Tujifunze biashara kidogo

Tujifunze biashara kidogo

Aizi Azma

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
553
Reaction score
1,151
Haya mambo sidhani kama yanafundishwa darasani. Hii ni street knowledge, real life situations ambazo zinatufunza mengi. Sasa kuna matukio mawili hapa ya kibiashara, naomba mwenye jibu la mojawapo au yote anipe.

1. MOJA TZS 3,000/=, MATATU TZS 10,000/=.
Mzee mmoja pale Magomeni Mapipa anauza matikiti maji. Tikiti moja anauza kwa TZS 3,000/=, matatu anauza kwa TZS 10,000/=. Mchana wa leo akapita kijana pale, akanunua tikiti la kwanza, akalipa TZS 3,000/=. Akanunua jingine tena, akalipeleka kwenye gari lake, akalipa TZS 3,000/=. Akarudi tena, akanunua tikiti la tatu, akalipa TZS 3,000/= halafu akamwambia yule mzee,''Ivo we mzee umeona? Nimenunua matikiti matatu kwa TZS 9,000/= tu badala ya TZS 10,000/=!!! Inaonesha we mzee ni mgeni kwenye masuala ya biashara eh?!?!?"

Wakati yule kijana anaondoka na gari lake, mzee akajisemea huku anacheka,"Watu bwana, yaani mtu amenunua matikiti matatu lakini bado anataka anifundishe masuala ya biashara! Hahahaha!!"

SWALI: Kwanini mzee ameweka bei zake kwa mtindo huu? Je, ni kweli mzee hajui biashara? Fafanua.

2. TUONGEZE BEI ILI KUSHINDANA NAO!
Kampuni moja ya magari nchini Ujerumani ilikuwa inafahamika kwa kutengeneza magari ya kifahari yanayouzwa ghali sana. Ghafla ikaibuka kampuni nyingine ya Kichina inayotengeneza magari kama yale ya Ujerumani, lakini wao sasa wanauza kwa bei ambayo ni nusu ya ile ya magari ya Ujerumani.

Kuona hivyo, meneja mauzo wa ile kampuni ya Kijerumani akamfuata Mkurugenzi wake ili kumweleza kuhusu ujio wa hii kampuni mpya inayotengeneza magari kama ya kwao na kuyauza kwa bei chee.

Meneja mauzo akamuuliza Mkurugenzi wake,"Tunafanyaje sasa kukabiliana nao sokoni?". Mkurugenzi akajibu,"Tuongeze bei ya magari yetu!"

SWALI: Kwanini mkurugenzi anafikiri kuongeza bei ya magari yao ndio njia bora ya kushindana sokoni? Fafanua.

NB: Kwa ambae yuko interested na tricks kama hizi, unaweza kuupitia uzi huu pia; GROWTH HACKING

#virus
 
Kuna kitu kidogo hapo. Kuna kitu kinaitwa PSYCHOLOGICAL PRICING kwa sisi tuliosomea kozi moja mbili za Marketing hiyo ni mojawapo ya pricing techniques.

Kwenye biashara ya mzee ya matikiti, kijana amekwenda na idea ya kumkomoa mzee lakini amejikomoa mwenyewe. Bei ya tikiti ni 3,000 ina maana anayenunua matatu anatakiwa alipe 9,000/- tu. Ila psychology aliyoiweka mzee ni kuwa ukinunua matatu ulipe elfu 10. Lengo ni nini? Ili wewe uone kuwa unafaidi, badala ya moja utanunua moja moja mara 3 na kulipa elfu 9 ukidhani umesave 1000 ila kimsingi mzee kauze large quantity kwa bei ile ile inayotakiwa.

Hii psychological pricing ndio ile unaambiwa simu inauzwa 299,999 hehehehe hiyo ni laki 3 jombaa. Ila unaitamkaje?

Tuje kwenye magari. Kuna kitu kinaitwa PREMIUM PRICING.
In simple words maana yake ni charging more for your products than your immediate competitors. Let me explain it in English nadhani ndio utanielewa zaidi. Kimalkia kina raha yake banah.

Premium pricing is a strategy that involves tactically pricing your company’s product higher than your immediate competitors. But why so? The purpose is to cultivate a sense in the market of your product being just that bit HIGHER IN QUALITY than the rest. It works best alongside a coordinated marketing strategy designed to enhance that perception.

Yep, lengo ni kuwajengea imani wateja kuwa bidhaa yako ndio bora zaidi na hivyo inastahili bei hiyo. Na uzuri wa technique hii ni kuwa kuna wateja wake maalum wa vitu vya bei mbaya, sababu they believe in quality. Yaani umuambie anunue bidhaa za Mohamed (code) akuelewi kabisa, ndio maana akitaka energy drink ataulizia Redbull. Ndio maana kuna whitedent na colgate, colgate ni ghali ila bado inauza. Above them kuna Sensodyne (not sure kama nimeandika vizuri Sensodyne). Ndio maana kuna Toyota na BMW.

