Tujisahihishe - Viongozi wa Serikali na Chama tawala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujisahihishe - Viongozi wa Serikali na Chama tawala

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hosida, Nov 17, 2011.

 1. H

  Hosida Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau,

  Kujisomea ni mojawapo ya juhudi binafsi za binadamu kujiongezea maarifa. Napenda kuwaasa viongozi wa serikali na chama tawala kujitahidi kukumbuka kuwa katika kumuenzi hayati baba wa Taifa ni pamoja na kufanya au kuyaendeleza yale mazuri aliyofanya. Lakini kubwa zaidi ni kujitahidi kusoma baadhi ya nyaraka/machapisho aliyoandika wakati wa uhai wake. Moja ya waraka muhimu ambao unaonesha msimamo wa Falsafa yake ya kutetea ukweli na haki ni chapisho alilolipa jina "TUJISAHIHISHE". Nawakaribisha wanajamvi ambao hamjafanikiwa kuupata waraka huo mjaribu kuutafuta una mawazo mazuri sana ambayo viongozi wetu wa sasa wanayapoozia huenda kwa kutokufahamu au kwa falsafa ya UNAFSI aliyoielezea hayati baba wa Taifa wakati ule. Katika kitabu hiki mwalimu alisema "...hoja zetu zikijibiwa kwa kupingwa halafu tukawakasirikia waliozipinga tunafanya mazungumzo yasiwe na maana, kwa sababu tunapenda hoja zetu zikubaliwe tu hata kama si hoja safi"

  A real critical thinker must be ready to be critisized.
   
Loading...