Tujiepusha na migogoro isiyo ya lazima na nchi jirani

siyabonga

Senior Member
Jan 25, 2012
125
35
Wakuu,

Jana, Jumanne, WaZIRI Mkuu wa Kenya, Raila Odinga alitembelea jimbo lake la zamani la Langata, jijini Nairobi na kuwasihi wapiga kura wake kutulia na kusubiri maamuzi ya Supreme Court kuhusu hatma ya maombi yao kupinga ushindi wa Uhuru Kenyata. Katiba yao mpya inaruhusu kupinga Mahakamani matokeo ya Urais.

Katika Mkutano huo, lilitolewa pia angalizo kwa mabalozi na wawakilishi wa Nchi mbalimbali kuheshimu Katiba ya Kenya na kuacha kufanya haraka kutoa baraka zao na kupongezana katika kipindi hiki ambacho shauri litakuwa Mahakamani mpaka hapo uamuzi utakapotolewa. Imezungumzwa kuwa huku ni kukiuka misingi ya Itifaki na Diplomasia.

Katiba yake Kenya inatoa muda wa siku saba kuwasilisha pingamizi kuhusu matokeo Mahakamani. Aidha, Supreme Court inatakiwa itoe maamuzi yake ndani ya siku 14.

Kwa kuzingatia uzito wa suala hili na taarifa ambazo zimekuwa zikiripotiwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, ni vema viongozi wetu na balozi waepuke kuingia katika mtego huu.

Tukumbuke kwamba hivi sasa bado tuna mgogoro unaofukuta na Malawi. Tutumie akili kuepuka migogoro mingine kwa ujinga tu, ushabiki au uvivu wa kufikiri. Tusitumie vichwa kufugia nywele tu!
 
Back
Top Bottom