Faida ya premium pricing ni kuwa (a)inafanya kampuni ipate faida kubwa sana. Hata mkiuza chache mtapiga hela ndefu sababu kuna margin kubwa.

b) Inaongeza brand value na perception nzuri ya kampuni yako kwa wateja.

Ubaya ni kwamba technique hii si nzuri kwa mass market. Yaani si kila mtu atamudu so kunakuwa na low sales volume.
 
Kwenye biashara ya mzee ya matikiti...kijana amekwenda na idea ya kumkomoa mzee lakini amejikomoa mwenyewe. Bei ya tikiti ni 3,000 ina maana anayenunua matatu anatakiwa alipe 9,000/- tu. Ila psychology aliyoiweka mzee ni kuwa ukinunua matatu ulipe elfu 10. Lengo ni nini? Ili wewe uone kuwa unafaidi, badala ya moja utanunua moja moja mara 3 na kulipa elfu 9 ukidhani umesave 1000 ila kimsingi mzee kauze large quantity kwa bei ile ile inayotakiwa...
UKO VIZURI HAKIKA UMEWEZA KUFAFANUA VEMA
 
Nilikuwaga na duka la nguo Dodoma nilicho kuwa nakifanya nikienda kufunga mzigo let say jins 50 basi nazigawa nusu kwa nusu harafu nazipa bei tofaut kundi la kwanza nitaziuza bei nusu ya elf 25 na kuziita copy na kundi la nitaziuza 45 na kuziita original hivyo mteja ataangalia quality yake na kuchagua inayo mfaa
 
Umemaliza mkuu NO COMMENT.
Premium pricing is a strategy that involves tactically pricing your company’s product higher than your immediate competitors. But why so? The purpose is to cultivate a sense in the market of your product being just that bit HIGHER IN QUALITY than the rest. It works best alongside a coordinated marketing strategy designed to enhance that perception...
 
Katika biashara cha muhimu ni kuwa na wateja wengi na sio kupata faida kubwa mfano wa biashara ya magari kampuni ya ujerumani itapata faida kwa kuuza gari mojamoja lakini itakuwa na wateja wachache lakini kampuni ya china itapata faida kubwa zaidi kwani mbali ya magari yao kupata faida ndogo watakuwa na wateja wengi watakaowaingizia faida kubwa na magari yao hayatakaa sokoni muda mrefu
 
Hapo kwa mzee amepwaya hiyo psychology ya kuuza ila hawafanyi hivyo.

Ni inakuwa kama mfano moja 3000, basi matatu 8000 | hapo ndipo ilipo pyschological convincing ya mteja kiona nita save 1000 nikichukua matatu ila kwa mfano ulioweka mzee hakuna anayefanya hivyo umeufosi.
 
Kuna kitu kidogo hapo. Kuna kitu kinaitwa PSYCHOLOGICAL PRICING kwa sisi tuliosomea kozi moja mbili za Marketing hiyo ni mojawapo ya pricing techniques.

Kwenye biashara ya mzee ya matikiti, kijana amekwenda na idea ya kumkomoa mzee lakini amejikomoa mwenyewe. Bei ya tikiti ni 3,000 ina maana anayenunua matatu anatakiwa alipe 9,000/- tu. Ila psychology aliyoiweka mzee ni kuwa ukinunua matatu ulipe elfu 10. Lengo ni nini? Ili wewe uone kuwa unafaidi, badala ya moja utanunua moja moja mara 3 na kulipa elfu 9 ukidhani umesave 1000 ila kimsingi mzee kauze large quantity kwa bei ile ile inayotakiwa.

Hii psychological pricing ndio ile unaambiwa simu inauzwa 299,999 hehehehe hiyo ni laki 3 jombaa. Ila unaitamkaje?

Tuje kwenye magari. Kuna kitu kinaitwa PREMIUM PRICING.
In simple words maana yake ni charging more for your products than your immediate competitors. Let me explain it in English nadhani ndio utanielewa zaidi. Kimalkia kina raha yake banah.

Premium pricing is a strategy that involves tactically pricing your company’s product higher than your immediate competitors. But why so? The purpose is to cultivate a sense in the market of your product being just that bit HIGHER IN QUALITY than the rest. It works best alongside a coordinated marketing strategy designed to enhance that perception.

Yep, lengo ni kuwajengea imani wateja kuwa bidhaa yako ndio bora zaidi na hivyo inastahili bei hiyo. Na uzuri wa technique hii ni kuwa kuna wateja wake maalum wa vitu vya bei mbaya, sababu they believe in quality. Yaani umuambie anunue bidhaa za Mohamed (code) akuelewi kabisa, ndio maana akitaka energy drink ataulizia Redbull. Ndio maana kuna whitedent na colgate, colgate ni ghali ila bado inauza. Above them kuna Sensodyne (not sure kama nimeandika vizuri Sensodyne). Ndio maana kuna Toyota na BMW.

