figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,479
Desemba 2, 1995:
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilitumia askari wa Jeshi la Wananchi na polisi kusimamia zoezi la kuharibu ngano ya mfanyabiashara maarufu nchini, Bw. Said Bakhresa. Ngano hiyo inakisiwa kufikia tani 3,800. Zoezi hilo lilifanyika huku kukiwa na amri ya muda ya mahakama inayozuia kuharibiwa kwa ngano hiyo hadi kesi iliyofunguliwa na mahakamani na Bw. Bakhresa dhidi ya Jiji itakaposikilizwa.
Desemba 7, 1995:
Watu 10 wafariki, 42, wajeruhiwa baada ya basi la Shirika la Posta nchini, SU 31644 kupinduka kati ya vijiji vya Mtyangimbole na Gumbiro kilometa 40 kutoka mjini Songea katika barabara ya kwenda Njombe.
Januari 9, 1996:
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Hali ya Hewa, Dk. Mohamed Mhita atangaza Tanzania kukumbwa na ukame kutokana na kuchelewa kunyesha kwa mvua za vuli. Alisema mkondo ambao ulikuwa ukileta mvua katika ukanda wa Tanzania umebadili mwelekeo.
Januari 16, 1996:
Watu 17 wafariki kwa ajali ya basi la Abood Service lenye Na. TZB 5534 lililokuwa likitokea eneo la Bwawani, mkoani Morogoro.
Januari 30, 1996:
Mkurugenzi wa Idara ya Uslama wa Taifa, Imrani Kombe auawa akitokea mjini Moshi kwenda nyumbani kwake maili sita wilayani Hai.
Mei 21, 1996:
Watu wanaokisiwa kuwa 948 walikufa kufuatia kuzama kwa meli ya MV Bukoba waliyokuwa wakisafiria kutoka Bukoba kwenda Mwanza.
Agosti 1, 1996:
Wachimbani wa madini 12 wafukiwa wakiwa hai kwenye migodi ya Bulyamhulu, wilayani Kahama.
Desemba 27, 1996:
Watu kadhaa wafariki kufuatia ajali ya basi la Air iliyotokea eno la Kilimanjaro Machame, Moshi.
1996:
Njaa yaikumba mikoa ya kusini hadi wananchi wa Kilwa wafikia kula majani.
Januari 9, 1997:
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Hali ya Hewa, Dk Mohamed Mhita atangaza Tanzania kukumbwa na ukame kutokana na kuchelewa kunyesha kwa mvua za vuli. Alisema mkondo ambao ulikuwa ukileta mvua katika ukanda wa Tanzania umebadili mwelekeo.
Januari 17, 1997:
Mbunge wa Morogoro Kaskazini, Prof. Nicas Mahinda auawa na majambazi nyumbani kwake Kunduchi Mtongani.
Januari 10, 1997:
Moto mkubwa wazuka na kuteketeza eneo kubwa la msitu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).
Januari 29, 1997:
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Brigedia Hassan Ngwilizi atangaza ugonjwa wa kipindupindu walikumba Jiji la Dar es Salaam na hadi siku hiyo watu 8 walikuwa wamefariki na watu 61 kulazwa Hospitalini.
Januari 30, 1997:
Akihutubia kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya, Rais Benjamini Mkapa akanusha watu kufukiwa Bulyanhulu na kuagiza utaratibu wa kisheria dhidi ya wote waliotoa habari hizo katika vyombo vya habari wafikishwe mahakamani.
Februari 7, 1997:
Serikali yatangaza kwamba ugonjwa wa malaria waikumba wilaya ya Korogwe, mkoa wa Tanga na kuua watu 36.
Machi 12, 1997:
Waziri Mkuu, Frederick Sumaye aagiza jeshi la polisi Jijini kukamata na kuwafungulia mashitaka watu wanaomwagilia bustani, mboga kwa kutumia maji ya bomba.
Machi, 13, 1997:
Watu saba wafariki baada ya kufukiwa na udongo kwenye mgodi wa kuchimba marumaru ulioko kijiji cha Moivaro, wilaya ya Arumeru, Arusha. Pamoja nao, pia lori tani saba aina ya Isuzu lenye Na. ARJ 583 mali ya kikosi cha kuzuia ujangili Arusha lilifukiwa kabisa bila kuonekana.
Machi 25, 1997:
Mwanzo wa mvua za maafa za El-Nino.
Agosti 13, 1997:
Watu 14 wafariki na 31 wajeruhiwa vibaya baada ya mabasi matatu kugongana katika eneo la Kingolwira, mkoani Morogoro. Mabasi hayo ni No.Challenge Na. Ta TZJ 1958, lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Singida, basi la Safina Na. TZJ 2658 na basi la Abood TZK Na. 3812.
Octoba 28, 2015
Edward Lowassa ajitangaza mshindi. Alisema amepata jumla ya KURA milion 10,268,795 sawa na 62%. Aliitaka Tume kumtangaza yeye ndiye mshindi mara moja.
Ajali Treni Dodoma mwaka 2002
Tuendelee kujikumbusha Matukio ya Nchini mwetu ambayo hayawezi kusahaulika kirahisi. Naomba uongezee ili kuweka kumbukumbu sawa. Usisahau kuweka Mwaka.
Karibuni.