Tujikumbushe Maproducer wakali wa zamani

Tujikumbushe Maproducer wakali wa zamani

Roy alikuwa mtundu sana.

Nakumbuka 1999 Raha Towers tumeenda kwenye internet cafe ya Raha.com pale, basi kachukua computer kaifanyia utundu niliokuwa siujui siku hizo, akaibadilisha keyboard ya computer kiwa jeyboard ya kupigia muziki.

Salute.

Kama nakumbuka hii stori.
 
...kulikuwa na producer anaitwa Effector kutoka studio ya Serious Record,sijui kapotelea wapi jamaa. Aliproduce ngoma kama Kazi pesa Matanuzi ya Snare ft. AY na Buff G,akatoa Itikadi Zetu ya East Coast Team (ECT) na nyinginezo....nakumbuka ndipo dogo Stan Boy alipojulikana enzi zile katka chorus za ECT huku akitoa ngoma akitoa zake kama Sweet Girl nk. Nimemkumbuka baada ya kuisikiliza ngoma ya AY ft Stan Boy - mademu watafutaji ambayo.ni mkono wa Effector....

Kupotea kwa huyu jamaa, katika game kuliniumiza sana, kwanza ilikua ni ghafla na ndio ilikua hazina ya ECT. Alimmudu GK vizuri. Na nadhani kati ya maproducer wazuri mbali na Master Jay, walioweza kummudu GK ni yeye.
 
Roy alikuwa mtundu sana.

Nakumbuka 1999 Raha Towers tumeenda kwenye internet cafe ya Raha.com pale, basi kachukua computer kaifanyia utundu niliokuwa siujui siku hizo, akaibadilisha keyboard ya computer kiwa jeyboard ya kupigia muziki.

Salute.
Kumbe Kiranga na viranga vyako bado mtoto mdogo hivyo? Ma comments yako yalinifanya nikufikirie wewe ni mbabu aliye stow away in the 70s kabla hata Kishtobe haijaanza ku dock pale Dar port ( jokingly)
One love no offense intended ;-) ;-) ;-)
 
Hivi Producer Q yuko wapi? dunga wa mandugu digital pia hasikiki sasa hivi
Q niliskia alienda bongo record......dunga yuko kwao Kenya si unajua bongo majungu mengi ilibidi jamaa asepe
 
Kuna kichwa kama Ambha wa iringa, D money wa Downtown records
 
Kama kweli unathamini na kutoa shukurani,nafikri si busara kuwa kimbilia waakina p funk na kuwasahau bon luv na enrico,
 
Bonny Luv- Mawingu Studio.
Amit Mento- Agies Record
Miika Mwamba- Fm Studio
Roy Bukuku - G Records.
Akili The Brain- Akili Records
P. Funk Majani- Bongo Records
Master Jay- Mj Records
Joshua Kameta - Kameta Studio
Said Comorien- Metro Studio
Enrico - Soundcrafters

Lakini kuna maproducers walipita katika studio hizi katika vipindi tofauti kama Marlon Linje, Marijani,Prof. Ludigo, Castro Ponela, na John Mahundi. Pia kuna wanamuziki walijaribu kuproduce kwa kipindi flani kama Marehemu Complex,Bodea na Soggy Dog Hunter.

Ila kuna Kizazi cha mwisho cha maproducer kabla hawajawa wengi kama mchele na studio kuongezeka kama bar za Sinza.... Hawa ni kama
Marco Chali wa Kama kawa Records. Dunga, producer Jonas (ukisikiliza ngoma za wakali kwanza utamsikia anatajwa), Downtown Records, Pasu kwa Pasu Records, na Active Record ya Producers Shakii toka kenya.

Hizo zote ilikuwa kabla ya 2008... Enzi hizi kila msanii lazima uje Dar ufuate studio nzuri....labda uende Zanzibar kulikuwa na Jupiter Records na Chuchu na studio yake ya Heartbeats Records.
Mkuu imekuaje Bizman hajatajwa kwenye list yako pamoja na kuwakumbuka wengi
 
Jamaa Q is my brother hajaenda bongo Record yupo mwanza studio yake inaitwa sheydon record
 
Q niliskia alienda bongo record......dunga yuko kwao Kenya si unajua bongo majungu mengi ilibidi jamaa asepe
Q the Don alitoka Bongo Records around 2009 hii Ni baada ya kutoa CCN ya mangwair wakishirikiana Na Paul. Kuna kipindi alitaka kuleta bifu Na dogo Lamar ambapo ndipo ikawa amsha amsha zake. But he's very talented man. Dunga yupi Kenya kwao.
 
Mkuu imekuaje Bizman hajatajwa kwenye list yako pamoja na kuwakumbuka wengi
Bizzman kipindi hicho sometimes alikua Bamaga pale kwa majani akipiga vinanda akiwa Na Prof Ludigo rejea ngoma ya Mangwair Mikasi. Beat alitengeneza Ludigo kinanda Bizzman production Bongo Records
 
kipindi bonny luv alipika ngoma fikirishi sana `ingekuwa vip? ya mwana fa,dot.com ya dknob producer simkumbuki enzi zile ila kwa sasa huyu nahreal anatisha xaana
 
Producer jonas alitolewa pale Tanzania regions na jamaa mmoja anaitwa lobi kwenda kuanzisha MID MAN Records pale faya na baadae wakahamia mwenge. Wakati wapo kwenye majaribio wakaona wamchukue kijana mmoja kwa ajili ya majaribio!! Wakamchukua josselin pale faya na ngoma yake ya kwanza tu ikamtoa ngoma flani ilikua inaitwa mshkaji flani kama sikosei. JONAS alikua anakuja vizur sana ila mwenye studio akaifunga na na JONAS akapotea sijui yuko wapi sasa
Ngoma ilikuwa Perfume.
 
Bonny Luv- Mawingu Studio.
Amit Mento- Agies Record
Miika Mwamba- Fm Studio
Roy Bukuku - G Records.
Akili The Brain- Akili Records
P. Funk Majani- Bongo Records
Master Jay- Mj Records
Joshua Kameta - Kameta Studio
Said Comorien- Metro Studio
Enrico - Soundcrafters

Lakini kuna maproducers walipita katika studio hizi katika vipindi tofauti kama Marlon Linje, Marijani,Prof. Ludigo, Castro Ponela, na John Mahundi. Pia kuna wanamuziki walijaribu kuproduce kwa kipindi flani kama Marehemu Complex,Bodea na Soggy Dog Hunter.

Ila kuna Kizazi cha mwisho cha maproducer kabla hawajawa wengi kama mchele na studio kuongezeka kama bar za Sinza.... Hawa ni kama
Marco Chali wa Kama kawa Records. Dunga, producer Jonas (ukisikiliza ngoma za wakali kwanza utamsikia anatajwa), Downtown Records, Pasu kwa Pasu Records, na Active Record ya Producers Shakii toka kenya.

Hizo zote ilikuwa kßabla ya 2008... Enzi hizi kila msanii lazima uje Dar ufuate studio nzuri....labda uende Zanzibar kulikuwa na Jupiter Records na Chuchu na studio yake ya Heartbeats Records.
Mkuu kuna producer mmoja ndio alikuwa hapo Heartbeat Records kwa Chuchu na alitengeneza nyimbo za Dada mmoja V2 na ile ya Banana Zorro "Naamini Kama Kweli Wanipenda" alikuwa ni nani? Nadhani pia alishafanya kwenye studio ya JaG Records ya JayDee na Gardner.
 
Nimemkumbuka Huyo jamaa ni Alain Mapigo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom