Tujikumbushe tungo za Dr. Remmy Ongala- Open post

Mi nazikumbuka hizi

Mariam

Nakonda kama mnazi kwa mapenzi niliyonayo,
Jina lako nakuota mchana kutwa sili ee
Moyo wanichechemea, mwili damu kauka eee

...na hiki kipande, katika Mola nalilia mtoto

Nakulilia mola wangu eee
Nakuwaza mola wangu eee eh
Yaliyonikuta ni makubwa naona haya
Mbona nateseka,

Wenzangu wana watoto mimi sina hata wa dawa eee
Yailah mtoto si nguo ningenunua
Mtoto ni mtoto kwa mama hakui iiih
hata angelikua ni kilema au mbaya kama remmy, n mtoto tu uuuh

Karibuni mnaozikumbuka tungo za nguli huyu aliyetutoka 2010.....
Mkuu hiyo ya kwanza naikumbuka lakini haitwi Mariam, wimbo unaitwa mtaka yote kama sikosei, ni tungo matata sana na haichoshi kusikiliza,


Sent using Jamii Forums mobile app
 
MUZIKI ASILI YAKE WAPI

Muziki asili yake wapi eeee
Muziki ni wa nani eee

Muziki hauna mwenyewe,
Muziki ni wito,
Muziki ni fundisho,
Muziki ni maombolezo, kilioooooo
Usinione nikiimba ukadhani ninayo furaha
Kumbe ninayo huzuni moyoniiiiiiii

WIMBO NISEME NINI
Niseme nini?
Niseme nini?

Sina la kusemaaaaa

......
....
Wengi hutishika na sura yangu mbaya lakini roho yangu ni nyeupe,
Nitahakikisha sifanyi mabaya hapa ulimwenguni,
ili siku ya mwisho nionane na Muumba

SIKU YA KIFO

Wandugu wapenzi,
Hii nyimbo ni nyimbo ya ukumbusho,
wa siku ya kuzaliwa na siku ya kufa,
Ulikuja kwa udongo utarudi kwa udongo,

Mawazo mawazo ya mtu mziiiiiima,
Kama akikwambia neno usibishe,
Neno ya muzee, ukabisha,
mwisho utapata shida.....

NAPENDA pia KAROLA, MREMA, NARUDI NYUMBANI, SAUTI YA MNYONGE, HARUSI YA MWANZA
Remmy ongala dakrar wa muzick mungu ailaze roho yake mahala pela
 
Back
Top Bottom