Faida ya premium pricing ni kuwa (a)inafanya kampuni ipate faida kubwa sana. Hata mkiuza chache mtapiga hela ndefu sababu kuna margin kubwa.

b) Inaongeza brand value na perception nzuri ya kampuni yako kwa wateja.

Ubaya ni kwamba technique hii si nzuri kwa mass market. Yaani si kila mtu atamudu so kunakuwa na low sales volume.
Mkuu una masters ya Business Management au ts just street smart!?!?!? Umetoa jibu ambalo ni the best ever.
 
Hapo kwa mzee amepwaya hiyo psychology ya kuuza ila hawafanyi hivyo.

Ni inakuwa kama mfano moja 3000, basi matatu 8000 | hapo ndipo ilipo pyschological convincing ya mteja kiona nita save 100 nikichukua matatu ila kwa mfano ulioweka mzee hakuna anayefanya hivyo umeufosi.
Ila jamaa hapo juu nimemuelewa vyema zaidi
 
Hapo kwa mzee amepwaya hiyo psychology ya kuuza ila hawafanyi hivyo.

Ni inakuwa kama mfano moja 3000, basi matatu 8000 | hapo ndipo ilipo pyschological convincing ya mteja kiona nita save 100 nikichukua matatu ila kwa mfano ulioweka mzee hakuna anayefanya hivyo umeufosi.
Hahaha... wapo wengi wanaofanya hivyo mkuu, pita madukani utaona. Here is the thing though, huwezi kuona kama huna jicho la Kibiashara. Lengo la mzee ni kukufanya uone unamkomoa yeye wakati ni yeye ndiye ameku-fosi ununue bidhaa nyingi zaidi badala ya moja!!!
 
Nilikuwaga na duka la nguo Dodoma nilicho kuwa nakifanya nikienda kufunga mzigo let say jins 50 basi nazigawa nusu kwa nusu harafu nazipa bei tofaut kundi la kwanza nitaziuza bei nusu ya elf 25 na kuziita copy na kundi la nitaziuza 45 na kuziita original hivyo mteja ataangalia quality yake na kuchagua inayo mfaa
Brilliant! Ivi nyie watu kwanini hamteuliwi kuwa mawaziri wa biashara?!! (*Najaribu kuwaza kwa sauti ni nini kingetokea kama watu ambao wako smart kama hivi wangekuwa kwenye system.)
 
Kuna kitu kidogo hapo. Kuna kitu kinaitwa PSYCHOLOGICAL PRICING kwa sisi tuliosomea kozi moja mbili za Marketing hiyo ni mojawapo ya pricing techniques.

Kwenye biashara ya mzee ya matikiti, kijana amekwenda na idea ya kumkomoa mzee lakini amejikomoa mwenyewe. Bei ya tikiti ni 3,000 ina maana anayenunua matatu anatakiwa alipe 9,000/- tu. Ila psychology aliyoiweka mzee ni kuwa ukinunua matatu ulipe elfu 10. Lengo ni nini? Ili wewe uone kuwa unafaidi, badala ya moja utanunua moja moja mara 3 na kulipa elfu 9 ukidhani umesave 1000 ila kimsingi mzee kauze large quantity kwa bei ile ile inayotakiwa.

Hii psychological pricing ndio ile unaambiwa simu inauzwa 299,999 hehehehe hiyo ni laki 3 jombaa. Ila unaitamkaje?

Tuje kwenye magari. Kuna kitu kinaitwa PREMIUM PRICING.
In simple words maana yake ni charging more for your products than your immediate competitors. Let me explain it in English nadhani ndio utanielewa zaidi. Kimalkia kina raha yake banah.

Premium pricing is a strategy that involves tactically pricing your company’s product higher than your immediate competitors. But why so? The purpose is to cultivate a sense in the market of your product being just that bit HIGHER IN QUALITY than the rest. It works best alongside a coordinated marketing strategy designed to enhance that perception.

Yep, lengo ni kuwajengea imani wateja kuwa bidhaa yako ndio bora zaidi na hivyo inastahili bei hiyo. Na uzuri wa technique hii ni kuwa kuna wateja wake maalum wa vitu vya bei mbaya, sababu they believe in quality. Yaani umuambie anunue bidhaa za Mohamed (code) akuelewi kabisa, ndio maana akitaka energy drink ataulizia Redbull. Ndio maana kuna whitedent na colgate, colgate ni ghali ila bado inauza. Above them kuna Sensodyne (not sure kama nimeandika vizuri Sensodyne). Ndio maana kuna Toyota na BMW.

