Tujifunze kichagga (kinyumbani) hata kama tunaishi ugenini

Mar 2, 2011
86
20
LUGHA YETU UTAMADUNI WETU

Naomba nitoe wito kwa wachagga wote wanaojua kichagga watufundishe kichagga na watutengenezee mada kabisa.

Ikiwa utakuwa unafundisha Kirombo useme unachofundisha ni kirombo
Ikiwa unafundisha Kimarangu au kimachame useme unafundisha kichagga cha wapi ili kila mchagga ajue ni lugha ya mahali gani anajifunza.

Ni aibu wengi wetu tumekulia mjini afu tunajiita wachagga lakini kilugha hatukijui. Tafadhalini tusaidieni wajameni tuweze kuwa wamoja.

KARIBUNI WALIMU MTUFUNDISHE.... HATA KWA ADA.
 
na nyie nao!!! mmmmmh!
hivi ndizi mbivu kwa wachaga wa Uru wanaziitaje vileeeeee!!!!
 
sijui ni lini nchi yetu na watu wake wataacha kuzungumzia ukabila!!! sasa kama hukijui si uende huko kijijini kwenu ukajifunze, mpaka muanze kututangazia kwenya majukwaa na mitandao ya kijamii kwamba kuna wachaga mnataka kutambika!!
 
Itondo.
 
Nategemea kuanzisha darasa wewe uje na mada yako nami nikupe tafsiri.Ada itakuwepo maana hii kazi inatakiwa kufanywa na wazazi lakini wako bize.
 
sijui ni lini nchi yetu na watu wake wataacha kuzungumzia ukabila!!! sasa kama hukijui si uende huko kijijini kwenu ukajifunze, mpaka muanze kututangazia kwenya majukwaa na mitandao ya kijamii kwamba kuna wachaga mnataka kutambika!!

Kutokusema hakufuti kabila la wachagga kuwepo, wala wasukuma, wala wapare, wala wanyakyusa n.k. haya makabila yoote na mengine yapo Tanzania.... wala kujifunza kilugha cha kabila si vita wala si ukabila. Nadhani unahitaji tu uelewa mdogona tena hauhitaji kwenda shule ili kutofautisha ukabila na lugha za kikabila (makabila). Kuwa makini na ukabila wako unapoutamka.... vinginevyo nitakutafsiri kwamba hujui ulichokitamka maana yake nini..!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom