Tujikumbushe namna mahakama zetu zinavyoingiliwa na watawala kisa wapinzani

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
Kwa mujibu wa kitabu cha Jaji Barnabas A. Samatta kiitwacho “Uhuru wa mahakama” anasema, chombo cha utoaji haki yaani mahakama kinapaswa kuwa huru na kifanye kazi yake kwa misingi ya uadilifu inayo zingatia sheria. Kitabu hiki ni kizuri sana, kimesema mengi, mwandishi amewahi kuwa Jaji mkuu tangu mwaka 2000 mpaka 2007, mwaka 1984-1987 alikuwa Jaji wa mahakama kuu ya nchini Zimbabwe. Ameandika mengi kuhusu uhuru wa mahakama, nimechomekea hilo ili kuweka msingi tu.

Turudi kwenye hoja ya msingi, hivi karibuni mbunge wa Arusha mjini ndugu Godbless Jonathan Lema alikamatwa na kukaa ndani kwa takribani miezi 4. Suala la dhamana yake lilishikiliwa mahakamani kupitia ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka yaani DPP. Huyu Lema ni mbunge, ni mwana siasa ni mtu maarufu wengi wanamfahamu. Sasa jiulize, kuna watu wangapi wanao fanyiwa kama Lema na hawana sauti?? Ndiyo maana Lema alisema ataandika waraka kwa Rais, mantiki ya waraka wake ina anzia hapo.

Dhamana ya Lema iliamuliwa na “majaji watatu” (Kipenka, Luanda, Mugasha) nao walionyesha masikitiko yao dhidi ya maamuzi ya awali ya mahakama kushikilia dhamana ya Lema kupitia ofisi ya DPP. Majaji hawa wanatupa tafsiri ya haraka kwamba “uhuru wa mahakama una chezewa” mara kwa mara ila ni kujua nani ananyimwa haki, wapi na lini ni suala la muda tu na pengine mpaka awe angalau mwenye hadhi, cheo au jina kama la “Lema” tunaweza kufahamu haraka.

Uhuru wa mahakama haukuanza kupigiwa kelele leo wala jana. Kwa mujibu wa gazeti la MwanaHalisi Online, mwaka 1995 jaji mmoja aliwahi kutumiwa na serikali kutoa amri ya kuzuia mikutano yote ya siasa. Lengo ilikuwa ni kudhibiti mkutano wa mwana siasa “machachari” wa miaka hiyo ndugu Augustine Mrema aliyekuwa chama cha NCCR-MAGEUZI baada ya kujiondoa CCM. Watu walipo hoji uamuzi ule, waliambiwa Jaji anaweza kuamua popote kwa hiyo hakuna kifungu wala sheria inayo mtaka Jaji kuamua akiwa mahakamani tu.

Mwaka 2008, chama cha waalimu nchini (CWT) kilitangaza mgogoro na serikali na baadae kutishia mgomo nchi nzima. Mahakama ilitoa uamuzi usiku wa kuharamisha ule mgomo. Pia watu walisema chini chini lakini Jaji Robert Kisanga alisema "HAPANA" wazi, alipinga uamuzi ule kutolewa katika namna inayo tia shaka.

Mwezi Novemba mwaka 2011, Godbless Lema (Mbunge wa Arusha mjini) alinyimwa dhamana. Katika kipindi hicho majaji walisema, dhamana ni haki ya mshtakiwa au mtuhumiwa lakini mahakama ina uwezo na mamlaka ya kuzuia hiyo dhamana. Watu walihoji na baadae kukaa kimya suala hilo likaishia hivyo.

Mfano mwingine ni kesi ya aliye kuwa mgombea ubunge jimbo la Kigoma kusini (NCCR-MAGEUZI) ndugu David Kafulila. Alifungua kesi ya uchaguzi namba 2 ya mwaka 2015 dhidi ya Husna Mwilima (mbunge), msimamizi wa uchaguzi (mkurugenzi Halmashauri ya Uvinza) na Mwanasheria mkuu wa serikali katika mahakama kuu kanda ya Tabora.
Kafulila aliiomba mahakama katika kesi hiyo, itumie majumuisho ya kura kupitia fomu 382 zilizo sainiwa na wasimamizi na mawakala wote ili kuthibitisha kuwa alipata kura zaidi ya 34,000 dhidi ya 32,000 za mpinzani wake ndugu Husna Mwilima.

Kesi ya msingi ilihusu nani aliyepata kura nyingi, kwa hiyo tume ikaleta fomu mahakamani na zikawasilishwa mbele ya Jaji Ferdinand Wambali lakini alikataa zisihesabiwe kujua nani mshindi. Baadae Jaji Ferdinand Wambali akapandishwa cheo kuwa Jaji Kiongozi Mahakama Kuu Tanzania.

