Tujikumbushe sheria; abiria ni nani?

Philipo D. Ruzige

JF-Expert Member
Sep 25, 2015
9,428
27,070
*Tujikumbushe Sheria*
Khalid Shekoloa: ( ROAD SAFETY AMBASSADORS- TANGA )

*ABIRIA NI NANI?*
ABIRIA ni mtu yeyote anayesafiri kwenye chombo cha usafiri na inahusisha mtu yeyote mwenye tiketi halali tangu muda wa kuripoti kituoni kwaajili ya safari.

Rejea kanuni ya 3 ya kanuni za Usafirishaji Abiria, GN. 218/2007.

Kwa mujibu wa kifungu cha 39(4(a)) cha Sheria ya Usalama Barabarani (Road Traffic Act Cap, 168) mtoto ambaye kwa kumuangalia tu yupo chini ya miaka mitatu(3) na ambaye hakai kwenye kiti hatahesabika kuwa ni abiria.

Aidha kwa mujibu wa kifungu cha 39(4)(b) watoto wawili, ambapo kila mmoja yupo juu ya umri wa miaka mitatu (3) na si zaidi ya miaka kumi na miwili (12), watahesabika kuwa ni abiria mmoja.

Hivyo mtu anapoambiwa amezidisha abiria kwenye gari ni lazima afisa husika azingatie matakwa ya kisheria ya kifungu cha 39(4)(a) na (b).

*USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE*

Credits to: Khalid Shekoloa: ( ROAD SAFETY AMBASSADORS- TANGA)
 
Mtoto anaezidi miaka mi3,kama ni mmoja na aidha anayo seat au kapakatwa...
Je? sheria inamtambuaje!?
 
Back
Top Bottom