Tujikumbushe tungo za Dr. Remmy Ongala- Open post | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujikumbushe tungo za Dr. Remmy Ongala- Open post

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Kizimkazimkuu, Jan 5, 2011.

 1. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Mi nazikumbuka hizi

  Mariam

  Nakonda kama mnazi kwa mapenzi niliyonayo,
  Jina lako nakuota mchana kutwa sili ee
  Moyo wanichechemea, mwili damu kauka eee

  ...na hiki kipande, katika Mola nalilia mtoto

  Nakulilia mola wangu eee
  Nakuwaza mola wangu eee eh
  Yaliyonikuta ni makubwa naona haya
  Mbona nateseka,

  Wenzangu wana watoto mimi sina hata wa dawa eee
  Yailah mtoto si nguo ningenunua
  Mtoto ni mtoto kwa mama hakui iiih
  hata angelikua ni kilema au mbaya kama remmy, n mtoto tu uuuh

  Karibuni mnaozikumbuka tungo za nguli huyu aliyetutoka 2010.....
   
 2. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  MUZIKI ASILI YAKE WAPI

  Muziki asili yake wapi eeee
  Muziki ni wa nani eee

  Muziki hauna mwenyewe,
  Muziki ni wito,
  Muziki ni fundisho,
  Muziki ni maombolezo, kilioooooo
  Usinione nikiimba ukadhani ninayo furaha
  Kumbe ninayo huzuni moyoniiiiiiii

  WIMBO NISEME NINI
  Niseme nini?
  Niseme nini?

  Sina la kusemaaaaa

  ......
  ....
  Wengi hutishika na sura yangu mbaya lakini roho yangu ni nyeupe,
  Nitahakikisha sifanyi mabaya hapa ulimwenguni,
  ili siku ya mwisho nionane na Muumba

  SIKU YA KIFO

  Wandugu wapenzi,
  Hii nyimbo ni nyimbo ya ukumbusho,
  wa siku ya kuzaliwa na siku ya kufa,
  Ulikuja kwa udongo utarudi kwa udongo,

  Mawazo mawazo ya mtu mziiiiiima,
  Kama akikwambia neno usibishe,
  Neno ya muzee, ukabisha,
  mwisho utapata shida.....

  NAPENDA pia KAROLA, MREMA, NARUDI NYUMBANI, SAUTI YA MNYONGE, HARUSI YA MWANZA
   
 3. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  SIKU YA KUFA by DR. REMMY  MUZIKI ASILI YAKE WAPI  KIFO HAKINA HURUMA

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Binafsi naukumbuka wimbo wa MABMO KWA SOKSI. Wakti wimbo huu unaimba mie nlikuwa primary. Nakumbuka jinsi wimbo huu ulivyopigwa marufuku na serikali kisa eti ulikiuka maadili ya mtanzania. Kiukweli remmy alikuwa akiwaasa watanzania waache kufanya ngono bila kondom.
  Kila nikisika matangazo yanayohusu kondom mie naukumbuka huu wimbo, nafikiria jinsi serikari yetu isivyoweza kufanya mambo yake hadi itakiwe na wahisani. remmy alikuwa ni mtanzania wa kwanza kushtukia ishu ya ukimwi na hivyo kuwaasa vijana wavae kondom, mwenyee remmy aliziita soksi. Na kweli vijana tulihasika, tulikuwa na kauli mbiu ya MAMBO KWA SOKSI. Kama remmy angeungwa mkono na serikali basi vijana wengi wasingeteketea na ukimwi. Tunakumbuka shuka wakati kumeshakucha!!!!
  Hebu usikilize wimbo wenyewe.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 645
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  [I want To Go Home - Matimila(Dr. Remmy Ongala)]

  [Remmy]
  Narudi nyumbani yooo
  Narudi nyumbani
  Eeeee nyumbani.....
  Nilipoamua nirudi nyumbani
  Nyumbani ni nyumbani hata kukiwa kubaya au kuzuri
  Nyumbani kwako ni nyumbani eee...nyumbani

  Narudi Songea ooo
  Narudi Matimila
  Narudi Narimo
  Ooooooo narudi nyumbani
  Narudi Pilamio ooooo eee
  Narudi Ungonini
  Wangani wote mjiunge walongo vangu(Kikabila sikipati vizuri hapa)

  Eeee nyumbani.....

