Ipi dot com
JF-Expert Member
- Mar 28, 2011
- 306
- 166
Mwaka 1997 nilikuwa nafanya kibarua cha ujenzi ktk wilaya moja mkoani Mbeya
Wakati naendelea na kazi siku moja alikuja ndugu yangu ambae awali tulikuwa tukiishi wote ilala mtaa wa bungoni kabla sijaenda mbeya kwa ajili ya kibarua.
Baada ya kunisabahi alinieleza kuwa ana mpango wa kwenda south africa wakati huo ilikuwa kama fashen kwa vijana kwenda South
Kwa vile nilikuwa na fedha kidogo nikaona hii fursa ya kutoka na mimi haraka na mimi nikamshirikisha jamaa yangu john(nadhani yumo jumu JF)
Sikumbuki tarehe rasmi lakini ulikuwa mwezi desember haraka nikafanya maandalizi na jamaangu john nae alifanya maandalizi tukawa watatu tayari kuanza safari
Mala kaja jamaa yetu mwingine katoka dar tukawa wanne siku moja kabla ya safari jamaa mwingine kajiunga nasi tukawa watano
Mtihani wa kwanza ni kibali cha wazazi baba alikubali japo kwa shingo upande mama kagoma ilibidi nikamuone mjomba ambaye amesafiri sana Afrika ili amshawishi mama anikubalie lakini nilishaamua kusafiri hata wakigoma
Baada ya mama kuonana na mjomba akanikubalia hapo sasa tukapanga siku inayofuata tuanze safari rasmi.
Asubuhi tukaondoka kwenda tunduma safari kama masaa mawili tukafika pale na kuanza procces za uhamiaji nakumbuka mimi nilikuwa ma pass ya muda baada ya kukamilisha ilibidi tutafute chumba tulale maana kulikuwa na shida ya usafiri kwenda lusaka si kama sasa
Wakati tunasubiri kesho ifike huyu jamaa alieongezeka ambaye wa tano katika kuzunguka tunduma akakutana na jamaa yake ambae alikuwa mwenyeji pale tunduma ghafra jamaa kabadili mawazo hataki tena kusafiri tukaona poa katupunguzia mzigo.
Asubuhi ilipofika ndugu yangu alienishawishi kwenda SA kaanza kusuasua na yeye tulikua tukimtegemea maana aliwahi kwenda kabla,na tulijua angekuwa mwenyeji wetu.
Hapo bado masaa machache tuanze safari likawa pigo kwetu tumebaki watatu.
Wakati huo mabasi yalikua yanaanza safari jioni yakiwa yamebaki masaa mawili jamaa wa tatu akajitoa tukabaki wawili mimi na jamaangu John.
Tukaona poa tuu ngoja tukapambane wanaume tukachanganya hela zetu tukachenji tupate kwacha,kisha tukaenda kukata tiket tayari kwa safari.
Hapo ugumu wa safari unaanza ni kaanza kujuta nimeanzaje mimi.
Itaendelelea...