Faida ya premium pricing ni kuwa (a)inafanya kampuni ipate faida kubwa sana. Hata mkiuza chache mtapiga hela ndefu sababu kuna margin kubwa.

b) Inaongeza brand value na perception nzuri ya kampuni yako kwa wateja.

Ubaya ni kwamba technique hii si nzuri kwa mass market. Yaani si kila mtu atamudu so kunakuwa na low sales volume.
La pili umeeleza vizuri lakini la kwanza sidhani. pyschological pricing ni ile inayokufanya uamini kuwa unanunua kitu kwa bei rahisi kumbe hakuna unafuu mkubwa. Mfano uliotoa wa bei ya 100,000 kuandikwa kama 299,999 hiyo ndiyo psychological pricing. Ila kwenye huo mfano wa tikiti kwangu hai-make sense kwenye psychological pricing. Hii ya tikiti nadhani maelezo yake yangekuwa ukinunua moja unalipa 3000 na ukinunua matatu unalipa 8000. Hiyo ndiyo itafanya watu wanunue kwa sababu ya punguzo la elfu.
 
Sales is an art mjombaa. Na katika sanaa hakuna mbinu moja ya kucreate psychology ya wateja. Katika kuuza kila mtu ana usanii wake wa kuihadhiri hadhira yake ili lengo lake litimie. Hivi unadhani kwanini mzee kaongeza bei?
Sales sio science kusema kwamba 2x2 jibu ni 4 au ukichanganya acid na base unapata chumvi na maji.

Hiyo unayosema wewe ni discount kabisa....nayo ni technique mojawapo.
 
Ni kweli lakini kwa mfano wa tikiti mhh.. outcome yake inaweza kuwa negative.
 
La pili umeeleza vizuri lakini la kwanza sidhani. pyschological pricing ni ile inayokufanya uamini kuwa unanunua kitu kwa bei rahisi kumbe hakuna unafuu mkubwa. Mfano uliotoa wa bei ya 100,000 kuandikwa kama 299,999 hiyo ndiyo psychological pricing. Ila kwenye huo mfano wa tikiti kwangu hai-make sense kwenye psychological pricing. Hii ya tikiti nadhani maelezo yake yangekuwa ukinunua moja unalipa 3000 na ukinunua matatu unalipa 8000. Hiyo ndiyo itafanya watu wanunue kwa sababu ya punguzo la elfu.
Mzee kaweka hivo ili watu kama nyie mfanye kama huyo kijana alienunua kumkomoa muuzaji

Kumbe yeye anajua watu mtajifanya wajanja kwa kwenda mara 3 na kununua tikiti moj moja ili kumkomoa

Kumbe yeye tayari anakuwa ameuza tikiti tatu badala ya moja

Upo?
 
Are you jerking my bobber son? Sipo kabisa. Na sidhani kuna mtu, dunia ya leo anayenunua bidhaa kwa kumkomoa muuzaji. Watu wanafuata unafuu na quality na siyo kukomoa. Hiyo trick itakuwa na negative outcome kwa muuzaji!
 
Hapo kwa mzee amepwaya hiyo psychology ya kuuza ila hawafanyi hivyo.

Ni inakuwa kama mfano moja 3000, basi matatu 8000 | hapo ndipo ilipo pyschological convincing ya mteja kiona nita save 1000 nikichukua matatu ila kwa mfano ulioweka mzee hakuna anayefanya hivyo umeufosi.
Hata mimi ndio niliwaza kama wewe.
Ile concept aliyoitoa mtoa mada ipo kinyume.

Yaani mteja anayechukua bidhaa nyingi ndio umkomoe kwa kumuongezea bei sasa mteja gani ni mjinga atakayekubali kuchukua vitu vingi kwa bei iliyozidi thamani halisi.

Na ile ya mteja kusema achukue bidhaa moja apeleke kwenye gari arudi tena mpaka mara 3 ni nani atakubali huu usumbufu kwani hakuna wafanyabiashara wengine kama wewe.
Labda kama mkoa mzima matikiti unauza peje yako hapo sawa lkn kama kuna wauzaji wengine inakula kwako.

Na ile concept ya 2 ya kusema mchina ameleta magari kama yako na akauza kwa bei ya chini halafu mkurugenzi akashauri kwamba wazidi kuongeza bei bado practically haiwezi kufanikisha.

Nasema haiwezi kufanikisha kwa sababu utawapata watu wachache ambao hawajui kutofautisha kitu bora na kisicho bora.

Ila wale wenye uwezo wa kutofautisha bidhaa bora na isiyo bora hautawapata kwenye ule mtego.

Na pia wale ambao hawajui kutofautisha utawapata siku za mwanzoni ila wakishaanza kutumia na kujua kwamba zile gari za kampuni zote mbili ni sawa wataambiana na hutawaona tena.
 
Back
Top Bottom