Tujikumbushe Maproducer wakali wa zamani

Roy alikuwa mtundu sana.

Nakumbuka 1999 Raha Towers tumeenda kwenye internet cafe ya Raha.com pale, basi kachukua computer kaifanyia utundu niliokuwa siujui siku hizo, akaibadilisha keyboard ya computer kiwa jeyboard ya kupigia muziki.

Salute.

Kama nakumbuka hii stori.
 

Kupotea kwa huyu jamaa, katika game kuliniumiza sana, kwanza ilikua ni ghafla na ndio ilikua hazina ya ECT. Alimmudu GK vizuri. Na nadhani kati ya maproducer wazuri mbali na Master Jay, walioweza kummudu GK ni yeye.
 
Roy alikuwa mtundu sana.

Nakumbuka 1999 Raha Towers tumeenda kwenye internet cafe ya Raha.com pale, basi kachukua computer kaifanyia utundu niliokuwa siujui siku hizo, akaibadilisha keyboard ya computer kiwa jeyboard ya kupigia muziki.

Salute.
Kumbe Kiranga na viranga vyako bado mtoto mdogo hivyo? Ma comments yako yalinifanya nikufikirie wewe ni mbabu aliye stow away in the 70s kabla hata Kishtobe haijaanza ku dock pale Dar port ( jokingly)
One love no offense intended ;-) ;-) ;-)
 
Hivi Producer Q yuko wapi? dunga wa mandugu digital pia hasikiki sasa hivi
Q niliskia alienda bongo record......dunga yuko kwao Kenya si unajua bongo majungu mengi ilibidi jamaa asepe
 
Kuna kichwa kama Ambha wa iringa, D money wa Downtown records
 
Kama kweli unathamini na kutoa shukurani,nafikri si busara kuwa kimbilia waakina p funk na kuwasahau bon luv na enrico,
 
Mkuu imekuaje Bizman hajatajwa kwenye list yako pamoja na kuwakumbuka wengi
 
Jamaa Q is my brother hajaenda bongo Record yupo mwanza studio yake inaitwa sheydon record
 
Q niliskia alienda bongo record......dunga yuko kwao Kenya si unajua bongo majungu mengi ilibidi jamaa asepe
Q the Don alitoka Bongo Records around 2009 hii Ni baada ya kutoa CCN ya mangwair wakishirikiana Na Paul. Kuna kipindi alitaka kuleta bifu Na dogo Lamar ambapo ndipo ikawa amsha amsha zake. But he's very talented man. Dunga yupi Kenya kwao.
 
Mkuu imekuaje Bizman hajatajwa kwenye list yako pamoja na kuwakumbuka wengi
Bizzman kipindi hicho sometimes alikua Bamaga pale kwa majani akipiga vinanda akiwa Na Prof Ludigo rejea ngoma ya Mangwair Mikasi. Beat alitengeneza Ludigo kinanda Bizzman production Bongo Records
 
kipindi bonny luv alipika ngoma fikirishi sana `ingekuwa vip? ya mwana fa,dot.com ya dknob producer simkumbuki enzi zile ila kwa sasa huyu nahreal anatisha xaana
 
Ngoma ilikuwa Perfume.
 
Mkuu kuna producer mmoja ndio alikuwa hapo Heartbeat Records kwa Chuchu na alitengeneza nyimbo za Dada mmoja V2 na ile ya Banana Zorro "Naamini Kama Kweli Wanipenda" alikuwa ni nani? Nadhani pia alishafanya kwenye studio ya JaG Records ya JayDee na Gardner.
 
Nimemkumbuka Huyo jamaa ni Alain Mapigo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…