  [Wote]
  I want to go home
  I need to go back ho
  I need to go back home
  The place that is our home
  Good or bad still home
  (repeat x 3)

  [Remmy tena]
  Narudi nyumbani yooo
  Narudi nyumbani
  Eeeee narudi Majimaji
  Narudi Afrika eee( x 2)
  Narudi Nigeria
  Eee narudi Ghana
  Yooho narudi Kenya eee
  Yoo narudi Uganda
  Eeee narudi Gabon
  Yooho narudi Congo
  Eeee narudi Zaire eee
  Yooho narudi Burundi
  Narudi Rwanda
  Narudi Majimaji
  Nakwenda kula likono na la nyungu
  Eee narudi Zambia
  Narudi Zimbabwe
  Narudi Botswana
  Narudi Afrika ya Kusini
  Mandela narudi nyumbani eee
  Mwinyi weee narudi Tanzania
  Eee narudi Tz ooo
  Maricela ooo narudi nyumbani
  Maricela ooo narudi nyumbani ooo
  Murema narudi nyumbani
  Baba Murema narudi nyumbani
  Kawawa narudi nyumbani.........Salamwela eee
  Kamwenye ee narudi nyumbani
  Nyerere narudi nyumbani oooo x2
  (kinaendele kiloingala hapa sikipati)

  [Wote]
  I want to go home
  I need to go back home
  I need to go back home
  The place that is our home
  Good or bad still home
  (repeat x 3) .........
   
 7. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 645
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  [NALILIA MTOTO - Matimila]

  Nakulilia Mola wangu weee,
  Nakuwaza Mola wangu wee,
  Yalonipata makubwa naona balaa,
  Wala hamu sina x2

  Wenzangu wana watoto,
  Mimi sina hata wa dawa eeeh,
  Niwatumapo wana wa wenzangu,
  Mama zao hunisimanga x2

  Nalia nasikitika bahati sina,
  Kwa waganga wa kila namna nimefika ni bure tuuuu,
  Hospitali za kila namna nimekenda ni bure tuuuu,
  Mola nimemuomba na sadaka nimetoa ni bure tuuuu,

  Mola, Mola, Molaaa eeeh,
  Mola eeeh nataka mtoto,

  Mola Mola, Molaa eeh,
  Mola eeh, nalilia mtoto

  Mtoto angelikuwa ni nguo ningenunua,
  Mtoto ni mtoto kwa mama hakui,
  Hata angelikuwa kilema au mbaya kama Remmy ni mtoto tu!

  Mola Mola, Mola eeeh....
   
 8. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 645
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  [Mariamu - Matimila]
  (Remmy)
  ataka yote akosa yote
  apita ahangaika asijue la kufanya ... asijue la kufanya
  mshika mawili yote yamponyoka
  apita akebakeba asijiue la kujitetea
  mmmhhh mapenzi yawaka moto
  naitika nilikukosea sasa nihurumie
  si ninafikiri zaidi kuliko wewe
  nakonda kama mnazi kwa mapenzi nilionayo
  nilalapo nakuota mchana kutwa sili
  moyo wanichechemea mwili damu hukauka
  penzii eh ..... mmmh penzi eh x 2

  nasumbuka kwako unionavyo moyo wangu
  wewe ndio dawa yangu
  Maraimu wangu
  Tanga mbali
  waja leo wondoka leoo
  waja leo warudi leo

  Mariamu bibi
  mwenzenu sina pumuzi kujizuwia siwezi ohhh
  mwanaume barabara kazi ya mume kwa mke
  neno ya mke chumvi kwa mumewe
  neno ya muke kachumbari kwa mumewe
  penzi oh penzi likamung'uma he heh heh

  likamung'uma hen heh heh .... mmhhhh
  mdundiko, mdundiko ........ waaaaaa
  mdundiko ...... waaaa
   
 9. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 645
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  [MWANAIDI - Matimila]

  (Kibao MWANAIDI kilipigwa na wana Matimila enzi hizo.
  Sauti ni za Skassy Kasambula, Kyanga Songa, Fan fan na solo
  ni la Batii Osenga bila kumsahau Mbwana Cox katika rythim)

  nimetokea kumpenda binti Mwanaidi
  nimeridhishwa na tabia yake
  nikaamua tufunge nae pingu za maisha
  urithi ulioacha baba niliutumia
  ili kuneemesha ukoo wake
  nilianza kuuza mifugo
  hatimaye shamba
  ili kumtosholeza mahitaji yake ehhh

  baada ya miezi michache nikapata barua kutoka kwa Mwanaidi
  ..... .. kuwa yeye hanitaki tena
  tena hawezi kuolewa na mimi

