shule unayoweza kuimudu na sio kuteseka mpk mnashindwa kula. All in all primary hutakiwi kuteseka sana, subiri elimu za juu huko. Mpeleke shule ya kawaida nzuri na unayomudu gharama zake

Mtoto asome vizuri huku chini aelewe,akiwa zezeta huku msingi huko juu atakuwa boya zaidi na zaidi.

Kama shule nzuri apelekwe sasa hivi akasome vozuri apanue ubongo wake aelewe mambo,huko mbele ndo ada kubwa zaidi na majukumu yanazidi na mtoto anazidi kujitambua hiyo itafanya awe na uchungu wa kujisomea hata kama yupo shule ya kata.
 
Tatizo watz tunafanya mambo kwa mkumbo na sio kwa kufikiri ay kufanya research. Shule za kawaida zina msingi mzuri tu sio lazima kujitesa kwa gharama kisa mtoto apande mabasi ya njano na kuongea kiingereza. Fanya pale unapopaweza kama unazo mpeleke shule kubwa na kama huna usiangaike na kujitesa tofauti ya elimu vs gharama ni ndogo sana
 
Nilipata changamoto kubwa sana first born alipoanza shule,kila tukitunza ada na mwenzangu ilikua haitunziki hata tukipata ka tatizo kadogo tunachukua hapo hapo vichwa viliuma kwelikweli.

Tulijitahidi Hadi kuweka kwa watu lakini ka pepo ka si Kuna hela kwa fulani hakakutuacha salama,ikabidi nikae chini peke yangu kwanza ili nijue tunajikwamua vipi.

1.Wazo la kwanza kunijia ni je tunahitaji kuweka kiasi gani kila mwezi ili kufikia lengo la ada kwa mwaka?

2.Hii pesa inatunzwa wapi ili tusishawishike kuichukua?

Katika kujiuliza kwa watu wawili watatu ndo mmoja akanishauri,...nifungue akaunti ya mtoto na nisichukue kadi ya ATM ili nione aibu kwenda benki kila mara tena kwenye akaunti ya mtoto kupunguza aibu iliyoje!!!

Ndugu zangu imesaidia sana,Sasa Niko mwezi wa8 kamchezo kamenoga natunza huko Hadi pesa za mipango midogo ya baadae,pesa yoyote inayotokeza nje ya salary ht kama 20 inatupiwa huko yani Sasa navuta pumzi.

N.B :Kipato changu ni cha kawaida sana chini ya laki5 kwa mwezi naamini waTz wenzangu wengi tunaangukia hapa. Pia msinishauri kufanya biashara hiyo ilishashindikana kwangu.
Hapo kwenye neno "Tusikushauri biashara ilishashindikana ndipo ulipoharibu" ..pesa invest...ukitunza tu na kutegemewa mshahara utaishia kwenye rat race....wallah nakwambia badilisha hio mentality yako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom