Sivan
JF-Expert Member
- Jul 17, 2020
- 923
- 1,232
Jamaa kayumba sana pale eti uende kwenye gari malatatu kupelela tikitimaji yaani hayo matikiti yamaana sana.Hata mimi ndio niliwaza kama wewe.
Ile concept aliyoitoa mtoa mada ipo kinyume.
Yaani mteja anayechukua bidhaa nyingi ndio umkomoe kwa kumuongezea bei sasa mteja gani ni mjinga atakayekubali kuchukua vitu vingi kwa bei iliyozidi thamani halisi.
Na ile ya mteja kusema achukue bidhaa moja apeleke kwenye gari arudi tena mpaka mara 3 ni nani atakubali huu usumbufu kwani hakuna wafanyabiashara wengine kama wewe.
Labda kama mkoa mzima matikiti unauza peje yako hapo sawa lkn kama kuna wauzaji wengine inakula kwako.
Na ile concept ya 2 ya kusema mchina ameleta magari kama yako na akauza kwa bei ya chini halafu mkurugenzi akashauri kwamba wazidi kuongeza bei bado practically haiwezi kufanikisha.
Nasema haiwezi kufanikisha kwa sababu utawapata watu wachache ambao hawajui kutofautisha kitu bora na kisicho bora.
Ila wale wenye uwezo wa kutofautisha bidhaa bora na isiyo bora hautawapata kwenye ule mtego.
Na pia wale ambao hawajui kutofautisha utawapata siku za mwanzoni ila wakishaanza kutumia na kujua kwamba zile gari za kampuni zote mbili ni sawa wataambiana na hutawaona tena.
Kafosi sana kuwa applicable.