  (wote)
  mimi najuta eh najuta mama
  gharama nilizogharamia
  ameona bure
  sijui la kufanya .. nasikitika oh
  sababu yako ....... Mwanaidi x 3
   
 10. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 645
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  [Mwanza - Matimila]

  Mwanza oooh Mwanza eeeh,
  Mwanza mji mzuri eeh,
  Mwanza nitarudi Mwanza,
  Mwanza nitakuja tena! x2

  Mji wa Mwanza umezungukwa na milima ya mawe,
  Milima ya alimasi,
  Milima ya dhahabu,


  Mji wa Mwanza umezungukwa na Lake Victoria,
  Lenye maji bariiiidi,
  Na samaki watamu wazuri,
  Mwanza ooh,

  Nalia Mwanza,
  Wakazi wa Mwanza ni Wasukuma ooh,
  Kabila Wasukuma,
  Sukuma waaa!
  Sukuma waaa!


  Kutoka Mwanza tulielekea Bukoba,
  Bukoba tulipokewa vizuri eeh,
  Matoke kwa wingi,

  Wakazi wa Bukoba wanasema Kihaya,
  Mwabonaki waitu,
  Mmmmh waitu eeeh


  Mwanza oooh Mwanza eeeh

   
 11. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  KAKURUVI thanks a lot ....U have made my day. Hizi nyimbo za huyu jamaa zilikuwa na maneno na ujumbe mtamu uliowasilishwa kwa lugha nyepesi sana na ya kila siku.....asante kwa kuchangia!
   
 12. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Nawashukuru wote (nimewaachia thanks kwenye posts zenu)..baba Mtu, 3D na Kakuruvi kwa kuchangia. Tumepoteza msanii mahiri ambaye aliipenda Tanzania na watanzania wengi , hasa walahahoi walimpenda!
   
 13. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Nafikiri hawa walikuwa ni orchestra Toma toma
   
 14. Mtumpole

  Mtumpole JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,444
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  SAUTI YA MNYONGE

  Mama yeh yeh yeh yeeeh
  Mama ninalia weh
  Mama uko wapi
  Mama nateseka eh
  Mama umejificha wapi
  Mama yoh yoh yoh yoh yoh yohoooo...
  Mama mi nalia ohooo
  Mama mi nalia eheee
  Mama mi nalia
  Ninalia ohooo
  Mama uko wapi
  Mama weh
  Mama uko wapi ohoo
  Remmy analia eheee
  Mama uko wapi ohoo
  Uko wapi ohoo

  Mimi mtoto yatima
  Sina baba wala mama
  Sina dada wala kaka
  Sina ndugu mwenzenu
  Sina ndugu mwenzenu ehee
  Nikaombe kwa nani ihiii
  Niende wapi

  Najutia ulimwengu
  Nimekosa nini mola
  Unyimwa ndugu
  Nikazaliwa peke yangu
  Mwenzenu sina baba wala mama
  Sina shangazi wala mjomba
  Sina babu wala bibi
  Niende wapi ohoo
  Niende wapi eheee
  Jamani niende wapi

  Masomoni nimefukuzwa
  Nalikuwa sina sare
  Nalikuwa sina viatu
  Nalikuwa sina madaftari
  Nimekwenda eh kwa mwalimu mkuu
  Mwalimu nihurumie ehee mwalimu
  Baba yangu ni kiwete eheee
  Mama yangu ni kipofu mwalimu
  Madaftari nani ataninunulia mwalimu ehee
  Unapinga kunisikiliza oh mwalimu
  Amenifukuza kiroho mbaya
  Shauri ya unyonge eh
  Sababu ya unyonge
  Sababu ya unyonge ehee
  Niende wapi ohoo

  Nimekwenda kuomba kazi nikaambiwa sina kisomo
  Nimeuza machungwa nipate kula nikaambiwa sina kibali
  Nimeuza big g nikaambiwa mimi mzururaji
  Nimeuza sigara nikaambiwa mimi mlanguzi jamani
  Sijui nile wapi ohooo
  Jamani nile wapi eheee
  Nikaombe kwa nani

