Tujipime kisha tuamue vema

Tujipime kisha tuamue vema

pambe samanini

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2015
Posts
464
Reaction score
271
Kwa muda sasa siasa za Afrika na waafrika zimekuwa sikifanana na kutofautiana toka taifa moja hadi jingine hasa muundo na mwenendo wa kisiasa katika nyakati hizi za vyama vingi
Afrika imekuwa na utitili wa vyama vya siasa na wanachama hoi kiuchumi na kiuweledi hali ambayo kwao kila wakati ni uchaguzi wa kula na kuchezea mali na raslimali za taifa kwa chaguzi nyingi zisizokuwa na tija kwa taifa na wananchi wao
Mfumo wa siasa unaoendeshwa Afrika unabebwa na dhana ya demokrasia na utawala bora ukiwa umeandikwa kwenye kioo wala hagusiki. Kwa hali ya uchumi na elimu wa waafrika walio wengi maneno haya hayana tija bali ni mitaji ya watu wachache walioko kwenye taasisi dhaifu ( vyama) kwani muda mwingi sana watu hutumia kujadili siasa na wanasiasa kuliko kufanya kazi zitaziambatana na siasa kuwaletea maendeleo huku kwenyewe ni kupoteza raslimali muda.
Ni aibu sana kwa wanasiasa kuhama vyama kila wakati huku wakijua ni kulitia taifa hasara kubwa hasa wanyonge wa nchi na walipa kodi wa taifa hili changa kiuchumi na bahati mbaya viongozi wetu wanafurahia kupata watu kwenye vya vyao bila kuhesabu hasara inayopatikana kwa taifa na wananchi, kwani wanyonge wa taifa hili waishio vijijini hawana maji, umeme, barabara mbovu, miundombinu ya kielimu shida, pamoja na umasikini uliokithiri nk huu ni ufisadi mkubwa sana unaoendeshwa na wanasiasa wa bara la Afrika.
Kama taasisi dhaifu ( vyama) havilioni hili halafu wao ndo wa kwanza kuwahadaa wananchi kuwa tunapigania hali za wanyonge wa mataifa yao huu ni usaliti mkubwa usio sameheka mbele ya mwenyazi Mungu, yanayosemwa majukwaani hayafanani ya bungeni pia maisha yao. Hutumia gharama mkubwa (jasho la wanyonge) kuwakusanya wanyonge na umaskini wao kuhudhuria mukutano yao na kununua magazeti ili kujua watetezi wao wanasemaje? Kipato kidogo, muda mwingi siasa na elimu ndogo vinawagharimu waafrika walio wengi
Hivi demokrasia na utawala bora ni nini kma siyo kuwapa haki stahiki watawaliwa? Kuhama vyama nako ni demokrasia na utawala bora? Kuwakusanya maskini na kuwaaminisha utajiri, nao ni utawala bora? Kuhudumu chaguzi ndogodogo nao ni utawala bora na demokrasia?
Kweli taasisi hizi (vyama) za kiafrika na watu wake ni dhaifu sana, siyo watu wema kwa watu wake na mataifa yao.
 
Rekebisha thread yako inaleta uvivu kusoma,mfano jaribu kuweka paragraph kadhaa.
 
Mkuu ungeipanga vyema ingependeza sana.
Ni aibu sana kwa wanasiasa kuhama vyama kila wakati huku wakijua ni kulitia taifa hasara kubwa hasa wanyonge wa nchi na walipa kodi wa taifa hili changa kiuchumi na bahati mbaya viongozi wetu wanafurahia kupata watu kwenye vya vyao bila kuhesabu hasara inayopatikana kwa taifa na wananchi, kwani wanyonge wa taifa hili waishio vijijini hawana maji, umeme, barabara mbovu, miundombinu ya kielimu shida, pamoja na umasikini uliokithiri nk huu ni ufisadi mkubwa sana unaoendeshwa na wanasiasa wa bara la Afrika.
 
Umesema vyema, hakuna kiongozi yeye mweusi mwenye dhamira ya kuwakomboa wanyonge, wanyonge ni daraja La kupandia ngazi kwa wajanja,uzungumza sana maendeleo kwa uchungu lkn vitendo vyao haviakisi maneno. Wakati mwingine naona Africa inapesa nyingi sana za kuchezea kuliko kwenye maendeleo, viongozi wote wanaamini Ukitaka kuwatawala watu wafanye kuwa masikini
 
Back
Top Bottom