bukoba boy
JF-Expert Member
- Jan 15, 2015
- 5,370
- 3,956
Wengi wetu tz tuko familiar na ule mchezo wa kwenye bodi unaoitwa DRAFT ,sasa huu mchezo wa chess,bodi(board) yake imefanana vilevile na draft ila lenyewe halitumii mfumo wa mainroad..
Draft halina aina za michezo inayozidi mitano sababu kete zote zinaenda kwa hatua moja diagonally.
Chess ndio mchezo mtamu sababu kila kete inaenda kivyake na linaitaji akili nyingi hata mara 60 ya akili ya kucheza draft
Mchezo unakufundisha mbinu za vita.Kumlinda King wako na Kumwinda wa mwenzio.sio ilimradi kwenda mbele.
Chess unafanya kazi ya kumlinda King wako asikamatwe.Na huu ndio uzuri wa chess,hata kama umeliwa kete moja tu King akikamatwa(akiliwa) mchezo ushafungwa.checkmate!
Chess board liko labelled.(kama x na y) kwenye geometry.Line x(horizontal) iko labelled A-H na vertical line (y axis) 1-8.Hii inasaidia ukiulizwa umecheza wapi unaweza ukasema Knight to B7.
Huwezi kula kete zaidi ya 1,na ukila kete,kete yako inakaa pale ilipokuepo uliyoila.
King wako analindwa na walinzi(kete) wasiopungua 5,zikiwemo
1.Queen
Hii inatembea pande yeyote ile ya uwanja,lakini haiwezi kuruka chumba chenye kete.
2.Knight
Huyu sura ya kichwa cha farasi.Anatembea kwam mfumo wa herufi L.Anaweza kuruka kete nyingine.
Hii kete inaweza kupita juu ya kete zingine iwe zako au adui ila lazima atue sehemu iliyowazi,kama sio wazi basi kwenye kete ya adui na kwa kufanya hivo utakua umeila..
3.Bishop
Anatembea diagonally tu na haruki kete ingine
4.Castle au Rook
Huyu anaenda kokote ila sio diagonally na haruki kete
5.Pawn
Hizi ni kete zenye dhamani ndogo kuliko zote.zinambea hatua moja tu mbele na hula digonally.Lakini akifanikiwa akavuka kufika mstari wa kwanza ambao King anapangwa(ukiingiza king) unaongeza moja ya kete nilizotaja hapo juu,wengi huingiza Queen sababu ndio the most powerful kete.Kwa maana nyingine ni Pawn tu anaingia king kwenye chess.
Hizi kete zote zinakua katika pair,kutoa King tu ni moja.Zinapangwa katika mistari mwili ya nyuma.
Pawn pekee ndio wanapangwa mbele na hizo kete nyingine zote nyuma katika pair kama nilivosema,ukitoa King tu ndio mmoja. Na mchezo wake wa kwanza inaweza ikaruka box moja kama ukitaka..