  Kijijini nimefika nikaambiwa mimi ni mwizi
  Ngedere kala mahindi nikaambiwa ni mimi
  Nguruwe kala mihogo nikasingiziwa ni mimi
  Jirani akiibiwa naambiwa ni mimi jamani
  Sijui niishi wapi ohooo
  Jamani niishi wapi eheee
  Uko kijijini nakoishi hakuna bia
  Uko kijijjini nakolima hakuna stoo ya soda
  Sasa uniambie ninywe nini ehee
  Jamani naomba kinywaji ninywe gongo
  Gongo pombe ya wanyonge ehe
  Gongo pombe ya wakulima
  Nikinywa gongo nalima kama punda
  Nikinywa gongo nalima kama farasi
  Hiyo nyanya unanunua kariakoo unajua inatoka wapi
  Kwa sisi walevi wa gongo uko kijijini
  Sisi ndio tunanguvu ya kulima
  Jamani nasikitika ehee
  Niende wapi ohooo
  Jamani niende wapi ohooo
  Mimi sikusoma
  Hata ulaya wazungu wengine hawakusoma
  Sisi wote tukisoma
  Nani atamsomesha mwenzie
  Jamani nanyanyaswa ohoo
  Niende wapi ehee
  Jamani niende wapi ohoo
  Sikupendelea nizaliwe kilema
  Sikutaka kabisa nizaliwe kipofu
  Nikiomba msininyime ehee
  Nikipita msinicheke ehee
  Mimi mtoto yatima
  Pia ni mukulima
  Nyumba nalijenga ya makuti
  Nalalia ngozi la mbuzi
  Chini kuna viroboto ohooo
  Pia kuna kunguni ihiii
  Jamani sina umeme ehee
  Naishi kwa kibatari
  Sina chandaruha
  Hata kidonge ya klorokwini nyumbani kwangu sina
  Naishi kimungu mungu
  Naogopa ukimwi
  Niende wapi ohooo
  Wenye nguvu mnawajua vizuri
  Matembezi yao ni kwa gari
  Starehe zao kilimanjaro
  Ukienda kilimanjaro sasa hivi utawakuta
  Wake zao wamepaka lipstiki wazuri kama malaika
  Watoto zao wote wanasoma ulaya
  Niambie mimi mkulima jamani
  Mwanangu shuleni amefukuzwa
  Mke wangu anavyaa midabwada
  Mimi mwenyewe sina pesa jamani
  Niende wapi ohooo
  Jamani niende wapi eheee
  Nikaombe kwa nani
  Mama yoh yoh yoh yoh
  Mama ninalia weh
  Mama uko wapi
  Mama nateseka ohooo....

  Mama yeh yeh yeh yeeeh
  Baba ninalia weh
  Baba uko wapi
  Baba nateseka eh
  Baba umejificha wapi
  Mama yoh yoh yoh yoh yoh yohoooo...
  Mama mi nalia eheee
  Remmy analia ohooo
  Masikini remmy analia ohooo remmy weh
  Remmy ni mnyonge ehe
   
 15. allobaby95

  allobaby95 Senior Member

  #15
  Jun 5, 2017
  Joined: Feb 20, 2017
  Messages: 139
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
   
 16. allobaby95

  allobaby95 Senior Member

  #16
  Jun 5, 2017
  Joined: Feb 20, 2017
  Messages: 139
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
   
 17. shatisuruali

  shatisuruali JF-Expert Member

  #17
  Jun 5, 2017
  Joined: Jul 28, 2016
  Messages: 416
  Likes Received: 787
  Trophy Points: 180
  Weema wema k...
   
 18. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #18
  Jun 5, 2017
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,867
  Trophy Points: 280
  Wema, wema kumanyoko
   
 19. kifinga

  kifinga JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2017
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 1,710
  Likes Received: 1,619
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa nikiwa mdogo nilikua najua ni mngoni kumbe ni mtu wa Congo ila aliipenda sana nchi ya tanzania
   
 20. gwa myetu

  gwa myetu JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2017
  Joined: Aug 18, 2014
  Messages: 4,202
  Likes Received: 4,060
  Trophy Points: 280
  Hivi aliimba hivi kweli au watu wameedit?
   
Loading...