Ipo mifano mingi sana, katika mifano hii utaona kuna mazoea yame jengeka. Hapa nimetoa mifano ya zamani kidogo na mifano ya hivi karibuni kuonyesha kuwa kelele za uhuru wa mahakama hazikuanza juzi, jana wala leo. Unaweza kujiuliza mahakama zetu ziko huru kiasi gani ikiwa kuna “hisia na harufu” za kutotenda haki?? Yamkini kuna watu ambao wapo katika muhimili huu lakini hawakustahili kuwepo. Doa au kashfa yoyote juu ya mahakama siyo jambo dogo, mara nyingi bunge limekuwa likitaka kujadili mambo ya msingi lakini serikali ina ingilia kwa kusema “uhuru wa mahakama” ulindwe.

Duniani pote, kila muhimili yaani bunge, mahakama na serikali, hufanya kazi kwa wivu mkubwa. Lengo la wivu huo ni kufanya kila muhimili uwe na heshima yake. Ni aibu muhimili mmoja kuingiliwa kiutendaji, ni dharau na fedheha kubwa, ni dalili ya udhaifu na kushindwa kujimudu.

Muhimili wa bunge na Mahakama, wakikaa vizuri na kusimamia mamlaka zao, serikali itakaa vizuri kwa heshima ikijua kuwa haina "mtetezi wa kutumiwa". Tazama bunge halina meno, uchama na ukada umetawala, Muhimili pekee ulio baki yaani mahakama nao una nyooshewa vidole......... Ina sikitisha, ina shangaza na ina tia shaka ya upataji haki.
Je, pale mtu anapo nyimwa dhamana katika mazingira yenye hisia za kukomolewa, nini kifanyike?? Bado najiuliza ni wangapi wana fanyiwa kama Godbless Lema na hawana sauti?? Je, nani anawasaidia watu hao?? Wasio na uwezo wa kuweka hata wakili, nani anawasaidia?? UHURU WA MAHAKAMA BADO NI KITENDAWILI KIGUMU.

TUTAFAKARI PAMOJA:
Mbunge na kiongozi wa chama cha ACT-WAZALENDO ndugu Zitto Kabwe amehoji katika muktadha huo kuwa ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka iwajibike. Ikiwa majaji watatu wamegundua kuwa kulikuwa na mbinu za makusudi ili Lema aendelee kusota pale gerezani Kisongo, kwanini wahusika wote nao wasiwajibike??

Je, waachwe ili tuendelee kuzoea hali hii?? Ikiwa hakuna atakaye wajibika, tufikiri kwamba mambo haya ni kwa ajili ya wapinzani pekee??

Ikiwa kulikuwa na nia au dhamira ya kumkomoa Lema, kwanini asingepewa dhamana mapema kisha wapambane naye kwenye kesi ya msingi?? Nini ukomo wa mamlaka ya kisheria ya DPP kuhusu dhamana ya mshtakiwa au mtuhumiwa??
 
Eden hilo sasa lipo wazi saana kuwa Mahakama haiko huru. Kama ulivyotoa ule mfano wa Jaji Wambali kupanda cheo baada ya kubana haki, si muda mrefu kuanzia sasa, utasikia huyo hakimu mtu wa Ifakara, aitwaye Mteite, anapanda cheo kama shukurani kwa kusaidia ccm , na kumfunga mpinzani Sugu wa Mbeya. Viongozi wa Tanzania wanadhani wanazima upinzani, lakini kwa hakika ndiyo wanachochea moto wa mabadiliko. Leo kila unapopita watu wa rika zote wanazungumzia uminywaji wa HAKI unaosimamiwa na Mahakama. Mtu wa kawaida anajiuliza hivi sasa akimbilie wapi ? Nani mtetezi wa wanyonge leo hapa Tanzania. Yaani naiona shida kuuubwa mbele yetu. Usiniulize sasa tufanye nini.. Mimi, I just do not know what to do!!!!
 
Eden hilo sasa lipo wazi saana kuwa Mahakama haiko huru. Kama ulivyotoa ule mfano wa Jaji Wambali kupanda cheo baada ya kubana haki, si muda mrefu kuanzia sasa, utasikia huyo hakimu mtu wa Ifakara, aitwaye Mteite, anapanda cheo kama shukurani kwa kusaidia ccm , na kumfunga mpinzani Sugu wa Mbeya. Viongozi wa Tanzania wanadhani wanazima upinzani, lakini kwa hakika ndiyo wanachochea moto wa mabadiliko. Leo kila unapopita watu wa rika zote wanazungumzia uminywaji wa HAKI unaosimamiwa na Mahakama. Mtu wa kawaida anajiuliza hivi sasa akimbilie wapi ? Nani mtetezi wa wanyonge leo hapa Tanzania. Yaani naiona shida kuuubwa mbele yetu. Usiniulize sasa tufanye nini.. Mimi, I just do not know what to do!!!!
Kwa kweli taifa linapoelekea ni kubaya sana
 
Kinachowakuta mbowe na wenzake ni maelekezo kutoka juu hapo mahakama haina nguvu yoyote anaeendesha kesi ameshapewa maelezo yote kutoka juu
 
Back
Top Bottom